Habari zilizoandikwa katika magazeti na kusikika katika redio na Televisheni siku kadhaa zilizopita zilieleza kwamba Babu wa Loliondo ameoteshwa na Mungu dawa ya kuwatibu watu magonjwa sugu.
Wachunguzi na wataalam wa masuala ya kiroho wamegundua kuwa ndoto hiyo ni ya uongo kulingana na Neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia 23:25-32. Neno la Mungu (Biblia) katika mistari hiyo linasema hivi:
"Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto. Je, mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao...Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA...Basi kwa sababu hiyo...mimi [NIKO KINYUME]na manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema, Yeye asema. Tazama, mimi [NIKO KINYUME] na hao wanaotabiri ndoto za uongo, asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala hawatawafaidia watu hawa hata kidogo, asema BWANA."
Katika mistari hiyo, BWANA Mungu anazifananisha ndoto na makapi. Hazina maana. Neno lake(ngano) ndilo lenye maana. Maandiko hayo yanaonyesha wazi kuwa Mungu hajamtuma babu kusema wala kufanya hayo anayoyafanya sasa na kwa sababu hiyo yuko matatani au hatarini maana Mungu yuko kinyume naye sasa.
Vyanzo vingine vya habari kutoka nje ya nchi, vimethibitisha kuwa huyo babu wa Loliondo ni nabii wa uongo.
NDUGU YANGU MPENDWA INGE KUWA VEMA KAMA UNGETUMIA JINA LAKO HALISI BADALA YA KUFICHA: HUJUI KWAMBA HIYO NI SAWA NA KUFANYA JAMBO GIZANI ILI USIONEKANE. UNAMWAMBIA BABU MWONGO WAKATI WEWE UMETUMIAJINA LA UONGO HUMU JF . UNAJUA IMEANDIKWA NINI WAFANYAYE MAMBO GIZANI. KAME KWELI WEWE NI MKWELI TAJA JINA LAKO, NA DHEHEBU LAKO KAMA SI WATU WALE WALE. NI WIVU TU