Baby Madah afunguka 'michezo michafu' ya Industry

Baby Madah afunguka 'michezo michafu' ya Industry

Sasa prodyuza mkongwe si aambatane na msanii mkongwe mwenzie watoe kongwe kali? Madaha asizingue kachuja. Naujua wimbo wake mmoja tu na ni classic hadi dahari, nao ni Amore. Angefululiza na ukali huo angekuwa juu bado. Ajipange hata atoe Amore remix basi
 
2026

Legendary Sunday Linex, anaweza kuwa mhanga wa michezo michafu ya industry ya kudidimiza nyota na kipaji alichonacho msanii huyu mTanzania

Linex - Kwa Hela (official video)

 


Msanii tajwa fani ya muziki na filamu Baby Madaha aelezea changamoto zinazoua wasanii ktk fani zao ni za kimfumo.

Baby Madaha anashangaa kuwa msanii wa umri wa miaka 36 hapa Tanzania anahesabika ni kama gari la namba plate TZA wakati huko Marekani ya Kaskazini, Latin Amerika Ulaya, Mashariki ya Kati na Asia jambo la mtu kuwa na kipaji haliangalii umri bali uwezo wa kuitumikia fani ndiyo jambo la msingi.


Msanii wa kimarekani fani ya muziki Dolly Parton aliyezaliwa mwaka 1946 na sasa 2022 ana umri wa miaka 76 bado yupo juu katika fani na anaheshimiwa na kualikwa kufanya kazi za matamasha na wadau wa rika zote

View attachment 2191943


Mbali ya wasanii waimbaji haya watayarishaji wa muziki yaani maproducer wa umri mkubwa kama Quincy Jones wanaheshimika huko mbele na wanatafutwa na wadau wa rika zote wafanye kazi na Quincy Jones



Baby Madaha anaongeza kuwa mchawi wa kupunguza kasi ya ubunifu wa kazi za wasanii wa kiTanzania kuendelea mbele ni sisi wenyewe. Wenzetu huko ma-mbele wanaendeleza waliotangulia na kuongezea walipofika na wa jana wanashirikiana na wale wa leo katika industry iwe artists, promoters, producers, sponsors, media platforms owners, audiences na kwa pamoja wanaendeleza industry kupanuka ndani na kimataifa kwa kazi bora zaidi .

Baby Madaha anasikitika sana na hali hii pamoja ya kuwa sasa dunia imefunguka kwa kuwepo media platform huru zisizo na mageti ya kufungia vipaji vya wasanii wa kiTanzania vilivyopo lakini kiroho bado kuna vita ya 'uchawi' kufifisha vipaji vya wasanii wetu Tanzania


Latino America : Buena Vista Social Club - Chan Chan



Industry ya kiTanzania ya music na entertainment pia inaenzi wanamuziki wa nje kwa kualika wanamuziki au bendi toka nje na kufifisha muziki wetu wa dansi ya kitambaa cheupe ambao unaheshimika sana hapa ndani na kimataifa lakini industry yetu tunaudharau kwa kuubania pia muziki wa dansi

"Kitambaa Cheupe" - King Kikii na Wazee Sugu


Wasani wa huko ma-mbele ni sawasawa na mvinyo- mvinyo unakuwa Bora na wa gharama zaidi unapozeeka.
Wasanii wa Bongo sasa wao ni sawa sawa na mbege...masaa 24 tu imeishakuwa "Ngera" Haina thamani tena na ukiinywa Ngera tu utashinda chooni.
 
2026

Legendary Sunday Linex, anaweza kuwa mhanga wa michezo michafu ya industry ya kudidimiza nyota na kipaji alichonacho msanii huyu mTanzania

Linex - Kwa Hela (official video)


Wasanii wenye viburi watafute kazi nyingine za kufanya. Huyo Linex na kina Nikki Mbishi wanaponzwa na ujuaji. Kwenye sanaa na michezo dunia nzima lazima kuna wadau lazima wafaidike. Kwa mfano kwenye riadha tunasikia kila siku Simbu na Geay inamaanisha wale vijana ni wajanja washajua wakila peke yao ndo kujistaafisha mapema.
 
Back
Top Bottom