Bado tunazisubiri Ripoti hizi

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
413
Ilikuwa masaa, siku, na hatimaye miezi toka Mheshimiwa Reginald Mengi na baadae Mheshimiwa Harrison Mwakyembe walipotoa malalamiko dhidi ya mwenendo wa baadhi ya wafanyabiashara na wakubwa katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuhusika katika njama zilizosukwa za kuhakikisha kwamba wao wenyewe na/au familia zao, pamoja na wanasiasa kadhaa maarufu wanachafuliwa au kufupishwa maisha yao. Katika taarifa za awali wakati ule tuliarifiwa kwamba uchunguzi ulikuwa umeanza.

Kwa sasa miezi kadhaa imeshapita na sisi raia tunasubiri kupata ripoti za uchunguzi huo ili kubaini kama kweli tuhuma hizo zina msingi au ni uzushi tu. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba uchunguzi huu ni mgumu kiasi gani cha kuchukua muda wote huu? Basi angalau tupewe taarifa za awali wakati tunasubiri hizo ripoti za kina.  Ukimya huu unaondoa imani tuliyonayo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vina jukumu la kulinda raia na mali zao na vile vile kutekeleza matakwa ya kikatiba ya kuhakikisha kwamba haki ya uhai hainyang'anywi.
 
Hawana asili ya kuahidi then wakarudi . Ni wepesi wa kumkamata Mbowe na Mokiwa anaendelea kungoja wamkamate .Si wepesi wa maswala ya Watanzania hapana ila kwa CCM ni haraka .Je kuna posho kwenye vika vya uchuguzi ?
 
Kwa bahati waliotoa malalamiko na waliolalamikiwa wote wanatoka familia moja na kama ilivyo kawaida kwa familia hiyo wameamua kuyamaliza kifisadi, yaani kimya kimya wasije wakaumbuana. Ole wako uwe unatoka nyumba ya jirani, hapo utaipatapata kwani intelijensia huko iko nje nje. Wapemba hutambuana kwa vilemba yahe !
 
Inasikitisha sana kuona kwamba nchi hii mafisadi wanafanya wanavyotaka bila hata kuchukuliwa hatua. Tunaelekea wapi?
 
Hawana asili ya kuahidi then wakarudi . Ni wepesi wa kumkamata Mbowe na Mokiwa anaendelea kungoja wamkamate .Si wepesi wa maswala ya Watanzania hapana ila kwa CCM ni haraka .Je kuna posho kwenye vika vya uchuguzi ?
Aseee"""
Kwa hiyo hawa jamaa ni wepesi sana kwenye kufanya yale amabyo hawajatumwa sio??/
 
Back
Top Bottom