Habari za mda huu wana jf, bila kupoteza muda naomba niende kwenye tatizo langu ambalo nahitaji ushauri wenu, nilipokua secondary form four nilikua na gf ambaye yeye alikua form three, kiukweli nilimpenda na nadhani na yeye alinipenda pia kwani alikua ananisikiliza mno na alikua ananipa kila kitu nilichokua nataka kwani kwao walikua na uwezo kidogo so alikua hapendi nikae na matatizo ambayo yeye anaweza kutatua, mahusiano yetu yalikua moto kwani hakuna mtu ambaye alikua hajui si shuleni wala mtaani kote walijua kuhusu mahusiano yetu, na nakumbuka nilishawahi kuapa mbele ya marafiki zangu kuwa yeye ndo atakuja kuwa mke wangu kwani yeye ndo alikua msichana wa kwanza kuonyesha ameridhishwa na mimi katika kila kitu, baada ya muda wa kama miezi kumi katika mahusiano nilianza kuhisi kumchoka mwenzangu na kuanza kutamani wanawake wengine akiwemo dada yake, na kama mnavyojua sisi wanaume ni wazuri katika kuwashawishi wanawake, nikafanikiwa kutoka na dada yake wakati huyo gf wangu hajui lolote linaloendelea kati yangu mimi na dada yake, nilipunguza mapenzi kwa gf wangu na nikaanza kutoka na wasichana wengine na kujiona mimi ndo mjanja wa mjini, na hata baada ya kumaliza mtihani wangu wa mwisho niliondoka na kwenda mkoa mwingine bila kumuaga na hata baada ya kufika kule niliacha kabisa kumpigia simu na kumtumia sms kisingizio kikiwa ni vocha na hata akituma naleta kingine yan kwa kifupi radha yake kwangu iliisha kabisa na yeye alipunguza kunitafuta kwani nilikua namjibu majibu mengine yasiyostahili mtu kujibiwa,.Baada ya miezi kama miwili kupita nilirudi mkoani kwetu ila nilipofika watu wakaanza kunipa habari kuwa kuna kijana wanamuona sana na gf wangu na hata baada ya kufuatilia nikajua ni kweli na nilipomuuliza yeye alikubali kuwa anatoka nae na pia akaniomba msamaha na kusema alifanya vile kwa kuwa alikua mpweke sana na majibu yangu yalikua yalimkatisha tamaa ya kuwa na mimi nikamsamehe na tukaendelea, ila kadri siku zilivyozidi kwenda na yeye ndo jinsi alivyozidi kubadilika yaan akawa hanijali kama zamani yaan kwa kifupi kibao kikageuka yale niliyokua namfanyia mimi yeye ndo akawa ananifanyia nilikua naumia ila nilijua mimi ndo tatizo so nilijitahidi sana kuwa chini ili mahusiano yetu yawe kama zamani ila wapi ilishindikana ikafikia hatua hata kukutana nae inabidi nimwambie wiki mbili kabla ili ajipange yaan hapo ni kukutana tu kusalimiana kiukwel nilishindwa kuvumilia nikaachana nae nikabadilisha hadi namba na nikaenda kusoma mbali ili nisionane nae, ni miaka kama mitano au sita ila nashndwa kumsahau natamani kumtafuta ila naogopa nitaonekana dhaifu sana, ila moyo wangu unakiri kumpenda na nishapitia relation kama mbili ila zote naziona hazifai na sioni kama kuna wa kumfikia huyo msichana,.
Nahitaji ushauri wenu nampenda na nahitaji kuwa nae ila naogopa kuonekana dhaifu mno kwani ukizingatia yeye hajawahi kunitafuta kwa njia yoyote ile tangu tulipoachana,
Nahitaji ushauri wenu nampenda na nahitaji kuwa nae ila naogopa kuonekana dhaifu mno kwani ukizingatia yeye hajawahi kunitafuta kwa njia yoyote ile tangu tulipoachana,