Bado tuna safari ndefu ya ukombozi.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado tuna safari ndefu ya ukombozi....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Mar 29, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Bado tumetawaliwa na UTUMWA wa KIFIKRA, kwamba HATUWEZI na VYETU HATUVITHAMINI!
  WAHENGA WALISEMA "UTU BUSARA, UJINGA HASARA' haikutosha wkaongeza "MDHARAU KWAO MTUMWA"

  Leo hii Mtanganyika aliyekufa mwaka 1906 akifufuka hatoona tofauti baina yake na Mtanzania wa leo!!!

  Bado fikra za watanzania wengi zinaishi ughaibuni, wengi wetu tunadhani ukombozi na maarifa yote yanatoka huko. Tumepoteza uwezo wetu wa kufikiri na kujitegemea wenyewe na tumegeuka TEGEMEZI... si hoja wala ajabu kuona tunaowaita viongozi WAKITAWALA HIZI NCHI ZETU KUTOKA NJE YA NCHI!!

  Hainishangazi kuona hao wanaoitwa viongozi wakitafuta suluhisho na ufumbuzi kwa hao wanaoitwa WAHISANI! (KAULI ZA "TUTAWASHTAKI KWA WAHISANI) Hizo ndizo hutawala na kutisha! (wenye Nchi, WANANCHI wenyewe si kitisho!) HAWAHUSISHWI.. ni kama biashara fulani!

  SITOKOMA KUSEMA "HERI UTUMWA WA MWILI KULIKO UTUMWA WA AKILI!"

  NA KWA HAYA YANAYOTOKEA SI TANZANIA PEKEE, BALI AFRIKA ITAENDELEA KUPIGANIA UHURU KWA MUDA MREFU SANA!

  Uzalendo utaendelea kudidimia, huku watu wakiutukuza utamaduni usio wa asili yetu kwamba ndio ustaarabu! Tutaendelea kuzalisha wasomi na viongozi vibaraka kwa muda mrefu... UKOMBOZI WA KWELI UTAPATIKANA AFRIKA KUKIJA KIONGOZI KAMA HITLER KATIKA BARA HILI!

  VINGINEVYO TUTAENDELEA KUIMBA NA KUCHEZA NGOMA AMBAZO MIDUNDO YAKE HAIELEWEKI.

  WENYE UPEO PEVU KAZI KWENU HAPO.
   
Loading...