Badala ya kuwawinda na kuwakamata,serikali ielekeze wafanyabiashara wa viroba wavipeleke wapi

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Ni kweli kwamba biashara ya viroba ilikuwa biashara halali,na ilikuwa na leseni zote.

Katika kipindi ambacho biashara hiyo ilikuwa halali,kuna wafanyabiashara walinunua stock kubwa na kuweka katika stoo zao wakitarajia kuziuza hapo baadae,hata miezi au mwaka mbele kutegemea na tarehe ya ku-expire kwa bidhaa.

Ghafla likatoka tangazo la marufuku,likatoa muda mfupi,nadhani chini ya mwezi,kuzuia biashara hiyo. Kwa mfanyabiashara aliyenunua mamia ya tani,ni vigumu kuuza akamaliza stock hiyo ndani ya kipindi kifupi chini ya mwezi,kwa kuwa wakati ananunua biashara hiyo ilikuwa halali.

Pia hata notice iliyotolewa(chini ya mwezi) inaonyesha kiasi gani kama taifa,hatujaziweka akili zetu kutazama maslahi ya biashara. Haiwezekani maelfu ya tani yaliyokuwa yamesambazwa na mengine kuzalishwa tayari useme yatumike ndani ya mwezi na kuisha. Kibiashara,hapakuwa na sufficent notice,notisi ya msingi isingepungua miezi mitatu kwa mzalishaji,na miezi sita kwa muuzaji wa rejareja kumaliza stoku take

HOJA YA MSINGi

Kwa nini mamlaka zinazohusika zisiwaelekeze ambao bado wana stoku kwamba watoe taarifa mahali fulani, ili baadae maafisa waende na magari yao kukusanya viroba hivyo?

Hawa wananchi sio wataalam wa kuviteketeza,wakivitupa dampo,wananchi wataokota watakunywa,sasa kwa nini mamlaka husika zisitoe maelekezo?

Wananchi wamekaa na vitu wanasubiri serikali iwaambie hivi vipelekeni kule vikateketezwe,au kama bado una mzigo to a taarifa kwa afisa Fulani.

Mtu ana box elfu kumi au ishirini alinunua kihalali,kalipa na kodi,sasa unasema hiyo biashara si halali,mwambie hayo mabox ayapeleke wapi,.

Pia tamko hilo lilitakiwa liguse viroba vilivyozalishwa siku baada ya tamko,wewe unatoa tamko kuzuia hata vilivyozalishwa mwaka Jana? Yaani utunge sheria leo imfunge mtu aliyefanya kosa mwaka 1980?

MWISHO,hawa wafanyabiashara washitaki kudai fidia
 
Viroba ni haramu. Hakuna uhalali wa kuuza viroba vinavyo maliza watu.

Kwa walio hifadhi, viharibuni. Chimbeni mashimo mmwegie au tia moto iteketee.

Kunusuru watu ni gharama nzuri na kubwa kuliko kuwa na maviroba.
 
Kwa style hii sidhani kama tuna nia ya dhati ya kuinua uchumi wa Taifa hili.Sidhani kama serikali ina nia ya dhati ya kuwasaidia wafanyabiashara wa nchi hii.

Kwa kuwa hiyo pombe ilikuwa ni biashara halali,tena iliyohakikiwa ubora wake na mamlaka husika(serikali yenyewe),serikali ilipaswa kudhibiti uuzwaji holela tu na si kuipiga marufuku....Kupiga marufuku ni sawa na kuwafilisi wote walikuwa wanafanya biashara hiyo, SIO UAMUZI MUAFAKA,kwani kupitia marufuku hiyo,Tunapoteza mapato ya kodi na pia kuua ajira za watu.

Ni aibu kubwa kama Taifa,kushabikia matamko ya hovyo na yenye kuumiza uchumi wetu kwa kisingizio eti "tunalinda afya za vijana wetu"... Sababu ya kupumbavu kabisa.

Hawa waliopewa leseni ya kufanya biashara ya vileo,ambao Leo mnawatia hasara mtawafidia kunusuru mitaji yao?
 
Viroba ni haramu. Hakuna uhalali wa kuuza viroba vinavyo maliza watu.

Kwa walio hifadhi, viharibuni. Chimbeni mashimo mmwegie au tia moto iteketee.

Kunusuru watu ni gharama nzuri na kubwa kuliko kuwa na maviroba.

Uharamu wa viroba unaanzia wapi mkuu?Kwa nini tunakuwa wepesi wa kusombwa na kauli za hovyo hovyo za hawa tunaowaita viongozi wetu?
Ina maana unataka kuniambia biashara ya vileo sio biashara halali?vipi Kofi mnayokusanya kila Leo kwa wazalishaji,wasambazaji na watumiaji wake?

Tuache unafiki,tunaliamgamiza Taiga
 
Lengo la ccm ni kuwafirisi wafanyabiashara wa pombe hiyo , maana kwanza imebainika wote wanatokea kaskazini .
 
Acheni kupotosha mambo, huo mwezi mmoja walipewa nyongeza ili waclear stoo zao tu
ila biashara ilishazuiwa tangu october/november mwaka jana
 
Back
Top Bottom