SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,803
- 25,442
BAHARI YAMEZA WATU?
Kisa hiki ni cha kweli na hakijapatiwa ufumbuzi mpaka leo hii.
Hiki kisa kilianzia huko tarehe kumi na moja, mwezi wa pili mnamo mwaka 1979 ambapo marafiki watano wajenzi; Scott Moorman, Benjamin Kalam, Peter Hanchett, Patrick Woessner na Ralph Malaiakini, waliazima boti kwa ajili ya kwenda kutalii kwa starehe na kuvua samaki huko eneo lijulikanalo kama Hawaii.
Ilikuwa ni ndoto ya Scott Moorman kuishi Hawaii. Na ndoto yake hiyo ilipata msukumo zaidi baada ya kuwa mwanaume huru tangu aachane na mkewe.
Boti hiyo ambayo ilikuwa ni ya kisasa kabisa, ilikuwa na urefu wa futi 17 kwa urefu na ilikuwa na mashine ya kusukumia maji ‘85 horsepower engine’. Ndani ya boti hiyo wakapakia ‘snacks’ na vinywaji vilevile kontena liliilojazwa barafu kwa ajili ya kutunzia samaki watakaowavua.
Kwa muda huo walikuwa wakicheka na kufurahi. Walikuwa na muda mzuri. Na kila mmoja alitazamia kwenda kufurahia muda wao zaidi huko baharini.
Wakiwa wanaondoka kuanza safari yao kwenda majini, ikiwa ni majira ya saa nne asubuhi, hali ya hewa ilikuwa tulivu haswa. Upepo ulikuwa ni mdogo sana na anga lilikuwa jeupe ling’aalo kana kwamba kioo. Kila mmoja akaamini kuwa huo ulikuwa ni muda murua kabisa wa kwenda kuvua lakini baada tu ya masaa mawili tangu waache fukwe, ikiwa inakaribia mchana, hali ya hewa ikaanza kuwa mbovu kupita kiasi!
Hawakufanya uchunguzi wa hali ya hewa wala kufuatilia ripoti juu ya mabadiliko yatakayotokea ndani ya siku hiyo. Walihukumu hali ya hewa kwa kutumia macho tu kitu ambacho ni kosa kubwa kwa wasafiri wa majini. Laiti kama wangelifanya uchunguzi, basi wangejikuta wanafahamu juu ya msukumo mdogo wa hewa ambao ulikuwa unajongea kufuata Hawaii siku hiyo.
Basi katika majira hayo ya mchana, upepo ukawa mkali mno tena ukiambatana na mvua kubwa. Hata upepo huo ukasababisha mafuriko katika mji wa Hana hapo Hawaii. Ilikuwa ni dhoruba kali kuwahi kutokea kwa miaka hamsini ya karibuni! Mji ulimezwa na maji, watu wakajawa na hofu juu ya maisha yao.
Sasa kama watu waliokuwako nchi kavu walijihisi hawako salama, vipi wale walokuwa majini?
Baadhi ya meli kubwa za uvuvi zilizofanikiwa kurejea fukweni zikatoa ripoti kuwa huko baharini kulikuwa kumechafukwa mno. Wimbi la maji lilikuwa linafikia urefu wa takribani futi arobaini! Kitu ambacho kilikuwa ni hatari mno kwa boti ya wale jamaa watano, boti yenye urefu wa futi kumi na saba tu!
Ndani ya masaa, wanafamilia, baba yake Peter, kaka yake Ralph, wakaanza kutoa taarifa kwa wahusika wa uokoaji wa majini juu ya kutokuonekana kwa boti iliyowabebelea wapendwa wao. Na kwa wakati huohuo wanafamilia hao, wakaanza kusaka ufukweni kama watabahatisha kuona chochote ambacho kitawasaidia kupata habari zaidi.
Lakini wakiwa huko ufukweni wakakumbwa na kadhia ya mawimbi makubwa na hali ya hewa mbovu kabisa. Ilikuwa haiwezekani hata kuona chochote baharini. Wakazi wa karibu walipoulizwa kama wameona chochote, hakuna aliyesema ameona hata tone la jambo.
Basi siku iliyofuata, waokozi wa baharini wakaanza msako mkubwa ambao ulihusisha karibia ndege hamsini, helicopters na boti ambazo ziliweza kuzunguka zaidi ya square maili 73,000 ndani ya siku tano lakini hawakupata kitu.
Na kutokana na mabadiliko ya mkondo maji ambao unasadikika kupita eneo ambao jamaa hao walienda kuvua, iliaminika kuwa kadiri muda unavyozidi kwenda mbele, ndivyo watu hao watakavyokuwa wanaenda mbali zaidi, mbali na uokozi. Na kwa mujibu wa mmoja wa watu waliokuwa wanafanya msako huo majini, anasema kuwa hali ya hewa ilikuwa mbaya bado kiasi kwamba hata boti hiyo iliyopotea ingalikuwa hatua hamsini tu toka walipo, wasingeweza kuiona.
Kitengo cha mambo ya baharini cha San Diego nacho kikaenda mbali zaidi kwa kutuma njiwa waliofunzwa wakapate kurandaranda huko baharini kutazama lakini mpango huo nao ukafeli kutokana na ndege iliyowabeba njiwa hao kulazimika kurudi nchi kavu kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya na njiwa hao kupotelea baharini!
Baada ya siku tano za msako wa kufa na kupona, hakuna hata kitu kimoja kilichopatikana kuwasaidia, hivyo ikaaminika kuwa boti hiyo imezamia dhorubani.
Hata msako rasmi uliposimamishwa, rafiki na wanafamilia bado hawakuacha kutafuta wapendwa wao. Wakakodi ndege na boti na kuendelea kusaka pasipo kuchoka mpaka kwenye maji ya huko mbali lakini bado hakuna chochote kilichopatikana kwenye juhudi hizo. Ilikuwa ni kana kwamba bahari ilimeza boti hiyo isicheue hata kaushahidi.
Basi wanandugu na marafiki nao wakanyoosha mikono na taratibu zikafanyika kutunza kumbukumbu za watu hao waliopotea, wakiamini basi watakuwa wamejifia humo majini.
**
YANAKUJA KUZUKA MAMBO…
Watu wakiwa wameshasahau na wakiamini kuwa hamna kingine tena cha kufanya, baada ya miaka tisa, Mnamo mwaka 1988, tarehe 10 mwezi wa tisa, mwanabaiolojia wa majini, bwana John Naughton, ambaye naye alihusika kwenye msako wa awali, anakuja kuona jambo ambalo linazua mambo mengine.
Akiwa anafanya tafiti zake juu ya kobe wa kwenye maji na viota vya ndege kwenye kisiwa cha mbali kabisa kisicho na makazi ya watu, anaona mabaki ya boti fukweni. Alipoitazama vema boti hiyo, anagundua ina namba za usajili za Hawaii kitu ambacho kilikuwa si cha kawaida kwani kisiwa hicho kilikuwa mbali sana na Hawaii.
Muda mfupi mbele baada ya kufukua mabaki hayo anakuja kugundua kuwa boti huyo ilikuwa ndiyo ileile ambayo iliwabeba wale jamaa waliopotea, boti kwa jina la Sarah Joe.lakini boti hiyo haikuwa na mabaki yoyote ya kusaidia upelelezi, hakuna miili, hakuna nguo, wala notisi ya aina yoyote.
Bwana Naughton pamoja na wenzake, wakaamua kusaka kisiwa hicho kwa umakini wakiwa wanataraji huenda wakapata chochote kitu.
Basi walipotembea kwa umbali wa yadi mia moja toka pale kwenye mabaki ya boti, wakagundua kulikuwa na miti iliyofungwafungwa kutengeneza msalaba, na chini ya msalaba huo kulikuwa na kaburi lenye kina kifupi. Juu yake kulikuwa na makaratasi ya kawaida na yale ya material ya foil.
Walipofukua hapo, wakabaini mulikuwa na mifupa ya binadamu. Kwa lengo la kutoharibu mazishi hayo, watu hao wakasita kufukua zaidi. Mfupa wa taya walioubeba walipoenda kuufanyia uchunguzi, wakabaini ulikuwa ni wa mmojawao na wale jamaa waliopotea baharini, kwa jina Scott Moorman.
Hakuna mabaki mengine yoyote yaliyopatikana zaidi ya hayo. Haijulikani watu wengine wanne walipotelea au kuishilia wapi mpaka leo hii. Hata baadae utafiti zaidi ulipokuja kufanyika, mifupa mingine ilipatikana ila nayo ikabainika kuwa ya Scott Moorman tu!
SASA …
Jambo hili likazua maswali kadha wa kadha. Mosi, boti hii iliwezaje kumudu tafrani ile na mpaka kutafuta njia kwenda kwenye kisiwa cha mbali vile? Na kutokana na umbali ulipo basi, inakadiriwa boti hiyo kuchukua takribani miezi ama mwaka kabisa mpaka kufika huko kisiwani, ilikuwaje haikuonekana ingali msako ulikuwa mkubwa na kukatiza kila pande?
Alafu, kutokana na eneo ambapo boti hiyo ilikutwa, ilikuwa haiwezekani kuwapo hapo pasipo kuwekwa. Hivyo kuna swali juu ya watu hao watano kama walifika hapo salama. Kama ni hivyo, mbona Moorman amekutwa akiwa amezikwa? Walifika hapo akiwa amekufa au? Na kama ndio, hao wanne wengine wameenda wapi?
Ingawa hakuna mtu ambaye ana majibu na maswali haya lakini kuna nadharia ambayo imetokea kuaminika kuelezea tukio hili. Yasema kwamba wavuvi wa kichina waliiona boti hiyo ya Sarah Joe ikiwa inawandawanda na ndani yake kukiwa na mwili mfu wa Scott Moorman ambaye alinusurika kutupiwa majini kwa kujilaza chini wakati dhoruba inapiga.
Hivyo basi wachina hao wakamzika kwa heshima Scott, jambo hilo likithibitishwa kwa makaratasi yale yalokutwa kaburini kuwa ni utamaduni ya wachina kuweka hayo makaratasi kama imani ya kumtakia mema mfu kwenye safari yake ya mbeleni.
Na kwanini wachina hao hawakutoa taarifa? Inaaminika walikuwa wanavua kwenye eneo hilo kiharamu na hivyo wakaamua kunyamaza kwa usalama wao.
Lakini bila shaka bado maswali mengi yanabakia. Watu wale wanne wameenda wapi? Mabaki yao yamemezwa na nini? Kwanini wasionekane kwa muda wote huo wa msako mkubwa kama ule alafu baadae aje kuoneknana mmoja tena sehemu ya mbali sana?
Yote yamebakia kuwa maswali.
Sent using Jamii Forums mobile app