Bado Hatujafaidika na BOT: SMZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado Hatujafaidika na BOT: SMZ

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jun 26, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema suala la hisa za Zanzibar katika Benki Kuu Tanzania (BOT) na gawio la faida zake bado halijapatiwa ufumbuzi hadi sasa.

  Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009-2010 katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.
  Waziri Kiongozi amesema wizara mbili za fedha na uchumi ya serikali ya mapinduzi zanzibar pamoja na wizara ya fedha na uchumi ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania zimeagizwa zikutane kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo hali bado ufumbuzi wake haijapatikana.

  Nahodha alisema wizara mbili hizo zinatakiwa kukutana na kutoa ripoti ya mwisho katika kikao kijacho lakini hakuwaambia wajumbe wa baraza hilo kuwa kikao hicho lini kitafanyika.

  Alisema katika suala la misaada ya nje Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kupatiwa asilimia 4.5 ya ruzuku na mikopo kupitia misaada ya kibajeti kutoka kwa wafadhili.

  Alisema awali Zanzibar ilikuwa ikipatiwa asilimia 4.5 tu pekee ya ruzuku hali ambayo ilizusha malalamiko mengi kwa wananchi wakiwemo wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba ni kiwango kidogo kinachopata Zanzibar kutoka katika mgao huo.

  Nahodha aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba vikao vya kujadili kero za muungano vinavyofanyika kati ya pande mbili ya jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na serikali ya mapinduzi Zanzibar ambapo vinaendelea vizuri huku baadhi ya mambo yakiwa yameshapatiwa ufumbuzi wake.

  Alsisema yapo baadhi ya mambo ni kwlei hajayapatiwa ufumbuzi lakini mchakato wa kutayatua upo na unaendelea na bila ya shaka wananchi wataelezwa kianchoendelea kupitia vikao hivyo vya pande mbili.

  “ Kwa ghafla utaona kama hakuna jambo lililopatiwa ufumbuzi lakini kwa kweli vikao hivi vimepata mafanikio makubwa ambapo tayari yapo mambo mengi yaliyopata ufumbuzi wake katika utekelezaji” alisema Nahodha.

  Akielezea majukumu ya Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Nahodha alisema kwa sasa tume ipo katika mchakato wa kulifanyia marekebisho daftari la kudumu la wapiga kura ikiwemo kuingiza majina ya wapiga kura wapya na kazi hiyo itaanza muda mfupi kuanzia sasa.

  Alisema pia baadhi ya kazi nyengine ikiwemo kuandaa programu mbali mbali za elimu ya wapiga kura kupitia vyombo vya habari ambayo inatazamiwa kuanza hivi karibuni ambapo wananchi wengi watafaidika na elimu hiyo.

  kazi za daftari la kudumu la wapiga kura ikiwemo kuingiza wapiga kura wenye sifa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwakani unatazamiwa kuanza Mwezi ujao katika wilaya ya Micheweni Pemba.

  Nahodha alisema mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF ambao unaratibiwa na serikali mbili umepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wake hadi sasa amabpo wananchi wengi wameitikia wito wa serikali katika kuharakisha maendeleo katika maeneo yao.

  Mfuko huo ambao unatazamiwa kumaliza shunguli zake mwishoni mwaka huu tayari jumla ya miradi 306 yenye thamani ya shilingi 4,311,138,975.40 imetekelezwa kwa Unguja na Pemba.

  Alisema kumekuwa na uwiyano mzuri sana katika utekelezaji wa miradi ya TASAF ambapo katika kisiwa cha Pemba jumla ya miradi 166 imetekelezwa yenye thamani ya shilingi 2,273,602,928.00 wakati katika kisiwa cha Unguja jumla ya miradi 140 imetekelezwa yenye thamani ya shilingi 2,037,536,647.40.

  Waziri Kiongozi pia aliwashukuru wananchi na viongozi kwa ujumla kwa juhudi kubwa walizozichukuwa katika kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo.

  Alisema miradi ya TASAF imepata mafanikio makubwa kutokana na kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika utekelezaji wake na wananchi wengi wamekuwa wakivutiwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

  Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF umejikita zaidi katika ujenzi wa shule za msingi na sekondari, miradi ya maji safi na salama pamoja na vituo vya afya katika maeneo mbali mbali visiwani Unguja na Pemba.

  Miradi ya TASAF inafadhiliwa na Benki ya dunia ikiwa chini ya usimamizi wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  Waziri Kiongozi aliliomba baraza la wawakilishi kuidhinisha jumla ya sh.11,297,315,000 kwa mwaka wa fedha 2009-2010 ambapo jumla ya sh.10,989,315,000 kwa kazi za kawaida na jumla ya sh.308,000,000 kwa kazi za matumizi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2009-2010.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hivi ndugu waziri kiongozi wa serikali ya visiwa vya viongozi unaitakia mema Tanzania au unaiwazia madudu Tanganyika isiyokuwepo?
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakika huwezi kuzungumza maendeleo au jambo lolote la manufaa kwa wananchi bila kugusa UCHUMI.

  Hongere sana Mh Nahodha ka kulibainisha hilo. sasa ni juu yako kulifuatilia ili kupata muafaka.

  Dr Hamza
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kwani tatizo lipo wapi hapo?
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jun 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Bado hujaeleweka hapo kuhusu Tanganyika. Mimi naona as long as masuala yote yanazungumzika, hakuna tatizo. Kama hizo share BOT Zanzibar ilikuwepo kabla ya kuvunjika kwa iliyokuwa East African Currency Board (EACB) halafu zikawa transfered BOT kama wanavyodai basi wazirejeshewe. Kama hazikuwepo basi wazungumze upya kuhusu hilo kwani dunia ya sasa ni mambo ya bilateral or multilateral dialogue, au sio wakuu?
   
Loading...