Bado Tujiulize hivi ni sahihi wabunge kututafsiria kauli ya CAG?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
CAG aliulizwa "tunaona kwamba ofisi ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa Tanzania inafanya kazi nzuri sana, kila mwaka inatoa ripoti zinaoonyesha kuna ubadhilifu wa fedha lakini hakuna hatua zinazochukuliwa"

CAG akajibu " Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tu lakini kama tunatoa ripoti na hatua hazichukuliwi huo kwangu mimi ni udhaifu wa bunge, bunge linatakiwa lisimamie kuhakikisha kuwa pahali penye tatizo hatua zinachukuliwa"

baada ya kauli hii wanachama wa taasisi hii iliyoitwa "dhaifu" wamekasirika na kuanza kututsiria kuwa hasira zao sio kwa wao kuitwa dhaifu hata kama ingekuwa ni kwa ukweli bali hasira zao ni kutokana na taswira ya nchi kimataifa.

mmoja amesema "unajua kama nchi tunatumia fedha nyingi kupitia ubalozi kujenga taswira ya nchi yetu lakini sasa mmoja wetu akienda huko akasema wasimamizi ni dhaifu si tutanyimwa misaada?"

Je wewe unadhani kimaadili yoyote yenye kutetea maslahi ya Watanzania CAG alikosea kusema Bunge ndilo lenye wajibu wa kusimamia hatua zichukuliwe na kama hatua hazichukuliwi huo ni udhaifu kwa bunge?

Je unadhani ni lipi linahatarisha maslahi ya watanzania zaidi ubadhilifu kutokea na wenye kustahili kusimamia hatua zichukuliwe wakakaa kimya au kuwasema hawa wazi mbele ya wafadhili?

Je unadhani wanachama wa taasisi wasisitize maadili ya kutosemana mbele ya wafadhili na kugangania hawana mapungufu au watafakari mapungufu yaliyosemwa na kuyafanyia kazi?
 
Back
Top Bottom