Baby come back. . .

Baby come back. . .

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,010
Reaction score
60,472
Wasalaam jamani.

Kuna watu ambao mahusiano yao yametawaliwa na
"baby come back/baby please stay" miaka nenda rudi. Kuachana na kurudiana ni jambo la kawaida kwao maana kila mmoja anamjulia mwenzake. Akiondoka mama atabembelezwa atarudi, akitaka kuondoka baba atawekwa sawa ataahirisha. Haijalishi kama mmoja wao au wote wataamua kuanza mahusiano na mtu/watu wengine katika kipindi chao cha mpito, mwisho wa siku mmoja akimgeukia X(pired) wake wanarudiana upya tena jumla.

Nwy. . .swali langu ni hiviii, nini haswa kinachowasukuma watu kwenda na kurudi pale pale walipopakimbia over and over again? True love? Utegemezi/ utumwa wa kihisia? Uchanga kwenye swala zima la mapenzi? Kutokujitambua?
Inawezekana wawili hao wakawa wote hawajitambui? Kila mmoja akawa mtumwa/tegemezi kwa mwenzie kihisia kweli?

NB Missed you sana people. Wale wapenzi wa ZAWADI nipeni support bana, nataka nifanye kweli nitoe kitabu au hata filamu kabisa M'Mungu akijalia.
 
Lizzy hata siredi yako siisomi kwanza
karibu sana aise we missed you a lot
Long time dear
karibu sana
Siredi yako nitasoma baadae
 
Last edited by a moderator:
wewe hayo maisha ya watu yanakuhusu nini??na umiza kichwa utunge hicho kitabu chako sio kuunga unga sentensi za watu na pima akil yako utumbie ni futi ngapi?
 
swali langu ni hiviii, nini haswa kinachowasukuma watu kwenda na kurudi pale pale walipopakimbia over and over again? True love? Utegemezi/ utumwa wa kihisia? Uchanga kwenye swala zima la mapenzi? Kutokujitambua?
Inawezekana wawili hao wakawa wote hawajitambui? Kila mmoja akawa mtumwa/tegemezi kwa mwenzie kihisia kweli?

Yote uliyoyataja yanaweza kuwa ni sababu na hutofautiana baina ya mtu na mtu, mahusiano na mahusiano.
 
Wasalaam jamani.

Kuna watu ambao mahusiano yao yametawaliwa na
"baby come back/baby please stay" miaka nenda rudi. Kuachana na kurudiana ni jambo la kawaida kwao maana kila mmoja anamjulia mwenzake. Akiondoka mama atabembelezwa atarudi, akitaka kuondoka baba atawekwa sawa ataahirisha. Haijalishi kama mmoja wao au wote wataamua kuanza mahusiano na mtu/watu wengine katika kipindi chao cha mpito, mwisho wa siku mmoja akimgeukia X(pired) wake wanarudiana upya tena jumla.

Nwy. . .swali langu ni hiviii, nini haswa kinachowasukuma watu kwenda na kurudi pale pale walipopakimbia over and over again? True love? Utegemezi/ utumwa wa kihisia? Uchanga kwenye swala zima la mapenzi? Kutokujitambua?
Inawezekana wawili hao wakawa wote hawajitambui? Kila mmoja akawa mtumwa/tegemezi kwa mwenzie kihisia kweli?

NB Missed you sana people. Wale wapenzi wa ZAWADI nipeni support bana, nataka nifanye kweli nitoe kitabu au hata filamu kabisa M'Mungu akijalia.

Nafikiri wengi wanaofanya hivyo wana hulka ya kufikiria kuwa hawa wanaoishi nao either wamepungukiwa kitu fulani au wameshindwa kuwavumilia kwa sababu fulani fulani na hivyo kufikiria kuacha mahusiano na kwenda kuanza maisha mengine na mtu mwingine. Mwisho wa siku wanakuja kugundua kuwa, yule wa mwanzo alikuwa na nafuu zaidi hata kuliko mpya na hivyo inamlazimu kurudi kwenye maskani yake ya mwanzo.

Haya ni matatizo ambayo huwapata watu ambao hawapendi kufikiria au kuvumilia changamoto za ndani ambao pia ni wepesi wa kurubuniwa na watu lakini wana mioyo iliyowazi kujutia makosa na kukumbuka walikotoka. Ila binafsi, mtu akinimwaga, akaanza uhusiano na mtu mwingine, akirudi kwangu abadani asilani, sintamkubali kamwe!
 
Lizzy hata siredi yako siisomi kwanza
karibu sana aise we missed you a lot
Long time dear
karibu sana
Siredi yako nitasoma baadae
Mimi zaidi Mr Rocky
. . . . twende kazi basi.

wewe hayo maisha ya watu yanakuhusu nini??na umiza kichwa utunge hicho kitabu chako sio kuunga unga sentensi za watu na pima akil yako utumbie ni futi ngapi?

Wewe yako ni mm ngapi vile? 1.5?
 
Last edited by a moderator:
Hayo mambo ya kurudiarudia inaashiria tabia za huyo mtu kuwa hakuna mtu anayeweza kuwa nae for long....ndo maana anarudi kwa mtu wake ambae amezoea kuyakubali, lakini mambo ya aina hii huwa hayawapi heshma au hakupishi heshima kama wewe ndo umezoea kusamehe kila siku, usifikiri akirudiana ndio kuna jipya mambo ni yale yale....
 
Lizzy kuna mengi aise yanakukumbusha kwa X wako japo nauita ni ulimbukeni ila hiyo nenda rudi bana ahhh ina mwisho wake
Wengine ni utegemezi ambao unajikuta mtu alikuwa anamtegemea mtu wake kwa kila kitu sasa kuondoka anajiona kuna kitu amekosa
Wengine ni basi tuu hata huko alikoenda kuzunguka anajiona hajafika wala hajafikishwa alipokuwa anataka
Anaona bora afanye mchezo wa abracadabra huenda mambo yakawa sawa ila akirudi anakuta bado no ni ile ile hakuna lililobadilika
 
Last edited by a moderator:
True love!

Hmmm. . .talking from experience?

Nafikiri wengi wanaofanya hivyo wana hulka ya kufikiria kuwa hawa wanaoishi nao either wamepungukiwa kitu fulani au wameshindwa kuwavumilia kwa sababu fulani fulani na hivyo kufikiria kuacha mahusiano na kwenda kuanza maisha mengine na mtu mwingine. Mwisho wa siku wanakuja kugundua kuwa, yule wa mwanzo alikuwa na nafuu zaidi hata kuliko mpya na hivyo inamlazimu kurudi kwenye maskani yake ya mwanzo.

Haya ni matatizo ambayo huwapata watu ambao hawapendi kufikiria au kuvumilia changamoto za ndani ambao pia ni wepesi wa kurubuniwa na watu lakini wana mioyo iliyowazi kujutia makosa na kukumbuka walikotoka. Ila binafsi, mtu akinimwaga, akaanza uhusiano na mtu mwingine, akirudi kwangu abadani asilani, sintamkubali kamwe!
HP nimekusoma, ila naomba kuuliza kwanini hutomkubali mtu aloenda na kurudi kwako? Na je kama unampenda sana bado utamkatalia?
 
Hmmm. . .talking from experience?

HP nimekusoma, ila naomba kuuliza kwanini hutomkubali mtu aloenda na kurudi kwako? Na je kama unampenda sana bado utamkatalia?

Siwezi kumkubali kamwe, kwa sababu kama yeye alikuwa na mapenzi kwangu alipaswa kunivumilia au kuniweka chini tukazungumza na kuyarekebisha hayo ili mapendo yaendelee. Kitendo cha kuniacha na kuambatana na mwingine kinaonyesha hali ya tamaa na kukosa mapenzi ya kweli.

Fikiria kipuuzi tu, kama aliniacha kwa tabia zangu fulani fulani ambazo zilimkera, akaanza uhusiano mpya na mtu mwingine, kinachokuja kumrudisha kwangu ni kipi tena? kwenu nitakuwa nimebadilika? Mimi si yule yule aliyenimwaga? Na je akimpata mwingine tena atakayemuona anafaa zaidi yangu, si anaweza kuniacha tena? Nitageuzwa spare tyre mpaka lini? Si bora nimwache aende moja kwa moja "kupunguza msongamano, hata kama zamani nilipenda" kama 20% alivyoimba?
 
Daaaaa....ulikuwa lupango nini my dear!
Halafu hiyo tabia yako ya kutoweka hivyo uiache tunakumisi bhana...

Back to the point waswahili wanasema awali ni awali hakuna awali mbovu!!
my be hiyo inaaply.... see u sometimes later...
 
Ulimbukeni wa mapenzi ndio unachangia haya....tatizo dogo la kuongea na kumaliza wanatumia shortcut kuachana baada ya muda mfupi huko nako yanawashinda wanarudiana tena. Usishangae ikawa ndio mfumo wao milele.
 
Back
Top Bottom