Baby Tanzania naogopa utafumaniwa

Baby Tanzania naogopa utafumaniwa

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
2,953
Reaction score
2,044
Mfano ukiamua utoke leo siku ya valentine utatoka na nani,una wapenzi kibao wengine umefanya mikataba nao chumbani,ile ya richmond hadi leo aijatutoa gizani,

Nakushauri tu ili wasikupate zima simu,umeingia ubia na mabwana kibao kumkomesha TTCL aloshindwa kukutunza umekuja na voda,airtel,tigo zantel na bado pia huduma zao zinatukata stimu.

leo niambia utatokaka na nani sasa,utaoga nini huna hata maji ya uhakika japo umemkubali DAWASCO na ukamtosa DAWAS,huna lolote,mmarekani,mchina,mwarabu we unabeba yoyote,leo utatoka na nani na we cha wote,ulivutia kama tausi juu ukipaa,etc wamekuchakachua hadi umechakaa,

kila kiungo chako kilikuwa imara,ukialikwa uende vijiji vya mbele na Ifakara,kaangalie majanga ya kuhairishwa kwa safari sio reli ya kati mda si mrefu kwa tamaa yako tutaizika hadi TAZARA,una mengi ya kujibu ila unajarbu kukwepa,mabilion ya EPA,wanao si wazalendo wanawakandamiza watanzania wenzao nnje matirion wanayaweka,huu ufukara gani tulio nao wa kusaidiwa neti mpaka na mikeka.

Malawi wamekugusa ziwani unacheka
 
what nonesense have you written??!

nimejaribu tu kufikiria na kujaribu kuunganisha mambo,leo ni valentine,nkawaza nnchi yetu na wabia wake.leo ndio angeambiwa atoke na mmoja wapo out angemchagua nani..ni ubunifu tu.si lazima kikupendeze wewe,wengine wanaweza pendezwa, kama jamii forum n uwanja mpana wa great thinkers hii iko sawa inaruhusiwa
 
nimejaribu tu kufikiria na kujaribu kuunganisha mambo,leo ni valentine,nkawaza nnchi yetu na wabia wake.leo ndio angeambiwa atoke na mmoja wapo out angemchagua nani..ni ubunifu tu.si lazima kikupendeze wewe,wengine wanaweza pendezwa, kama jamii forum n uwanja mpana wa great thinkers hii iko sawa inaruhusiwa
Asiyejua maana haambiwi maana. Watu kama hao unapotezea, wameshazoea posti za kibongo fleva ndio wanaelewa.
 
Hapa mbona kama unamnanga mjomba anayehangaika na vifo vya ndovu huko ughaibuni...
 
Back
Top Bottom