Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Hongera nyani kwa kuchelewa kuelewa ila mimi nilijua toka August 2015
 

The drugs have kicked in[emoji1549]
 
Japo kuwa sijawahi kuwa mfuasi wao hawa jamaa kwa hili naomba niwatetee,

Nia ya Maandamano ilikuwa kuujulisha umma wa Watanzania kuwa haki Demokrasia na uhuru vinakandamizwa,
ukitazama karata zao walicheza vizuri sana sana,kwanza walitoa muda mrefu sana toka watangaze kuwa watafanya hayo maandamano yao,
Hapa ukitazama kwa nje utaona kama jamaa wamefail lakini ukweli hawajafail wameshinda sana tu,lengo lao lilikuwa kuwajulisha watanzania kuna tatizo nchini,
Serikali na Taasisi zake bila kujua au kwa kujua au kwa chuki wakaingia mkenge wa kuanza kuutangaza UKUTA kwa wiingi sana na nguvu kubwa mno kila sehemu na kila pembe ya nchi umejulikana na watu wamehoji maana ya UKUTA sasa hapo lengo na nia ya chadema imefanikiwa bila hata kuandamana,
Ingekuwa hata mimi Mbowe wala nisingeingia mtaani kwa sababu kama mashtaka waliokuwa wanataka kuyaleta kwa wananchi yamefika
Bashe aliwaambia Jamhuri inacheza ngoma ya Upinzani bila kutaka
 
Well said Ngosha,kusema ukweli watakaoendela kuwaamini CHADEMA basi wana hitilafu kwenye
Frontal lobe yao.Watu wazima Adrenaline zao zimepanda kwa mwezi mzima,leo mwishoni kabisa wanaambiwa their workdone is equal to zero.Halafu wanapewa siku 31 zingine tena,bado wamo tu,itabidi wapimwe akili kwa kweli.
 
Chadema imepoteza Identity yake (Vita dhidi ya Ufisadi).
Uimara wa Chama ni Itikadi sio wingi wa wafuasi kutokana na hamasa ya viongozi.Iko wapi NCCR ya Mrema?, iko wapi NARC ya kina Raila Odinga, kiko wapi chama cha Morgan Tsvangirai?
Uimara wa Chama sio kushika dola bali kuwa na Wafuasi wenye kuamini katika sera na itikadi.
Chadema Imeteua Katibu Mkuu nje ya mfumo wa Chama
Imeteua Mgombea Urais nje ya Mfumo wa Chama
Imeteua Mgombea Mwenza kutoka CUF
Imeteua Mgombea Uspika kutoka CCM
 
CHADEMA Wanafanya Siasa za Digitali!
 
Naiangalia kwa utofauti kidogo. Kwanza kabisa UKUTA umepata publicity ya kutosha hata kama haujafanyika. Pili, naona kuahirisha ni mtego wa kuonyesha kwa wananchi nani ana dhamira ya dhati na amani ya nchi hii. Tukumbuke kwamba dhamira ya kutumia nguvu kupitia Jeshi la Polisi ilionekana ni kubwa (iwe ni kutisha au ni kweli) hivyo mpira umehamia upande wa pili. Tusubiri tuone
 
Poleni sana.
Nyani kama viongozi wote wa dini, taasisis binafsi , mabalozi wanaweza wakakujia na kukuomba ubadilishe msimamo, ni ishara kuwa you have a right worth of being realized and are on your side! No dignitary will side with ISIS
 
Nyani kama viongozi wote wa dini, taasisis binafsi , mabalozi wanaweza wakakujia na kukuomba ubadilishe msimamo, ni ishara kuwa you have a right worth of being realized and are on your side! No dignitary will side with ISIS

Akina nani walikuJa kuwaomba UKUTA?
 
Tuliona na imani na CHADEMA unataka tuamini chama gani na kwanini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…