Bado sijaelewa kuhusu hii

Miguel Alvarez

JF-Expert Member
May 28, 2019
2,166
3,827
Ha bari za jioni wakuu..! Kuna jambo nimeliona nataka kupata ufafanuzi kwa wale wajuvi wa mambo,ni mara nyingi nimekuwa nikiona hizi nyimbo za singeli lakini kuna kitu bado sijaelewa naomba kueleweshwa ili nipate kujua, nimekuwa nikiona video nyingi za singeli utakuta mtoto wa kiume anajibinua huku akikatika viuno huku wakiwa vifua wazi ili tupate kuona vile wanavyokatika huku wakkijitizama kwa nyuma kana kwamba kutuonyeshea wanavyokatika , nimeshindwa kuelewa huu mziki wa singeli una uhusiano gani na vijana kukatika kiasi kile?ikiwa kama kijana wa kiume nimejiuliza sana kuhusu hawa vijana wenzangu sijawaelewa labda mwenye ufahamu kuhusu hili atujuze huu uhusiano wa singeli na ukatikaji mauno.
 
Ktk muziki unaobomoa maadili ya vijana ni huu wa singeli , unanikumbusha mchilikuuuuu yaaani ni vulugu mechi kwenye jamii na hakuna utiii wala mafunzo wa unabii
 
Ktk muziki unaobomoa maadili ya vijana ni huu wa singeli , unanikumbusha mchilikuuuuu yaaani ni vulugu mechi kwenye jamii na hakuna utiii wala mafunzo wa unabii
Acha kabisa mkuu ukiachilia uchezaji wao hata kile wanachokiimba huwa sielewi kabisa
 
Mimi mwenyewe siwaelewi..Kuna siku niliona video mkaka anatikisa tako Moja Kama ana twerk aibu niliona mimi
 
kuna bwana mmoja aliimba "asiyecheza mtie dole",nilikua na binti yangu aisee nilijisikia aibu sana
 
kuna bwana mmoja aliimba "asiyecheza mtie dole",nilikua na binti yangu aisee nilijisikia aibu sana
Huku uswahilini vitoto vidogo wakishasikia tuu inapigwa basi vinaanza kushindana kukatika hapo utakuta hata vitoto vya kiume na wazazi muda mwingne wanaona na kuchekelea tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom