Badilisha PC yako ya zamani kuwa Powerful MIKROTIK ROUTER

Badilisha PC yako ya zamani kuwa Powerful MIKROTIK ROUTER

QasraNet

Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
38
Reaction score
50
Router zenye uwezo mkubwa bei yake ipo juu sana. Sasa nikaanza kufanya research ya kama PC ikiwa na Windows OS ya kawaida kama inaweza kufanya kazi kama Router. Nilihangaika mpaka kuja kupata majibu kuwa kama unataka kutumia PC yako kama Router basi inabidi usasishe (install) OS ambayo ni special for Routers.
Katika hizo OS nikapata (Linux Kernel Based OS):
1. Mikrotik RouterOS x86
2. pfSense OS
Sasa kwakuwa mi ni fan wa Mikrotik kwa muda mrefu, ikanibidi nitembee na RouterOS ambayo nimeizoea na ninaifahamu. Shida ilikuwa PC yangu ina ethernet Port 1 na sio Gigabit port, ni FastEthernet port. Nikahangaika na ChatGPT ananiletea mambo ya kuwa niwe makini kwenye kununua PCI NIC maana nyingi huwa zinakuwa unrecognized. Nikajichinja midhali PC ilikuwepo fresh just haikuwa na SSD, nikaenda kununua SSD (128GB) na Gigabit (PCI) Network Cards 3, Nilinunua Machinga Complex upande wa magari ya Kigamboni (mtumba tested palepale). Usijisumbue kwenda kariakoo hautozipata labda uagize from AliExpress n.k.
20260102_081547.jpg
20260102_081600.jpg

So nilivyopata nafasi, nikafunga mzigo kwa maelezo ya video hii. Nilihofia zile card zisingetambulika kiasi nikachukua 2 za intel na moja ya Broadcom lakini zote zimesoma fresh kabisa.
Baada ya hapo mambo yakawa walete.
20260102_082324.jpg

Don't worry about me showing my local IP addresses, I know what I am doing.
Now ni zaidi ya masaa 12 yamepita tangu mzigo uwe hewani. Powerconsuption iko very low sana unaweza dhani pc ipo off.
20260102_081749.jpg
20260102_081613.jpg

Hapo Port niliyoifanya kuwa LAN, inaipa network SWITCH then SWITCH inasambaza unyama. Hiyo Router ya Fiberhome namna ya kutumia kama AP nilitolea maelezo kwenye andiko hili. Sijajaribu kutumia na WiFi Card but naona haina haja since nina AP za kutosha. Na hata umeme wa kuPower Hii Router na Switch nimeutoa humo humo kwenye PC. Waya wa Power wa HDD una Rangi Nyekundu (5V), Nyeusi (Ground), Njano (12V) na Nyeusi (Ground). So switch yangu hiyo ni Gigabit switch ila inahitaji just 5V na hiyo router inataka 12V nikajiongeza.

Kabla ya kufanya hivi, nilikuwa na Routerboard ambayo ipo configured kila kitu, nilichokifanya ikawa ni kuhamisha configurations sio Backup. Baada ya kuhamisha configurations ndo nikaRename Router kuwa jina linalosomeka hapo.
Screenshot 2026-01-02 082707.png

Screenshot 2026-01-02 082849.png

Kwa wauzaji wa WiFi kazi ni kwenu, mi kwangu inafanya kazi fresh.
Screenshot_20260102_082221_Captive Portal Login.png
Screenshot_20260102_082245_Settings.png

⚠️ Maelezo yangu sio rafiki kwa mtu asiyejua chochote kwenye upande wa networking. Na mimi hii pc ilikuwa haina kazi ndo nikaipa kazi hii.
 
Attachments

  • Screenshot 2026-01-02 082455.png
    Screenshot 2026-01-02 082455.png
    77.2 KB · Views: 12
Daah.
Umenikumbusha mbali Sana.
Niliajiriwa sehemu nikiwa fresh from college.
Kabla ya kumalizia kadigrii jalalani(UDSM) nilisoma CISCO CCNA pale UCC Main Campus nikaishia njiani majukumu mengi. Nilipendelea kuchapa code(programming) sasa ajira zetu za kibongo ukiwa supervisor au manager inatakiwa ujue vyote Database, Software Development, na networking.
Nikakutana na huo mfumo wa PC ya kawaida kuwa configured kuwa router.
Ilitumia FreeBSD na pfSense. Nilikuwa sijui chochote kuhusu hiyo router ilibidi niingie mtandaoni kujifunza. Nikaja kuwa mtaalamu nawanyanyasa department zingine wakizidisha matumizi (video streaming, YouTube n.k.).
Nilikuwa free sana kuweka filter za hatari firewall n.k.
Nazipiga ban device zinazo kula bandwidth kubwa, n.k.
Tulitumia LAN na wireless kwa pamoja. Naweka range flani ya IP address kwenye Dynamic IP zile za WiFi na zingine Static IP addresses
Sasa nimekaa mbali na hizo makitu nimeanza kusahau.
 
Hahahahaha ukiyaacha yanakuacha maana kila siku yanakuwa updated.
 
Watu wanadharau elimu na professionalism lakini elimu yangu ilinisaidia sana.
Nilimkuta mtu kazini anashikia department ya IT kasoma certificate na professional courses kadhaa pale Amazon sijui chuo gani kile cha wahindi maarufu karibu mnazi mmoja.
Anajua product za windows na CISCO tu.
Alikuta mifumo akakaa nayo siku nyingi lakini kazi nyingi za akili au za vitu asivyo wahi kuona darasani akashindwa kutatua changamoto.
Mimi nilitumia knowledge ya jumla ya chuo nikajifunza na kufanya vitu vingi sana advanced muda mfupi. Nika accelerate kwenye malipo na heshima. Au kuhitajika na kampuni.
Nilianza kuwa muhimu karibu department nyingi zaidi ya IT.
Hayo madudu yote uliyoweka hapa nilijifunzia practically kazini. Tena mwenyewe.
Nilijifunza hadi kazi za watu wa Finance n.k.
Nilikuwa kiraka, supersub.
 
Umesahau kitu kimoja muhimu sana

Ambacho ni power usage effectiveness

Hao watengenezaji wa router wanajua vyema pc nyingi zinaweza kufanya kile wanataka ila wanapambana usiku na mchana kupata hardwares zenye utumiaji mdogo sana wa umeme.

Unapotumia desktop kama router unaweza kuona ni rahisi na umeokoa gharama ila itafika muda gharama za umeme zinakuwa kubwa kuliko ungenunua hiyo router ya bei ghali.

Hivyo kwa project ndogo ndogo ni nzuri kujifunzia pia zipo hardware zinauzwa aliexpress zenye Ethernet port zakutosha nyingine mpaka zina SFP port kwa ajili ya fiber na zenye matumizi madogo ya umeme.

Ni hayo tu kuchangamshia mada.

Nb: pfsense nimecheza nayo sana miaka ya 2020, sijui saiv imefikia version gani ila ni nzuri sana kwa watu wa networking kupita huko kujinoa na kuchangamsha akili😁
 
Daah.
Umenikumbusha mbali Sana.
Niliajiriwa sehemu nikiwa fresh from college.
Kabla ya kumalizia kadigrii jalalani(UDSM) nilisoma CISCO CCNA pale UCC Main Campus nikaishia njiani majukumu mengi. Nilipendelea kuchapa code(programming) sasa ajira zetu za kibongo ukiwa supervisor au manager inatakiwa ujue vyote Database, Software Development, na networking.
Nikakutana na huo mfumo wa PC ya kawaida kuwa configured kuwa router.
Ilitumia FreeBSD na pfSense. Nilikuwa sijui chochote kuhusu hiyo router ilibidi niingie mtandaoni kujifunza. Nikaja kuwa mtaalamu nawanyanyasa department zingine wakizidisha matumizi (video streaming, YouTube n.k.).
Nilikuwa free sana kuweka filter za hatari firewall n.k.
Nazipiga ban device zinazo kula bandwidth kubwa, n.k.
Tulitumia LAN na wireless kwa pamoja. Naweka range flani ya IP address kwenye Dynamic IP zile za WiFi na zingine Static IP addresses
Sasa nimekaa mbali na hizo makitu nimeanza kusahau.
Kuwa IT bongo ni kama kuwa commando, na ndani ya commando Kuna category zingine, itategemea umezamia wapi Ili ukae wapi😅😅.
 
Hapa mngeniwekea mkeka (code) nadhani tungeelewana....

Nb:
Ukiona hujumbe hujauelewa, ujue hujaandikiwa wewe!

Anyway...nilikuwa nawasalimu, maExpart wa IT
 
Back
Top Bottom