Baharia alivyookoka kwenye mikono ya askari wa Dubai

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,045
Jana niliandika kisa kimoja cha bahari Mzee aliyezamia miaka ya 90-20s lengo likiwa kwenda Ulaya lakini hakufanikiwa aliishia kufika South America.

Sasa baada ya matatizo yote aliyopitia katika safari yake ya miaka 8 njiani alijifunza njia nyingi ili kusurvive. Na bila shaka njia nyingi zilikuwa siyo halali, ikiwemo udokozi, feymanian, utapeli n.k.

Mfano akiwa Libya walikuwa wana tabia ya kuingia kwenye maduka ya watu wanaiba mikate na vitu vingine hadi siku moja aliokoka pigwa risasi.

Basi baada ya kuzunguka sana alikuja kupata kutua Dubai in the early 2000s.
Kule akapata connection na Mpakstan flani alikuwa ana pesa mfanyabiashara mkubwa.

Jamaa anakwambia alipofika Dubai kwanza ili kuweza kuzungumza na huyo Mpakstan ilibidi aonekane naye si mtu wa mchezo aonekane naye mfanyabiashara mkubwa tu.

kwahiyo ilibidi hata hotel aliyofikia iwe na hadhi ya biashaara aliyokuwa anaenda introduce kwa huyo Mpakstan.

Kama kawaida Wapopo wako kila mahali wakifanya mambo yao, jamaa wakamconnect na mpopo mmoja ambaye kazi yake kubwa ni kuwa book in watu kwenye mahotel kwa kuhack system za hotel na yeye unampa ela kidogo tu. Jamaa akapata kukaa hotel nzuri tu.

Business yenyewe ilikuwa ni kutengeneza $$$$ kitu amabcho hakikuwa ni kweli ulikuwa ni utapeli na viini macho.

Akakutana na Mpakstan akamflash jamaa akachanganyikiwa. Jamaa anasema Mpakstan alipata moto kiasi kwamba alipiga hadi magoti mbele yake.

So akamwambia kama anahitaji kutengenezewa dollar inabdi alete usd 100,000 kwa kuanzia. Mpakstan akasema kwa sasa anaweza kutoa nusu ya hiyo pesa kwanza.

Jamaa akamwambia hakitoshi, Mpakstan akamwambia kama hakitoshi itabdi asubiri siku 5 ili ifike kiasi anachotaka. Baharia akaona siku tano nyingi akamwambia ok wataanza na hicho kiasi alichosema anacho

Mpakstan akaleta pesa na issue ilikuwa inafanyikiwa ofisini kwa huyo mpakstan. Jamaa akaomba kwanza dollar 3000 alizodai za kununulia material akapewa, akaenda eti kuandaa chemicals na makaratasi kwa ajili ya issue hiyo.

Later on akarudi then wakafanya kama inavyotakiwa kumbe mpakstan pesa jamaa ashaipiga alichomuachia pale ni makaratasi ambayo amemwambia asiyafungue chemical process itake place atakuja yafungua siku ya tatu mwenywe na ela itakuwa ishazaana.

kama mjuavyo pesa uwa inaleta tamaa, jamaa aliondoka na dollar za Mpkastan 50000 lakini bado akawa anatamaa ya kumalizia ile 50000 nyingine, na hotel akahama akaenda hotel nyingine.

Siku ya tatu akarudi kwa Mpakstan akafungua mzigo pesa zinaonekana lakini nyeusi tii (black dollar). Eti akamwambia Mpakstan chemical imezidi kuliko kiasi cha ela itabidi amalizie ile dollar 50000 ili process ibalance.

Mpakstanu akamwambia basi kesho ataleta mzigo. Jamaa akasepa
Kesho yake akiwa kwenye hotel moja Mpakstan akampigia simu uko wapi, jamaa akamuelekeza, mpakstan akamwambia ninakuja hapo hapo nakuletea ile dollar 50000 ili twende ofsini kwangu ukamalizia ile kazi.

Jamaa akaona yes, mambo si ndiyo haya anasema akiwa kwenye ukumbe llile eneo la chini ambapo pia kuna reception, mara anaona gari la polisi linatimba na anateremka askari na yule Mpakstan.

Jamaa akajua hapa kishanuka ashashtukiwa, sasa anadai hajui kama ni Mungu au shetani aliyemsaidia.

Anasema yule Mpakstan na askari wawili wakaenda pita mlango wa nyuma, polisi wengine wakapita mlango wa kawaida wa kuingia pale reception.

Naye hakungoja akaelekea kwenye ule ule mlango akapishana nao mlangoni wale askari na kwakuwa hawakuwa wanamjua akawapita akaingia mtaani.

Mara akiwa ashafika mbali kidogo akapigiwa simu na yule Mpakstan akimuuliza yuko wapi, jamaa akamjibu ataonana naye baadae amepata homa ya ghafla.

Jamaa akawa anasisitiza waonane jamaa anamwambia jioni. Akakimbilia hotelini kwake akachukua vitu vyake, kiasi kikubwa cha ela alikuwa ashakituma kwa mchumba wake siku hiyo hiyo akaondoka Dubai.
 
Asee kuna watu ni risk takers hatari.

Mkuu hiko kisa cha mara ya kwanza sikukisoma sasa hapo inakuwaje mtu anazamia bara la ulaya halafu anafika hadi America kusini. Huko kote anaenda kutafuta nini au kuna njia ya mzunguko

Naomba unieleweshe hapo maana mimi na fahamu wengi wanapitia nadhani Egypt then wanazamia baharini wanaibukia sijui Italy
 
Wazamiaji wa miaka ya 90
 
Watu wanajilipua balaa ila ukikamatika ndiyo utajua kuwa maji kamwe hayawezi kuwa mafuta. Kuna Baharia alimpiga mtu pesa Commoro wakamkamata ilikuwa atoswe baharini bahati yake akadakwa na polisi. Commoro ukikamwatwa na polisi ukiwa mgeni bahati yako kama umefanya uhalifu wanakurudisha kwenu tu.
 
Mexico wana ku-oka kwenye moto was makaa ya mawe
 
Back
Top Bottom