Bado mambo yako vilevile, rais fanya mabadiliko huko wizarani

365

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
1,377
1,455
Juzi nilikua wizara ya ajira, Jana nilikua wizara ya kilimo na leo nilikua wizara ya viwanda...

Kusema ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu...katika hizo wizara zote kwanza bado kuna urasimu wa hovyo kiasi kwamba masekretari ndo wanajifanya wanajua kila kitu kiufupi wao ndo wasemaji wa wizara usipokuwa mtata unaishia reception lakini pia kila unachouliza wanasema hawajui...mfano unauliza utaratibu wa kuanzisha kiwanda ukoje unajibiwa njoo kesho...

Ushauri wangu...Rais Pombe arekebishe mifumo ya wizara na ateue watu weledi wenye ari ya kujua na kufuatilia mambo mbalimbali..vinginevyo Tanzania maendeleo tutaendelea kuyasoma kwenye mitandao tu.
 
Hivi wewe unategemea jipya, viwanda ilikuwa njia ya kutongozea kura kwa ajili ya kula.
 
Msijali serikali hii sikivu italifanyia kazi suala lako
 
Kiukweli JPM amenajitahidi lakini bado ipo kazi nzito sana. Mfano bado vibali vya kazi kwa wageni vinatolewa kirahisi sana bila uchunguzi wa kutosha. Wageni wasiostahili kufanya kazi hapa nchini bado wapo na Uhamiaji wanawajua....hatuwezi kulinda hata hizi ajira chache zilizopo? Hongera JPM maana tumeona position kibao zikitangazwa kupisha Watanzania lakini huku ground bado wageni wanaofanya kazi zisizostahili wamejaa.
 
Nchi masikini zinahitaji mifumo imara BA si watu imara!! Leo hii kila uchafu na uozo ktk pembe ya nchi anasubiriwa Magufuli akasafishe tutafika kweli?
 
Nchi hii ina magonjwa mengi ,unadhani kutumbua majipu kutaponya malaria iliyopanda kichwani?
 
Wateuliwa wengi hawana ubunifu wanasubiri mpaka rais aseme wao ndo watekeleze. Wana Kali yao kwamba wanatekeleza maagizo ya rais. Sasa kwa hali hii tusubiri mh. afike hayo maeneo atoe maagizo labda ndo kutakaa sawa.
 
Mimi nilienda wizara ya mambo ya ndani..ku renew my passport nilikutana na urasimu wa hali ya juu plus ubabaishaji...yaani mambo ni yalee yale..kwanza hawana record yoyote ya vitu nilivyojaza..kwa passport iliyoisha..ikabidi nianze upya..wako na system ya ki zamani computer data base ziko empty...with No records yaani maajabu..maajabu!
 
  • Thanks
Reactions: 365
ni hatari sana...yaani watumishi wizarani na idara zake ni hovyo kwakweli mi nilisikitika sana...yaani jitu lipo wizara ya kilimo lakini halijui taratibu za kuingiza zana za kilimo...
 
Nchi masikini zinahitaji mifumo imara BA si watu imara!! Leo hii kila uchafu na uozo ktk pembe ya nchi anasubiriwa Magufuli akasafishe tutafika kweli?
Yeye mwenyewe ndio anataka hivyo! Kama kazi za katibu kata anafanya rais unategemea Waziri wake ajiamini kufanya maamuzi au kazi zake kwa uhuru? Mifumo imara nakubaliana nalo kabisa Mkuu na Rais auamini jambo ambalo haliwezekani
 
Juzi nilikua wizara ya ajira,jana nilikua wizara ya kilimo na leo nilikua wizara ya viwanda...
kusema ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu...katika hizo wizara zote kwanza bado kuna urasimu wa hovyo kiasi kwamba masekeletale ndo wanajifanya wanajua kila kitu kiufupi wao ndo wasemaji wa wizara usipokua mtata unaishia reception lakini pia kila unachouliza wanasema hawajui...mfano unauliza utaratibu wa kuanzisha kiwanda ukoje unajibiwa njoo kesho...

Ushauli wangu...RAIS Pombe alekebishe mifumo ya wizara na ateue watu weledi wenye ari ya kujua na kufuatilia mambo mbalimbali..vinginevyo Tanzania maendeleo tutaendelea kuyasoma kwenye mitandao tu.
Yaani wewe nawe unataka kuanzisha kiwanda? Hata Kiswahili hujui eti ushauli wangu ndio mini ushauli? Alekebishe ndio mini hiki kitu alekebishe? Sema arekebishe! Mmeharibu Nchi sasa mnataka kuharibu Kiswahili!
 
Kwahiyo Kama Hujui Kuongea Vizuri Kiswahili Huna haki Ya Kuazisha Kiwanda??.

Ama Kweli Kusoma Na Kuelewa Ni Vitu Viwili Tofauti.
 
Yaani wewe nawe unataka kuanzisha kiwanda? Hata Kiswahili hujui eti ushauli wangu ndio mini ushauli? Alekebishe ndio mini hiki kitu alekebishe? Sema arekebishe! Mmeharibu Nchi sasa mnataka kuharibu Kiswahili!
dhamira kuu ya lugha ni kufikisha ujumbe...kama hujaelewa uliza ujibiwe....
 
Wateuliwa wengi hawana ubunifu wanasubiri mpaka rais aseme wao ndo watekeleze. Wana Kali yao kwamba wanatekeleza maagizo ya rais. Sasa kwa hali hii tusubiri mh. afike hayo maeneo atoe maagizo labda ndo kutakaa sawa.
UKITAKA WAJE ANZISHA KIWANDA CHA SOSEJI INAYOTOKANA FISI HALAFU IITE FISI M HYENA HYENA SAUSAGE WATAKUJA TU KAMA SIO KUZINDUA KUTUMBUA KIWANDA FEKI
 
Yaani wewe nawe unataka kuanzisha kiwanda? Hata Kiswahili hujui eti ushauli wangu ndio mini ushauli? Alekebishe ndio mini hiki kitu alekebishe? Sema arekebishe! Mmeharibu Nchi sasa mnataka kuharibu Kiswahili!

Acha dharau wewe mwenyewe k.i....za hata ulichoandika hakieleweki
 
Back
Top Bottom