Bado naitafakari kauli ya Waziri Mwigulu Nchemba

Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,648
1,696
Bila shaka watanzania wengi sasa hivi wanafahamu kinachoendelea kuhamasishwa mitandaoni juu ya maandamano ya wananchi ya kupiga uvunjifu wa amani na ukosefu wa uhuru wa kweli na demokrasia vinavyoendelea kuchukua kasi nchini kwetu.

Juzi mkuu wa nchi akiwa Singida ktk tukio la kufungua kiwanda cha bwana mmoja cha kukamua alizeti alitoa hotuba na ktk hotuba yake alifoka kwa hali ya kutisha kuwa wanaopanga kufanya maandamano atawashughulikia kikamilifu. Aidha mkuu huyo hakujipambanua atawashughulikia namna gani na kwa sababu gani.

Baada ya hapo waziri wa mapolisi alisimama na kumuahidi mkulu kuwa vitisho vyake atavitafsiri kwa matendo. Kwa maneno yake mwenyewe waziri huyo alisema:

“Kinaachotafutwa siyo kuwa na mabango. Kinachotafutwa ni watu kukusanyika, wakishakusanyika ikitokea namna yoyote ya utawanyaji wa wale watu, wafyatue risasi waseme serikali imeua watu. Na njama hiyo tumeiona, na mimi mimemwelekeza IGP…..”

Ktk maelezo yake huyo waziri alishangaza watu kwa kuwatuhumu moja kwa moja wapinzani kwamba ndio wanaopanga hayo ingawa sote tunafahamu master mind wa jambo lenyewe ni nani. Wakati wote huyo waziri alipokuwa akiongea mkulu alionekana akimtazama huku akitikisa kichwa kama ishara ya kuafiki hoja ya waziri wake.

Suala la maandamano limekuwa pasua kicha kwa viongozi wa nchi ingawa sina hakika kama kweli yatafanyika kutokana na nature ya watanzania ninavyowajua kwa woga wao na kutojali (kutokujitambua). Hata hivyo kauli ya waziri kwa mtu yeyote mwenye akili ya wastani tu imeeleza bayana kile serikali inachopanga kufanya iwapo kweli maandamana hayo yatafanyika. Tumeelewa wenye akili kuwa waziri keshawaagiza mapolisi kuwatandika kwa risasi za moto raia watakaoandamana na excuse imeshatolewa kwamba watasema waandamanaji ndio waliofyatua risasi. Tumeelewa bila chenga kuwa kumbe ile kauli isiyo na haya ya yule polisi Dar juu ya mauwaji ya yule binti wa chuo mrembo asiye na hatia, Akwilina walikaririshwa na waziri wao!

Siyo kwamba waziri wa mapolisi hana akili ya kujua kwamba watanzania wanaelewa alichomaanisha. Ni kiburi na ulevi wa madaraka ndivyo vinatutawala kwa sasa. Waziri huyu keshajipambanua mwenyewe bila chenga tena kuwa yeye ni nani. Kwamba yeye ndiye master mind na kiongozi wa hao watu wasiojulikana. Nitaitetea hoja hii.

Bahati mbaya watanzania ni wasahaulifu sana kwani naona hawakumbuki kilichomwinua huyu waziri wa mapolisi hadi kwenye level ya uwaziri ndiyo maana sioni mtu akimnyooshea kidole kuwa ndiye kwa hakika master mind na kiongozi wa watu wasiojulikana. Naomba niwakumbushe tu kilichomfikisha hapo.

Wakati wa Awamu ya Nne kulitokea mgomo mkubwa wa madaktari nchini. Bunge lilipokuwa linajadili suluhisho la mgomo ili kunusuru maisha ya wagonjwa wasio na hatia waziri huyu akiwa bado mbunge tu wa kawaida alitengeneza hoja ya kwake akiwatuhumu wapinzani bila ushahidi wowote kuwa eti wapinzani ndio wanaowatuma madaktari wagome! Alisimama kidete na hoja yake hiyo na baada ya mgomo kuisha punde kidogo mkulu wa wakati huo akaunda ofisi mpya kwenye Wizara ya fedha ikawa na manaibu waziri wawili, huyu bwana mdogo akamteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha – Sera na Mipango. Kimsingi kitengo hiki kilikuwa ni cha CCM na jukumu lake lilikuwa kushughulika na allocation of funds ktk strategies za kichama, hasa ktk chaguzi na mambo yasiyojulikana. Bwana mdogo alipewa pia jukumu la ku-strategize impeachments kwa wapinzani.

Huyu bwana mdogo namfahamu sana. Mambo yanayotokea hivi sasa ya watu wasiojulikana na kukomaa kwa police brutality ambavyo vyote viko chini ya wizara yake vinafanana kabisa na hurka ya huyu bwana mdogo tangu akiwa shule. Ndiyo maana nilishituka sana kiongozi wa malaika alipomteua kuwa waziri wa mambo ya ndani baada ya kumtumbua Kitwanga. Niliwahi kuandika katika mitandao fulani baada ya uteuzi huu kwamba watanzania watarajie nini wizara ya usalama wa raia inapopewa mtu katili, mwenye hila na asiye na huruma kwa binadamu kama Mwigulu Lameki Nchemba. Yumkini yote niliyotabiri juu ya mtu huyu yametokea sawia na kwa muda mfupi kabisa!

Kabla ya watanzania kufikiria kujaribu kum - impeach rais kwa maandamano (kazi ambayo ni kubwa mno kwa maoni yangu) nilidhani wangeanza na huyu waziri kwanza na watendaji wake (wakuu wa vyombo vya usalama wa raia) maana ushahidi upo wazi, hoja zipo na inawezekana. Nasikitika kwamba huyu bwana hatajwi kwa msisitizo na hasira inayostahili!
 
“Kinaachotafutwa siyo kuwa na mabango. Kinachotafutwa ni watu kukusanyika, wakishakusanyika ikitokea namna yoyote ya utawanyaji wa wale watu, wafyatue risasi waseme serikali imeua watu. Na njama hiyo tumeiona, na mimi mimemwelekeza IGP…..”

Sasa si polisi wabebe vilungu tu ili tujue kama risasi si za polisi. Lakini, je, vipi kuhusu wale wa usalama wa taifa na polisi wasio vaa sare za polisi? Vipi kuhusu raia wanaomiliki silaha?
 
Bila shaka watanzania wengi sasa hivi wanafahamu kinachoendelea kuhamasishwa mitandaoni juu ya maandamano ya wananchi ya kupiga uvunjifu wa amani na ukosefu wa uhuru wa kweli na demokrasia vinavyoendelea kuchukua kasi nchini kwetu.

Juzi mkuu wa nchi akiwa Singida ktk tukio la kufungua kiwanda cha bwana mmoja cha kukamua alizeti alitoa hotuba na ktk hotuba yake alifoka kwa hali ya kutisha kuwa wanaopanga kufanya maandamano atawashughulikia kikamilifu. Aidha mkuu huyo hakujipambanua atawashughulikia namna gani na kwa sababu gani.

Baada ya hapo waziri wa mapolisi alisimama na kumuahidi mkulu kuwa vitisho vyake atavitafsiri kwa matendo. Kwa maneno yake mwenyewe waziri huyo alisema:

“Kinaachotafutwa siyo kuwa na mabango. Kinachotafutwa ni watu kukusanyika, wakishakusanyika ikitokea namna yoyote ya utawanyaji wa wale watu, wafyatue risasi waseme serikali imeua watu. Na njama hiyo tumeiona, na mimi mimemwelekeza IGP…..”

Ktk maelezo yake huyo waziri alishangaza watu kwa kuwatuhumu moja kwa moja wapinzani kwamba ndio wanaopanga hayo ingawa sote tunafahamu master mind wa jambo lenyewe ni nani. Wakati wote huyo waziri alipokuwa akiongea mkulu alionekana akimtazama huku akitikisa kichwa kama ishara ya kuafiki hoja ya waziri wake.

Suala la maandamano limekuwa pasua kicha kwa viongozi wa nchi ingawa sina hakika kama kweli yatafanyika kutokana na nature ya watanzania ninavyowajua kwa woga wao na kutojali (kutokujitambua). Hata hivyo kauli ya waziri kwa mtu yeyote mwenye akili ya wastani tu imeeleza bayana kile serikali inachopanga kufanya iwapo kweli maandamana hayo yatafanyika. Tumeelewa wenye akili kuwa waziri keshawaagiza mapolisi kuwatandika kwa risasi za moto raia watakaoandamana na excuse imeshatolewa kwamba watasema waandamanaji ndio waliofyatua risasi. Tumeelewa bila chenga kuwa kumbe ile kauli isiyo na haya ya yule polisi Dar juu ya mauwaji ya yule binti wa chuo mrembo asiye na hatia, Akwilina walikaririshwa na waziri wao!

Siyo kwamba waziri wa mapolisi hana akili ya kujua kwamba watanzania wanaelewa alichomaanisha. Ni kiburi na ulevi wa madaraka ndivyo vinatutawala kwa sasa. Waziri huyu keshajipambanua mwenyewe bila chenga tena kuwa yeye ni nani. Kwamba yeye ndiye master mind na kiongozi wa hao watu wasiojulikana. Nitaitetea hoja hii.

Bahati mbaya watanzania ni wasahaulifu sana kwani naona wahakumbuki kilichomwinua huyu waziri wa mapolisi hadi kwenye level ya uwaziri ndiyo maana sioni mtu akimnyooshea kidole kuwa ndiye kwa hakika master mind na kiongozi wa watu wasiojulikana. Naomba niwakumbushe tu kilichomfikisha hapo.

Wakati wa Awamu ya Nne kulitokea mgomo mkubwa wa madaktari nchini. Bunge lilipokuwa linajadili suluhisho la mgomo ili kunusuru maisha ya wagonjwa wasio na hatia waziri huyu akiwa bado mbunge tu wa kawaida alitengeneza hoja ya kwake akiwatuhumu wapinzani bila usahahidi kuwa ndio wanaowatuma madaktari wagome! Alisimama kidete na hoja yake hiyo na baada ya mgomo kuisha punde kidogo mkulu wa wakati huo akaunda ofisi mpya kwenye Wizara ya fedha ikawa na manaibu waziri wawili, huyu bwana mdogo akamteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha – Sera na Mipango. Kimsingi kigengo hiki kilikuwa ni cha CCM na jukumu lake lilikuwa kushughulika na allocation of funds ktk strategies za kichama, hasa ktk chaguzi na mambo yasiyojulikana. Bwana mdogo alipewa pia jukumu la ku-strategize impeachments kwa wapinzani.

Huyu bwana mdogo namfahamu sana. Mambo yanayotokea hivi sasa ya watu wasiojulikana na kukomaa kwa police brutality ambavyo vyote viko chini ya wizara yake vinafanana kabisa na hurka ya huyu bwana mdogo tangu akiwa shule. Ndiyo maana nilishituka sana kiongozi wa malaika alipomteua kuwa waziri wa mambo ya ndani baada ya kumtumbua Kitwanga. Niliwahi kuandika katika mitandao fulani baada ya uteuzi huu kwamba watanzania watarajie nini wizara ya usalama wa raia inapopewa mtu katili, mwenye hila na asiye na huruma kwa binadamu kama Mwigulu Lameki Nchemba. Yumkini yote niliyotabiri juu ya mtu huyu yametokea sawia na kwa muda mfupi kabisa!

Kabla ya watanzania kufikiria kujaribu kum - impeach rais kwa maandamano (kazi ambayo ni kubwa mno kwa maoni yangu) nilidhani wangeanza na huyu waziri kwanza na watendaji wake (wakuu wa vyombo vya usalama wa raia) maana ushahidi upo wazi, hoja zipo na inawezekana. Nasikitika kwamba huyu bwana hatajwi kwa msisitizo na hasira inayostahili!

Kiukweli mwigulu si mtu mzuri, , ni mtu katili n.a. mwenye kibri ,,
 
Simshangai Nwigulu. Naushangaa upofu wa watanzania wa kushindwa kuona vitu vya wazi kama hivi!
Tatizo washasahau mabaya yake ya nyuma kabla hajawa waziri, lakini ukiunganisha na mambo yake ya huko nyuma,, n.a. Leo yeye ndio waziri wa wizara nyeti ya washika bunduki n.a. mabomu
 
Hii serikali ya awamu ya Tano tutaikumbuka kwa vituko...lakin naomba Chadema msinisahau kunipa UDC baada ya Tarh 26/04
 
Back
Top Bottom