"Back to Sender" Kwa Upepo wa Kisulisuli

"Back to Sender" Kwa Upepo wa Kisulisuli

Queen Esther

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
2,206
Reaction score
1,465
" *BACK TO SENDER × 7 KWA UPEPO WA KISULISULI"*

SIKU YA LEO TUNAENDELEA NA MAOMBI YETU YA KUFUNGA NA KUOMBA TUKISIMAMA NA RAIS WETU MHE. DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

Tafadhali imba Zaburi hizi za Mfalme Daudi na iwe ni maombi yetu saa zote. Kumbuka Mfalme Sauli alivyozunguka amuangamize Mfalme Daudi, hata hivyo hakufanikiwa kwasababu KUSUDI la Mungu lilikuwa kwa Mfalme Daudi kama ilivyo kwa Rais Magufuli.

1. Zaburi 17;
2. Zaburi 35;
3. Zaburi 54;
4. Zaburi 63;
5. Zaburi 109
6. Hesabu 23

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *Zaburi 54*

1. Uniokoe, ee Mungu, kwa jina lako; unitetee kwa nguvu yako.

2. Uisikie, ee Mungu, sala yangu;
uyategee sikio maneno ya kinywa changu.

3. Watu wenye kiburi wananishambulia;
wakatili wanayawinda maisha yangu,
watu ambao hawamjali Mungu.

4. Najua Mungu ni msaada wangu,
Mwenyezi-Mungu hutegemeza maisha yangu.

5. Yeye atawaadhibu maadui zangu kwa uovu wao wenyewe;
kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize.

6. Nitakutolea tambiko kwa moyo mkunjufu;
nitakushukuru kwa kuwa ni vema.

7 Maana umeniokoa katika taabu zangu zote,
nami nimewaona maadui zangu wameshindwa.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *Zaburi 17*

1. Ee Mwenyezi-Mungu usikie kisa changu cha haki,
usikilize kilio changu, uitegee sikio sala yangu isiyo na hila.

2. Haki yangu na ije kutoka kwako,
kwani wewe wajua jambo lililo la haki.

3. Wewe wajua kabisa moyo wangu; umenijia usiku, kunichunguza,
umenitia katika jaribio; hukuona uovu ndani yangu,
sikutamka kitu kisichofaa.

4. Kuhusu matendo watendayo watu;
mimi nimeitii amri yako, nimeepa njia ya wadhalimu.

5. Nimefuata daima njia yako;
wala sijateleza kamwe.

6. Nakuita, ee Mungu, kwani wewe wanijibu;
unitegee sikio, uyasikie maneno yangu.

7. Onesha fadhili zako za ajabu,
uwaokoe kutoka kwa adui zao,
wale wanaokimbilia usalama kwako.

8. *Unilinde kama mboni ya jicho;
unifiche kivulini mwa mabawa yako,*

9. Mbali na mashambulio ya waovu, mbali na maadui zangu hatari wanaonizunguka.

10. Hao hawana huruma yoyote moyoni;
wamejaa maneno ya kujigamba.

11. Wananifuatia na kunizunguka;
wananivizia waniangushe chini.

12. Wako tayari kunirarua kama simba: Kama mwanasimba aviziavyo mawindo.

13. Inuka, ee Mwenyezi-Mungu,
uwakabili na kuwaporomosha.
Kwa upanga uiokoe nafsi yangu kutoka kwa waovu.

14. Kwa mkono wako, ee Mwenyezi-Mungu,
uniokoe mikononi mwa watu hao,
watu ambao riziki yao ni dunia hii tu.
Uwajaze adhabu uliyowawekea,
wapate ya kuwatosha na watoto wao,
wawaachie hata na wajukuu zao.

15. Lakini mimi nitauona uso wako, kwani ni mwadilifu;
niamkapo nitajaa furaha kwa kukuona.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *Zaburi 35*

1. Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;
uwashambulie hao wanaonishambulia.

2. Utwae ngao yako na kingio lako,
uinuke uje ukanisaidie!

3. Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.
Niambie mimi kwamba utaniokoa.

4. Waone haya na kuaibika,
hao wanaoyanyemelea maisha yangu!
Warudishwe nyuma kwa aibu,
hao wanaozua mabaya dhidi yangu.

5. Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6. Njia yao iwe ya giza na utelezi,
wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7. Maana walinitegea mitego bila sababu;
walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8. Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,
wanaswe katika mtego wao wenyewe,
watumbukie humo na kuangamia!

9. Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;
nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10. Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:
“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!
Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,
maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.”

11. Mashahidi wakorofi wanajitokeza;
wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12. Wananilipa mema yangu kwa mabaya;
nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13. Lakini wao walipokuwa wagonjwa,
mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;
nilijitesa kwa kujinyima chakula.
Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14. kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.
Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,
kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15. Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.
Walikusanyika pamoja dhidi yangu.
Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,
wala hakuna aliyewazuia.

16. Watu ambao huwadhihaki vilema,
walinisagia meno yao kwa chuki.

17. Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?
Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;
uyaokoe maisha yangu na simba hao.

18. Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;
nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.

19. Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,
hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20. Maneno wasemayo si ya amani,
wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21. Wananishtaki kwa sauti:
“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22. Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,
usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,
usikae mbali nami.

23. Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;
uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.

24. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee,
ufanye kulingana na uadilifu wako;
usiwaache maadui zangu wanisimange.

25. Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”
Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”

26. Waache hao wanaofurahia maafa yangu,
washindwe wote na kufedheheka.
Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,
waone haya na kuaibika.

27. Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia,
wapaaze sauti kwa furaha waseme daima:
“Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno!
Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

28. Hapo nami nitatangaza uadilifu wako;
nitasema sifa zako mchana kutwa.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *Zaburi 63*

1. Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, ninaendelea kukutafuta.+
Nina kiu kwa ajili yako.+
Ninazimia* kwa sababu ninakutamani
Katika nchi kame iliyokauka, ambayo haina maji.+

2. Kwa hiyo nimekutazama mahali patakatifu;
Nimeziona nguvu zako na utukufu wako.+

3. Kwa sababu upendo wako mshikamanifu ni bora kuliko uhai,+
Midomo yangu mwenyewe itakutukuza.+

4 . Basi nitakusifu maisha yangu yote;
Katika jina lako nitaiinua mikono yangu.

5 . Nimeridhika na fungu bora ambalo ni zuri kabisa,*
Kwa hiyo kinywa changu kitakusifu kwa midomo yenye shangwe.+

6. Ninakukumbuka wewe nikiwa kitandani mwangu;
Ninatafakari kukuhusu katika makesha ya usiku.+

7 Kwa maana wewe ni msaidizi wangu,+
Nami ninapaza sauti kwa shangwe katika kivuli cha mabawa yako.+

8 Ninashikamana nawe;
Mkono wako wa kuume hunishika kwa nguvu.+

9 Lakini wale wanaotaka kuniua*
Watashuka katika sehemu zenye kina zaidi za dunia.

10 Watatiwa katika nguvu za upanga;
Watakuwa chakula cha mbwamwitu.*

11 Lakini mfalme atashangilia kwa sababu ya Mungu.
Kila mtu anayeapa katika jina la Mungu atashangilia,*
Kwa maana kinywa cha wale wanaosema uwongo kitanyamazishwa.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
*Zaburi 109*

1 Ee Mungu ninayekusifu,+ usinyamaze.

2 Kwa maana waovu na wadanganyifu hufumbua vinywa vyao dhidi yangu.
Wanaongea kunihusu kwa ndimi za uwongo;+

3 Wananizingira kwa maneno ya chuki,
Na kunishambulia bila sababu.+

4 Wananipinga licha ya kwamba ninawapenda;+
Lakini ninaendelea kusali.

5 Wananilipa uovu kwa mema niliyotenda+
Na chuki kwa upendo wangu.+

6 Mweke mtu mwovu amhukumu;
Mpinzani* na asimame mkono wake wa kulia.

7 Anapohukumiwa, na apatikane kuwa na hatia;*
Hata sala yake ihesabiwe kuwa dhambi.+

8 Siku zake na ziwe chache;+
Mtu mwingine na achukue cheo chake cha uangalizi.+

9 Watoto wake* na wawe mayatima,
Na mke wake awe mjane.

10 Watoto wake* na watangetange wakiombaomba,
Wakitafuta chakula katika nyumba zao zilizoharibiwa.

11 Anayemdai na achukue kwa nguvu* vitu vyote alivyo navyo,
Wageni na wapore mali zake.

12 Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea kwa fadhili,*
Na asiwepo mtu yeyote wa kuwahurumia watoto wake mayatima.

13 Wazao wake na waangamizwe;*+
Jina lao na lifutwe katika kizazi kilekile.

14 Kosa la mababu zake na likumbukwe na Yehova,+
Na dhambi ya mama yake isifutwe.

15 Yehova na akumbuke daima waliyotenda;
Na afutilie mbali kumbukumbu lao kutoka duniani.+

16 Kwa maana hakukumbuka kutenda kwa fadhili,*+
Bali aliendelea kumfuatia mtu aliyekandamizwa,+ maskini, na aliyevunjika moyo
Ili amuue.+

17 Alipenda kulaani, kwa hiyo laana hiyo ikampata;
Hakupenda kubariki, kwa hiyo hakupata baraka yoyote.

18 Alivishwa laana kama vazi lake.
Nazo zikamwagwa mwilini mwake kama maji,
Mifupani mwake kama mafuta.

19 Laana zake na ziwe kama vazi analojifunika+
Na kama mshipi anaovaa daima.

20 Hayo ndiyo malipo yanayotoka kwa Yehova ya mtu anayenipinga+
Na ya wale wanaosema mambo maovu dhidi yangu.

21 Lakini wewe, Yehova Bwana Mwenye Enzi Kuu,
Tenda kwa niaba yangu kwa ajili ya jina lako.+
Niokoe, kwa sababu upendo wako mshikamanifu ni mwema.+

22 Kwa maana sina uwezo, nami ni maskini,+
Na moyo wangu umechomwa ndani yangu.+

23 Ninapitilia mbali kama kivuli kinachofifia;
Nimekung’utwa kama nzige.

24 Magoti yangu yanalegea kwa sababu ya kufunga;
Mwili wangu umekonda, unazidi kupungua.*

25 Nimekuwa kitu cha kudhihakiwa nao.+
Wanaponiona, wanatikisa vichwa vyao.+

26 Nisaidie, Ee Yehova Mungu wangu;
Niokoe kwa upendo wako mshikamanifu.

27 Na wajue kwamba mkono wako ndio uliotenda hili;
Kwamba wewe, Ee Yehova, umetenda hili.

28 Waache watangaze laana, lakini wewe toa baraka.
Na waaibishwe wanapoinuka dhidi yangu,
Lakini acha mtumishi wako ashangilie.

29 Wale wanaonipinga na wavishwe aibu;
Na wafunikwe na aibu yao kama joho.*+

30 Kinywa changu kitamsifu Yehova kwa bidii;
Nitamsifu yeye mbele ya watu wengi.+

31 Kwa maana atasimama mkono wa kulia wa maskini
Ili amwokoe kutoka kwa wale wanaomhukumu.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
*Hesabu 23*
(Hakuna uganga walanuchawi kwa Magufuli Hesabu 23:23)

1. Kisha Balaamu akamwambia Balaki: “Jenga madhabahu saba mahali hapa,+ nawe unitayarishie ng’ombe dume saba na kondoo dume saba.”

2 Mara moja Balaki akafanya kama Balaamu alivyomwambia. Kisha Balaki na Balaamu wakatoa dhabihu ya ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.+

3 Halafu Balaamu akamwambia Balaki: “Kaa hapa karibu na dhabihu yako ya kuteketezwa, nami nitaenda. Labda Yehova atawasiliana nami. Jambo lolote atakalonifunulia, nitakwambia.” Basi akaenda juu ya kilima kilicho wazi.

4 Ndipo Mungu akawasiliana na Balaamu,+ Balaamu akamwambia: “Nilijenga safu za madhabahu saba na kutoa dhabihu ya ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.”

5 Yehova akatia maneno haya katika kinywa cha Balaamu:+ “Rudi kwa Balaki, na hili ndilo utakalosema.”

6 Basi akarudi na kumkuta Balaki na wakuu wote wa Moabu wakiwa wamesimama karibu na dhabihu yake ya kuteketezwa.

7 Kisha akasema maneno haya ya kishairi:+
“Balaki mfalme wa Moabu amenileta kutoka Aramu,+
Kutoka katika milima ya mashariki:
‘Njoo umlaani Yakobo kwa niaba yangu.
Naam, njoo uwashutumu Waisraeli.’+

8 Ninawezaje kuwalaani watu ambao Mungu hajawalaani?
Ninawezaje kuwashutumu wale ambao Yehova hajawashutumu?+

9 Kutoka juu ya miamba ninawaona,
Na kutoka vilimani ninawatazama.
Wanaishi peke yao kama taifa;+
Hawajioni kuwa sawa na mataifa mengine.+

10 Ni nani anayeweza kuhesabu chembe za mavumbi ya Yakobo+
Au hata kuhesabu robo ya Waisraeli?
Acha nife kifo cha watu wanyoofu,
Na mwisho wangu uwe kama wao.”

11 Ndipo Balaki akamwambia Balaamu: “Kwa nini umenitendea hivi? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini badala yake umewabariki tu.”+

12 Balaamu akasema: “Je, sipaswi kusema neno lolote ambalo Yehova anatia kinywani mwangu?”+

13 Balaki akamwambia: “Tafadhali, twende mahali pengine ambapo unaweza kuwaona. Utaona baadhi yao; hutawaona wote. Ukiwa huko walaani kwa niaba yangu.”+

14 Kwa hiyo akampeleka kwenye uwanja wa Sofimu, juu ya Pisga,+ naye akajenga madhabahu saba na kutoa dhabihu ya ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.+

15 Kisha Balaamu akamwambia Balaki: “Kaa hapa karibu na dhabihu yako ya kuteketezwa ninapoenda pale kuwasiliana Naye.”

16 Basi Yehova akawasiliana na Balaamu na kutia neno hili kinywani mwake:+ “Rudi kwa Balaki, na hili ndilo utakalosema.”

17 Basi akarudi na kumkuta Balaki akisubiri karibu na dhabihu yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu walikuwa pamoja naye. Balaki akamuuliza: “Yehova amesema nini?”

18 Kisha Balaamu akasema maneno haya ya kishairi:+
“Inuka, Balaki, usikilize.
Nisikilize, ewe mwana wa Sipori.

19 Mungu si mwanadamu anayesema uwongo,+
Wala si binadamu anayebadili nia yake.*+
Akisema jambo, je, hatalitenda?
Akinena jambo, je, hatalitimiza?+

20 Tazama! Nimeletwa ili nibariki;
Sasa Yeye amebariki,+ nami siwezi kubadili.+

21 Havumilii nguvu zozote za uchawi dhidi ya Yakobo,
Wala haruhusu taabu yoyote impate Israeli.
Yehova Mungu wake yuko pamoja nao,+
Nao humsifu kwa sauti kubwa kuwa mfalme wao.

22 Mungu anawatoa Misri.+
Yeye ni kama pembe za fahali mwitu.+

23 Kwa maana hakuna ishara za msiba dhidi ya Yakobo,+
Wala hakuna uaguzi* wowote dhidi ya Israeli.+
Sasa inaweza kusemwa hivi kumhusu Yakobo na Israeli:
‘Tazameni mambo ambayo Mungu ametenda!’

24 Watu hawa watainuka kama simba,
Na kama simba, watajiinua.+
Hawatalala chini mpaka wale mawindo
Na kunywa damu ya waliouawa.”

25 Ndipo Balaki akamwambia Balaamu: “Ikiwa huwezi kamwe kuwalaani, basi usiwabariki pia.”

26 Balaamu akamwambia Balaki: “Je, sikukwambia, ‘Nitafanya mambo yote ambayo Yehova anasema’?”+

27 Ndipo Balaki akamwambia Balaamu: “Tafadhali njoo nikupeleke mahali pengine. Labda Mungu wa kweli atakubali uwalaani kwa niaba yangu kutoka mahali hapo.”+

28 Basi Balaki akampeleka Balaamu juu ya Mlima Peori, unaoelekeana na Yeshimoni.*+ 29 Kisha Balaamu akamwambia Balaki: “Jenga madhabahu saba mahali hapa, nawe unitayarishie ng’ombe dume saba na kondoo dume saba.”+ 30 Kwa hiyo Balaki akafanya kama Balaamu alivyomwambia, naye akatoa dhabihu ya ng’ombe dume mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿Zaburi 17:8
Unilinde kama mboni ya jicho;
unifiche kivulini mwa mabawa yako,*

Mungu mwenyewe akulinde Rais Magufuli kama anavyoilinda mboni ya jicho lake.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *Zaburi 118:13*
Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini BWANA akanisaidia.

Rais Magufuli watesi wamekusukuma sana ili uanguke, Mungu ameachilia KISASI sasa watajikwaa na kuanguka wao tena mara saba.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿 *Wafilipi 1:6*

Basi, nina hakika kwamba Mungu aliyeanza kazi hii njema ndani yako (Rais Magufuli,) ataiendeleza mpaka ikamilike katika siku ile ya Kristo Yesu.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
*Zaburi 27:12*

Usinitie katika nia ya watesi wangu; Maana mashahidi wa uongo wamenijia, Nao watoao jeuri kama pumzi.

Mwisho
Rais Magufuli usilipe kisasi. Kisasi ni cha Mungu. Mfalme Daudi alimwachia Mungu na ndipo maadui zake wote waliangamizwa na Bwana.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
1 Samweli 25:39

Na ahimidiwe BWANA ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumwa wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali BWANA amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe….”

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
*Warumi 12:19*

“ Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.”

Rais Magufuli moyo wa mtu ni kichaka. Wema na wabaya anawajua Mungu. Hivyo mwache Mungu ashughulike nao kwa mkono wake wenye nguvu.

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
*Kutoka 14:13*

Musa (Magufuli) akawaambia watu (Watanzania), Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.

AMEN; AMEN; AMEN

Queen Esther
 
Hahhaaaa Nadhani sasa mmejifunza mambo ya kujimwambafai hayana maana yoyote, kama mtu anakupinga kwa hoja tu za maneno mjibu kwa hoja za maneno sio mitutu na mabomu na kutesana.

Wikii hii tumeona jinsi wanaCCM na praise team walivyokuwa wanyonge....wadogoooo kama piritoni.

Hahahahhaaaa Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mtamu
 
Hahhaaaa Nadhani sasa mmejifunza mambo ya kujimwambafai hayana maana yoyote, kama mtu anakupinga kwa hoja tu za maneno mjibu kwa hoja za maneno sio mitutu na mabomu na kutesana.

Wikii hii tumeona jinsi wanaCCM na praise team walivyokuwa wanyonge....wadogoooo kama piritoni.

Hahahahhaaaa Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mtamu
Tulikuwa tunawachora tuuu!! Sasa mseme hiyo maiti iliyoko Ujerumani ni ya nani? Rais wetu Magufuli tumemwona live. Na waswahili wanasema kaburi halifukiwi bila mwili.
Sasa mjiandae kutumbulia kwenye mashimo mliyoyachimba.

Queen Esther
 
Kwa uzi huu ukipewa buku saba si utakuwa umedhulumiwa?
 
peke yako... tuliishi kwa raha zetu...
Aibu kwa wachawi mliokesha makaburini
Hahhaaaa Nadhani sasa mmejifunza mambo ya kujimwambafai hayana maana yoyote, kama mtu anakupinga kwa hoja tu za maneno mjibu kwa hoja za maneno sio mitutu na mabomu na kutesana.

Wikii hii tumeona jinsi wanaCCM na praise team walivyokuwa wanyonge....wadogoooo kama piritoni.

Hahahahhaaaa Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mtamu
 
Back
Top Bottom