Bado kidogo, tunakaribia kufika Sudan

Carnivora

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
3,651
5,987
Ndio, nasema bado kidogo. Wao waendelee na sisi hayajatuchoma vizuri tutaamka tu.

Inasikitisha. Wao wanasimama kwenye majukwaa wanasema dhahiri Watanzania sio wajinga. Huwa wanafatilia kila kitu na wanahoji kisha wanaamua kukaa kimya. Sio kwamba hawajui wanachofanyiwa. Huu uvumilivu una mwisho. Nawaambia.

Wamemuuwa Akwilina, wakasema mtu alifyatua risasi hewani. Watanzania sio wajinga eti wakubali tu kuwa risasi inakata kona. Kesi wanawapa wakina Mbowe kuwa wamesababisha mauwaji. Sisi sio wajinga. Narudia. Sisi sio wajinga. Siku yenu yaja.
Bado kidogo, tunakaribia Sudan.

Wamewanyamazisha hata waliokuwa wanachambua magazeti asubuhi the likes of Maulid Kitenge na wenzie. Yaani wanataka kusikia habari zao tu za kuwapendeza wao. Wakayafungia magazeti kwa kuandika yale yanayowaudhi wao hata kama ni ukweli. Leo tena nasikia msemaji wao kayapiga bit magazeti kwa kaundika habari za chama cha Zitto namna walivyochambua report ya sieiijii.
Bado kidogo, tunakaribia Sudan.

Wasiojulikana walimpiga Tundu Lissu risasi, wakamteka Azory Gwanda, wakamteka Abdul Nondo, wakamteka Mo Dewji. Hawa wote habari zao mpaka leo ni sintofahamu. Wanaoitwa polisi kazi yao ni kutishia watu watawapiga na kuchakaa. Komandoo wa polisi wa mkoa husika sijui ulikuwepo wakati Mugwai anashambuliwa au umelikuta tu jalada ofisini na wapelelezi wako mmeamua mkae kimya. Fureshi tu. Sisi sio wajinga. We endelea kutisha watu utawachakaza....wakati wewe mwenyewe maisha yamekuchakaza.
Bado kidogo, tunakaribia Sudan.

Kuna yule supika. Yeye anatoa tu matamko. Sijui ndio anaagizwa na mhimili uliojinasibu kuwa umejikita sana chini au ni mihemko yake tu. Lakini ajue, tunafahamu kuwa alikua India anatibiwa akitumia kodi zetu. Inawezekana hajapona vizuri. Sisi sio wajinga. Eti sieijii anamkwamisha Rais, mwenyewe mbona hajasema kama kakwama? Na amekwama wapi?
Sisi Watanzania sio wajinga. Tunaona kabisa anachokitafuta.
Bado kidogo, tunakaribia Sudan.

Koroshow zetu Wahindi walitaka kununua. Wao wakajifanya wanazo pesa. Niwaambie tu. Usumbufu mliotupa hatutaki tena mje kununua koroshow zetu. Bora tuchome wenyewe tuuze kwenye vifuko kama wale vijana wa kwenye mabus tukienda kwa watani zetu kuwasalimia. Bora tuwapelekee na akina nshomile Bukoba nao wajue utamu wa koroshow kuliko usumbufu mliotupa. Hao wanaoitwa kangomba sisi ni wakombozi wetu wakati nyie mkiwa mnakula samosa na chapati za bil 1 na hakuna anayewahoji. Maana wanaofukunyua mnataka wajiuzulu. Kwanini msianze nyie kwanza. Anza wewe kujiuzulu basi. Shubaamit. Sisi sio wajinga.
Bado kidogo, tunakaribia Sudan.

Yapo mengi sana. Bao la mkono, marudio ya uchaguzi Zanzibar, kesi za wabunge wa upinzani. Kununua wabunge, upotevu wa 1.5T, mauwaji ya Kibiti/Rufiji. Yapo mengi. Mengi sana. Naomba niishie hapa kwa leo, ila naendelea kuwakumbusha kuwa sisi sio wajinga. Sisi Watanzania sio wajinga.
Bado kidogo, tunakaribia Sudan.

Mmeyashuhudia yaliyotokea Sudan eeh? Nadhani jibu ni ndio. Basi muda sio rafiki sana. Hakuna aliyedhani Al Bashir angekuwa juu ya mawe hapa unaposoma uzi huu.


Watanzania sisi sio wajinga. Bado kidogo, tunakaribia Sudan.
 
Ndo hivo huwezi kufananisha Zimbabwe, Algeria na Sudan na nchi yetu, kwani hao viongozi wa nchi nilizotaja wamekaa muda mrefu sana kwenye nchi zao, vile vile bado wapo wengine ambao wamekaa muda mrefu . hapa hapa africa.
Unachoona wewe ni kukaa madarakani tu? Bro....hebu kuwa serious kidogo.
 
Unachoona wewe ni kukaa madarakani tu? Bro....hebu kuwa serious kidogo.
Ndiyo kwasababu kiongozi ukikaa muda mrefu madarakani kwa kulazimisha utawaudhi wengi hata wafuasi wako, lakini kwa unaloongelea wewe sijajua ni lipi, ila tu nikufunue ufahamu kidogo.

Ukiangalia viongozi wengi hapa duniani siyo africa pekee waliopata kupinduliwa au kufukuzwa madarakani matatizo yao asilimia kubwa ni kukaa muda mrefu madarakani pamoja na mambo mengine.

Mfano yule wa Misiri, Libya, Irack, na wenzao wengi sana.
 
Hivyo kukaa mda mchache ndio kibali cha kuisigina Katiba ya Nchi ??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wewe una ufahamu wa kuona katiba inasiginwa, lakini ikitokea ipigwe kura hapa nchini kwamba ni wangapi wanaoona katiba inasiginwa sijui kama watapatikana hata robo ya wananchi wa Tanzania, hapa nchini pana uhaba mkubwa sana wa Elimu au ufahamu juu ya mambo ya siasa tena wengine wengi wasomi lakini hawajui chochote juu ya mambo hayo.
 
Dah...Kama Sudan ilichukua miaka 39...Basi huku itatokea nikiwa na miaka 126

Sent using Beretta ARX 160
 
Acha kufananisha vitu vya ajabu na nchi yetu, kiongozi amekaa mpaka miaka 30 ndio uje ufananishe na huku?

Mkuu akuna tofauti tena yetu ndo mbaya zaid rais ana kula akiwa ikulu alafu akitoka anaendelea kula akuna atakae shiba kwaiyo tutaendelea kubeba misalaba yao hadi mwisho bora wao miaka 30 amekula mpk amechoka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu wewe una ufahamu wa kuona katiba inasiginwa, lakini ikitokea ipigwe kura hapa nchini kwamba ni wangapi wanaoona katiba inasiginwa sijui kama watapatikana hata robo ya wananchi wa Tanzania, hapa nchini pana uhaba mkubwa sana wa Elimu au ufahamu juu ya mambo ya siasa tena wengine wengi wasomi lakini hawajui chochote juu ya mambo hayo.
Watanzania sio wajinga, bado kidogo tunakaribia Sudan.

Sent using Boeing 737-MAX 8
 
Back
Top Bottom