Rais wa kwanza wa nchi ya Ivory Coast Marehemu Felix Houphouet Boigny aliufanya mji aliozaliwa wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa ivory Coast badala ya Abidjani.Zoezi la kuufanya mji wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa Ivory Coast liliambata na matumizi makubwa ya fedha za nchi kuelekezwa Yamoussoukro kwaajili ya ujenzi wa miundombinu na maofisi ya wizara mbali mbali ambayo tayari ilikuwepo Abidjani.Uwanja wa ndege,mabarabara makubwa,mahospital na lile kanisa kubwa [ Basilica of our lady of peace of Yomoussokro] lilijengwa kwa gharama ya U$ 300 million peke yake.
Rais Jakaya M Kikwete tangu alipochaguliwa kuingia madarakani mwaka 2005 kumekuwa na juhudi kubwa sana za kuuendeleza Mji Bagamoyo kwa kutumia kodi za wananchi au kutumia mikopo au misaada.Kuna mpango wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa,kuna mpango wa kujenga bandari sijui kwanini tusijenge bandari kubwa Tanga au Lindi,kumekuwa na juhudi za chini chini za kujenga kituo cha mikutano cha kimataifa badala ya Arusha,Kumekuwa na juhudi za kujenga kijiji cha michezo badala ya ule mpango wa kukijenga sambamba na uwanja wa taifa Dar es salaam,ujenzi wa barabara nne kutokea Chalinze hadi Segera wakati barabara ipo tena tusisahau kuna sehemu nyingi Tanzania hazijawahi kuona barabara ya lami,ujenzi wa barabara msata hadi Bagamoyo.
Baba wa taifa Julius alikuwa Rais wa JMT kwa miaka 24 lakini hakuwahi kufikiria kuijenga Musoma / Butihama kwa kutumia rasilimali chache za nchi kama anavyofanya Muungwana katika kipindi kisichozidi miaka 4 tu.Najaribu kutafakari tukimpa tena miaka 5 mingine Bagamoyo itakuwaje ?.
what is wrong if we get a second international airport in Bagamoyo?
Jamani Kikwete ni mbovu kwa mengi, lakini Bagamoyo kuilinganisha na Yamousoukrou is overstretching it.
Kuhusu uwanja wa Ndege mimi sioni tatizo kama uwanja wa ndege utawekwa strategically between the northern tip of Dar and Bagamoyo, where it could serve both the North Dar crowd- Mbezi and its suburbs is developing into a city within a city and will probably make ample use of this airport-. Kitu muhimu ni kuuendesha uwanja huu with business efficiency ili ujilipie katika miaka michache.
Kwa hiyo si kila kitu kinachofanywa na Kikwete ni cha kubezwa kwa kutumia mifano ambayo hailingani. Yamoussoukrou is something else, probably up there with Gbadolite, but not Bagamoyo.
Mkuu Bluray,
Kwanini mambo yote yaanze wakati wa awamu ya Muungwana.Project zinazopelekwa Bagamoyo ni nyingi sana tena nyinge zinahamishwa kutoka mikoa mingine.Bado haingii akilini uwanja wa ndege ujengwe Bagamoyo wakati ipo mikoa mingi isiyokuwa na viwanja vya ndege.
Nimezungumzia project nyingi zinapelekwa Bagamoyo ikiwemo uwanja wa ndege lakini wachangiaji wameamua kwa makusudi kukimbilia International Airport na kuacha kujadili project nyingine.
Bagamoyo inaweza kulinganishwa na Yamoussoukro kama miradi yote itapelekwa huko na kuacha mikoa mingine mingi bila project za maana.
Jamani Kikwete ni mbovu kwa mengi, lakini Bagamoyo kuilinganisha na Yamousoukrou is overstretching it.
Kuhusu uwanja wa Ndege mimi sioni tatizo kama uwanja wa ndege utawekwa strategically between the northern tip of Dar and Bagamoyo, where it could serve both the North Dar crowd- Mbezi and its suburbs is developing into a city within a city and will probably make ample use of this airport-. Kitu muhimu ni kuuendesha uwanja huu with business efficiency ili ujilipie katika miaka michache.
Kwa hiyo si kila kitu kinachofanywa na Kikwete ni cha kubezwa kwa kutumia mifano ambayo hailingani. Yamoussoukrou is something else, probably up there with Gbadolite, but not Bagamoyo.
Mkuu Bluray,
Na heshima zote, hapo ulichoandika kinapingana kabisa na sheria za UJENZI. Mjenzi yeyote anafahamu kuwa wakati anachora na baadaye kudesign structure na mwisho kujenga, hiyo structure yake lazima iwe nzuri, imara, ifanyekazi inayotakiwa kufanya, safe na ECONOMICAL.
Bagamoyo ni mbali saana na wasafiri wa JKN Airport hawajawa wengi hadi sasa. Watu wengi watataka kulipa dola mia zaidi ili ateremkie DIA kuliko kushuka Bagamoyo. Historia inasema hivyo kwani nchi nyinyi walizojaribu kufanya huo mchezo, viwanja vya mbali vimekufa. Mfano ni Canada walipojenga uwanja kwa ajili ya Olympic. Ule uwanja watu walikuwa wakigoma kushukia kule na kulipa zaidi ili washukie karibu na mji.
Ukitaka kuona vizuri, ingia Google Earth, na baada ya DIA utaona kuna uwezekano kabisa kwa sasa kujenga HIGHWAY kuzunguka mji wa Dar. Na hii inaweza kuja hadi bandarini na hapo kupunguza magari Mandela Road (port Acc.) na kupunguza ajali na vifo pale machinjioni. Hizi RINGS ndiyo best solution kwa sasa.
Hata kama DIA ikijaonekana IFUTWE, basi ni heri tujenge kati ya KIBAHA na DAR kama Wajeruman wanavyofanya sasa kuhusu AIRPORT lao jipya ambalo litakuwa kwa ajili ya Berlin na mji wa ....... Ila hizi RINGS lazima tuanze kuzifikiria kuzijenga na lazima ziwe katika level ya real HIGHWAY yaani hamna magari kukatiza barabara.
Mwisho, kwa nini sisi huku Tabora wasituwekee LAMI kwenye landing lane? Shinyanga, Musoma nk na wanazidi kupendeleana wenyewe kwa wenyewe? Jamani ningeliandika sana ila kwa ufupi niseme kuwa "hili jambo lifanyike kwa kutumia wataalamu wa Traffic Engineering na Wachumi na si kutumia Wanasiasa na kufikiri tu kuwa watu wa Tegeta na Mwenge watafaidika wakati waweza kukuta ni wachache saaana au wanaweza kupata solution nyingine.....
Hivi Tanzania haina tena taratibu za kuwa na Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano? Kama Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano upo, inawezekanaje kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Bandari au hata Barabara ya Two-Way traffic Chalinze Segera bila kufuata huo Mpango?
Mimi naona kwamba kitu kinachotakiwa kufanywa ni Bunge lidhibiti matoleo ya fedha za Mpango kama ulivyoidhinishwa hapo mwanzoni. Rais au Waziri Mkuu au waziri yeyote hawezi kuibuka na mipango mikubwa ambayo inaathiri utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano uliokwisha idhinishwa na Bunge. Bunge liwe na Wabunge jasiri wanaoweza kupinga kuibuka kwa miradi mikubwa nje ya 5-year Plan. Ama sivyo nchi itaendeshwa shagala bagala, na mwishowe tutakwama au maendeleo ya nchi yatakuwa lop-sided.
Project gani hizi zisizo majina?
NY ina JFK na Laguardia, London ina Heathrow na Gatwick, Paris ina DeGaulle na Orly it is time the Dar metropolis gets a second airport.
Dar ndege zinatua kwa foleni tangu lini?
Mkuu Bluray,
Kwanini mambo yote yaanze wakati wa awamu ya Muungwana.Project zinazopelekwa Bagamoyo ni nyingi sana tena nyingine zinahamishwa kutoka mikoa mingine.Bado haingii akilini uwanja wa ndege ujengwe Bagamoyo wakati ipo mikoa mingi isiyokuwa na viwanja vya ndege.
Nimezungumzia project nyingi zinapelekwa Bagamoyo ikiwemo uwanja wa ndege lakini wachangiaji wameamua kwa makusudi kukimbilia International Airport na kuacha kujadili project nyingine.
Bagamoyo inaweza kulinganishwa na Yamoussoukro kama miradi yote itapelekwa huko na kuacha mikoa mingine mingi bila project za maana.
Mkuu Magezi heshima mbele,
Kuna tatizo tena kubwa sana kuliko unavyofikiri.
Kutoka Bagamoyo hadi Dar es salaam ni km 75 tu,usisahau tayari serekali iko katika hatua za mwishoza kuwalipa fidia wakaazi wa maeneo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es salaam ili kiwanja kipanuliwe.
Awamu ya tatu ya Bwana Mkapa kulikuwa na mpango wa kujenga Arusha International Airport ,lakini watanzania wengi walipinga mpango huo kwasababu Kilimanjaro International airport mpaka Arusha mjini ni km 45 tu.Mpango wa kujenga Arusha International Airport ulikuwa na msukumo wa kisiasa kutoka kwa aliyekuwa waziri mkuu F Tluway Sumaye kama ulivyo mpango wa kujenga International Airport Bagamoyo unamsukumo wa Kikwete.
Tanzania ni nchi kubwa yenye mikoa mingi swali ni kwanini International Airport isijengwe katika mikoa mingine kama Ruvuma,Mwanza,Kigoma ,Mtwara,Iringa,Lindi au Dodoma ?.Bila shaka huitaji kuwa na akili nyingi kubaini project zote zinapelekwa sehemu moja kwa kuwa mkuu wa nchi anatokea sehemu hiyo.
Tukiwaacha viongozi wetu wafanye watakavyo itatufikisha mahali kila mkoa au kanda zitafanya juhudi kubwa Rais atoke sehemu yao kwasababu atakuwa katika nafasi nzuri ya kupendelea sehemu alikotoka au aliyozaliwa.Hii hatari bila shaka utaiona muda si mrefu sana,tutaanza kuchagua viongozi si kwasababu wana sifa za kutuongoza.
idea aliyokuwa nayo mkapa awamu ya tatu ilikuwa kuachana na upanuzi wa uwanja wa ndege wa dar....na kuubakisha kuhudumia jeshi..na safari za ndani...kutoka pale uwanja wa ndege dar ingejengwa barabara ya kuunganisha na kilwa road kwenda MKURANGA ...ambapo ndipo uwanja mpya wa ndege wa safari za kimataifa ungejengwa na tayari eneo lipo na limepimwa..na mwandosya anajuwa kwani alipokuwa pale wizarani tayari walikuwa wamefikia kutenga pesa za kuwekea uzio na kufanya upembuzi yakinifu....sasa nashangaa sana kama mpango wa uwanja wa kuachana na uwanja wa dar na kuhamishia safari za kimataifa mkuranga unaachwa bila maelezo ya kutosha.....
kama taifa lazima tuwe na vipaumbele ...sasa kama kila mtu akiwa rais anakuja na vipaumbele vipya hatutafika mahali....
lazima tujuwe ....
vipaumbele tulivokubaliana ni hivi:-
-uwanja wa ndege wa kimataifa [safari za nje]-MKURANGA
-SAFARI ZA ndani na JESHI - dar airport[uwanja huu ukipanuliwa hautafaa kwa mipango ya taifa miaka 25 ijayo]
-kukamilisha uwanja wa songwe international airport
-kujenga dodoma international airport
-kujenga international airport mwanza.
-kupanua viwanja vya bukoba na kigoma
-kujenga uwanja wa ndge wa kimataifa mtwara.
BANDARI
-KUENDELEZA south corridor- kupanua bandari ya mtwara.
-kujenga miundombinu ya barabara kwenda songea ..kuunganisha na barabara ya malawi na zambia..
-daraja la umoja.
kuunganisha bandari ya mtwara kwa reli na mchuchuma...na kuunganisha kwenye kipande cha reli ya TAZARA.
north CORRIDOR
- KUIMARISHA bandari ya Tanga kama njia mbadala ya uganda na rwanda[kushindana na mombasa]..
-kujenga reli arusha - musoma
-kuimarisha reli ya voi
KATI
kujenga upya njia ya reli ya kati ili kuteka soko la rwanda,burundi , congo,etc...
-kuimarisha bandari ya dar es salaam na bandari zake kavu na za maziwa....
HIVYO NDIO VIPAUMBELE VYETU....AJE RAIS YEYOTE .....!!! ATAKAYETAKA KULETA PERSONAL INTEREST NJE YA MIPANGO YA MAENDELEO YA TAIFA YA MIAKA 25....BASI ANA LAKE JAMBO!!!
KAMA NI BAGAMOYO KWENYE MIPANGO YA MAENDELEO MIRADI ILIYOKUBALIKA NI-
barabara ya bagamoyo - msata[lengo kupumua barabara ya mrogoro]
barabara ya bagamoyo -pangani[lengo kuibua fursa za utalii wa mahoteli na mbuga ya saadani...kwenye beach ya bagamoyo hadi pangani delta....
mradi wa EPZ bagamoyo ....utaungwa mkono ba barabara hizo....na mizigo inaweza kufika toka tanga au dar[50km] kirahisi]
kuna mradi wa muda mrefu wa kuunganisha reli kuanzia UBUNGO-WAZO-BAGAMOYO....ili kuwezesha viwanda vya pembezoni mwa mji na bagamoyo kufikisha malighafi bandarini...kwa uarahisi...[lakini ukaguzi uliofanyika ulikuta wakubwa wamejigawia viwanja juu ya njia ya reli kuanzia ubungo -chuo kikuuu-mbezi -wazo- [labda njia ya kuanzia wazo hadi bagamoyo ndio ipo wazi]....mpango huu ulikuwa pia na kuunganisha reli hii maeneo ya wazo na reli ambayo ingeenda kuibua mji wa viwanda KIBAHA [pale TAMCO,NYUMBU,KEC,VALMET...etc]...pale palikuwa pawe mji mkubwa wa viwanda...MIPANGO HII MINGI IPO TANGU ENZI ZA MWALIMU...na MWINYI ...na ilitakiwa utekelezaji tu ...wala hakuhitajiki study mpya hata moja ...labda bomoa bomoa tu!!!!......
mnaweza kuhakiki taarifa hii ninayotoa na viongozi wa miaka ya nyuma .....tatizo viongozi wanaokuja wanafanya kama vile nchi haiikuwa na viongozi wala wataalamu...kila mtu akiwa anakuja na mipango yake nje ya vipaumbele vya nchi...HATUTAKAA TUENDELEEEEEEE!!!