Kama tungalijua kesho itakuwaje tungesimama kidete na maamuzi.maana matokeo ya leo yanatokana na maamuzi ya jana.ndipo tuone na jinsi ilivyo vyema kuvumilia bila kikomo.kuna mtu alikuwa anapasua jiwe akagonga nyundo 99 uvumilivu ukamshinda akaacha akaja mmoja akapiga nyundo 1 tu jiwe likapasuka.wakati zilipokujilia hisia za kuachana nae haukujua nini kingefuata kumbe bado ulikuwa unampenda ila uvumilivu ulikupaa.lakin wakati huu ndio unaona kuwa ulimpenda,chakufanya kiri kosa mbele yake mueleze kinagaubaga kuwa unampenda kwa kiasi gani,muombe kwa unyenyekevu akupende tena,lakin wakati huo ukiwa umemtanguliza Mungu hakika utafanikiwa Mungu akusaidie dada yangu.