Babu wa Loliondo sasa yuko hatarini...



Si vizuri kupotosha maneno ya Mungu. Soma injili utaona Yesu alisema nini kuhusu dhambi, alipomwambia yule mgonjwa 'Nenda umesamehewa dhambi zako' Waliokuwepo wakakwazika akawauliza mnashangaa nini? Je hamjui kuwa mwana wa Adamu aweza kusamehe dhambi? Je ni kipi rahisi kusema umesamehwewa dhambi zako au enenda umepona? Hapo alikuwa anamaanisha nini? Go back to Genesis; kabla ya anguko la mwandamu hakukuwa na ugonjwa wala kifo kwani roho ya Mungu ilikuwa ndani ya mwanadamu. Alipokosa utii dhambi (roho ya Ibilisi) iliingia ndani yake na roho ya Mungu ikaondoka na ndipo magonjwa adha na shida yakwa ndiyo matunda ya kazi ya roho ya Ibilisi ndani yake. Bila dhambi hakuna magonjwa na wala Mungu hata siku moja haleti magonjwa bali maovu yetu. Ndiyo maana Yesu anaweza kusame dhambi maana yeye ndiyo huo utakaso kwani damu yake aliyomwaga msalabani ndiyo yenye nguvu ya kutusafisha dhambi zetu zilizo nyekundu kama bendera kuwa nyeupe kama theluji na miyo yetu migumu kama jiwe kuwa laini kama sufi.

Unaongelea asitumie jina la Yesu je wajua kwamba hakuna njia kweli ama uzima pasipo Yesu? Jina la Yesu ndiyo jina kuu kuliko majina yote. Kwa serikali ya Tanzania Jina la Jakaya Kikwete ndilo jina kuu kupita yote siyo kwasababu ni mtoto Wa Kikwete no kwasababu ya authority aliyonayo ya kuamri majeshi yote nayo yakafanya kama atakavyo amuru kwa kufuata katiba ya Jamuhuri ya Tanzania. Basi na kwajinsi hiyo hiyo jina la Yesu ndilo jina pekee mbinguni na duniani lenye uwezo wa kuamrisha majeshi yote ya Mungu kufanya kama anavyoelekeza kwafuata wisdom ya Mungu (Roho mtakatifu). Ndiyo maana kwa jina hilo tunaujasiri wote maana tukilitumia twaweza fanya chochote kama tu tutafanya kufuatana kwa maelekezo ya roho mtakatifu ambaye anakaa ndani yetu; kwa hivyo kwa neno au kwa tendo twaenenda sawa sawa na mapenzi yake. Na mapenzi yake ni haya kila roho ya mwanadamu iirithi uzima wa milele ambao haupatikani katika jinsi yoyote isipokuwa kwa kuliamini hili jina.

Mimi nikisema kwajina la Yesu hakuna uponyaji utakao fanywa na Babu wa Semunge na ndani yake Mungu akaona nimefanya kwa sifa na utukufu wake na siyo kwaajili ya self motives kama kukosa wateja wa kanisa langu au mafungu yao ya kumi na sadaka; inakuwa hivyo no less or more. Maana kila malaika atafuata order yangu. Neno la Mungu linasema hatupati tuviombavyo kwasababu twaomba vibaya kwaajili ya tamaa zetu za kimwili na kuwa maovu yetu yametufarakanisha na Mungu hivyo hata tukiomba yeye hasikii. Ndipo akasema ninyi mkiwa ndani yangu na maneno yangu yakiwa ndani yenu ndipo sasa ombeni lolote kwa jina langu baba atawapeni; hata sasa hamjaomba lolote ombeni nanyi mtapokea ili furaha yenu iwe kamili. Kwa ufupi wengi wetu tunaomba kwa selfish motives, kwamba ili mimi ndiyo nionekane mtakatifu kuliko wote na watumishi wengine wawe second class; ili kuwaumiza wengine e.g mimi ni mkristo naomba nguvu za Mungu ziwe juu yangu ili waislamu na wale wasio wa dini yangu wakome; niwe na afya ili nistarehe na wanawake na ulevi bar; nipate cheo ili watoto wangu wasipate shida na mimi niukate. Nifaulu ili watu wote waniite mimi genious na hivyo nikiwa profesor basi wanikome hapo University hasa wale wanaojidai wao ndo vichwa; Nioe mke mzuri kupita wote ili watu wote wajue mimi pamoja na sura yangu mbaya ni mwanaume wa nguvu etc..Hatusemi hadharani lakini Mungu ajuaye roho ya mwanadamu ajua yote ndiyo maana kwa upendo wake hutunyima hizo zote ili hatimaye tubaki tukimtegemea yeye na kuurithi uzima wa milele.

Amri ya Mungu imekamilika katika upendo maana katika pendo hakuna awezaye kutenda dhambi. Ukimwadhibu mtu kwasababu hiyo tabia inamsababisha huyo kutenda dhambi na kuumiza wengine Mungu yuko pamoja na wewe na ndipo utashangaa binadamu wote watakuchukia lakini baraka zitakufuata na kupitiliza hata usiwe na sehemu ya kuziweka. Lakini ukiacha kuadhibu mtu kwasababu unajua ukifanya hivyo utavuruga mahusiano yako na deal zako za kifisadi basi hata kama ukijipa kila aina ya heshima zote zitageuka kukuzomea na hatimaye utajiona mpweke usiyependwa na yeyote na hatimaye kuishia kulipiza kisasi ambacho nacho hatima yake ni kukugeukia wewe na njia zote ulizotumia kukumaliza wewe mwenyewe huku wale uliowatuhumu pasipo sababu wakiendelea kuheshimiwa na kuinuliwa mbele ya macho yako.

Be blessed!
 

Babu angesema anafanya biashara ya dawa tungekaa kimya. Lakini kwakuwa anadai hiyo ni huduma aliyopewa na Mungu lazima tumpinge kadri tuwezavyo. Mungu hafanyi biashara ya uponyaji. Ni wapi katika Biblia Yesu aliwaponya wagonjwa baada ya kupokea senti? MTAIJUA TU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU!!
 
Hizo hoja hazinihusu mimi. Unapoteza muda wako kuziandika. Am not a Pastor, am not a Bishop. Am a mediaman, Sir. My job is to use media to tell people the truth.
 
Hv Mediaman ni mmoja kt ya waumini wa kanisa gani? Maana nahisi ni mmoja kt ya wale waliopungukiwa na waumini hapo kwake. Mmmm!
 

I am sorry this is a wrong quote; Your is okay!
 
 
CRAP! CRAP! CRAP!!

Mbona husemi nabii wa ukweli tutamjuaje au ni wivu wa kiinjili? Kama kawaida yenu wahubiri wengi mmekuwa mkituchakachua mnalazimishia hisia zenu kuwa maono... sipati picha siku ya mwisho... nyinyi ni nani hata mtoe hukumu

Hebu tutumie lgic hii... hawa wahubiri wengine ambao tunaona kila ishara ya ,maisha ya ufahari wanatoa wapi hizo pesa? Magari ya ajabu ajabu na miradi mikubwa mikubwa... acheni bwana maana kila mtumishi atakula katika utumishi wake... yeye hapokei sadaka isiyo na kikomo kama wengine... hachangishi wala hahitaji zile mnazoziita mbegu... kinachowauma ni nini hasa? Msitizame ya mwili na kutuhadaa acheni

Kristo ni mmoja tu na atabaki kuwa yeye yule jana leo na hata milele sasa nyinyi wanadamu mnajipachika kila majina na makundi kedekede na wengine makundi hayo ya kikiristo ya 'kiroho' kama mngethamini kile alichosema mngekuwa mnaungana bila kuhangaikia utukufu, kwani kanisa likiwa na manabii hamsini kuna ubaya gani?

Wacha Crap zako mpendwa unatukwaza sana
 
Mtakitukana sana Kibabu na mifano kibao na kujifanya mnajua sana Biblia kuzidi hata watu wa Roma walioitangaza Biblia dunia hii.

Mtabwabwaja na kuchonga sana nye watu wa roho Mbaya ..............

Ila ukweli ni kuwa KIBABU kinadunda na Mia yake kwa kila mteja (Katika 500, anachukua 100 tu).....

Na nyie Wezi na Vibaka kwa kutumia jina la YESU, mtashangaa Makanisa yenu yanakuwa tupu.....

LOOSERRRRRRR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!



Pichani: Waziri William Lukuvi na Rosemary Nyerere, wakipata dawa kwa Babu bila mkaruzo....

Weee sasa nenda kawaambie hao nao kuwa hawana akili.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

WAKATI mamia ya watu wakiendelea kumiminika kupata tiba ya dawa ya magonjwa sugu kwa mchungaji wa KKKT katika Kijiji cha Samunge, Wilayani Loliondo, jana ilikuwa zamu ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (pichani) kupata kikombe cha babu huyo.

Hatua ya Sumaye ni mwendelezo wa uwazi kwa viongozi wanaokwenda Samunge siku za karibuni tofauti na awali ambao baadhi ya vigogo walidaiwa kwenda kupata tiba hiyo kwa kificho.Lakini, kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye alifika Samunge, Loliondo siku tatu zilizopita na kunywa kikombe cha Babu, jana Sumaye naye alifika kijijini hapo kunywa kikombe hicho.

Akiongozana na watu kumi wa familia yake, Sumaye alifika kijijini Samunge saa 7 mchana ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Elias Wawalali ambaye kwa kutumia njia maalumu ya viongozi alipelekwa moja kwa moja kwa Mchungaji Mwasapile na kunywa dawa hiyo.
 
nashindwa waelewa hao wanaompinga babu nawafananisha na wale wenye makanisa waliokimbiwa na waumini wao kwenda kupata tiba cha msingi ni uponyaji tu hasa na kwababu hana ushawishi pata kikombe nenda zako hamna amia kanisa ili wala nenda kanisa lime baki na imani yako tu
 



uufffff!!!!!!
 
Kwa kutumia Biblia unaweza ku-justify the un-justifiable ukiwa na mind ya kupotosha....Nimeweka post yenye kuhoji ambayo inahitaji neno zaidi ya kutoa maneno tu

JE UNA DEVINE REVELATION KUWA BABU HAJAPATA MAONO YA KIMUNGU?? Au unaongea kama Mafarisayo waliokuwa wakitumia Torati kupitezea ukweli wa Yesu kuwa mwana wa Mungu na kuja kutekeleza jukumu la ukombozi

Kama HUNA DEVINE REVELATION (kikata maneno kikuu) better keep quite mpaka watakaopata Reveleation waje

https://www.jamiiforums.com/jf-chit...asiri-wa-kimaono-wa-kupinga-tiba-ya-babu.html

 
Mediaman wewe ni Mwongo:
1. Wewe ndiye uliyeanzisha thread nyingine isemayo: Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na shetani. Ukweli ni kuwa hakukuwa na siri yoyote isipokuwa mahubiri yako ukitumia maandiko kama unavyopenda yasupport hoja yako. Na hapa unakuja na thread nyingine eti Babu wa Loliondo yupo hatarini ... Hatari gani? Kichwa cha habari yako hakina tofauti na vichwa vya magazeti ya alasiri na dar leo au na magazeti ya udaku. Kichwa kingine habari nyingine.
2. Hapa unasema: Wachunguzi na wataalam wa masuala ya kiroho wamegundua kuwa ndoto hiyo ni ya uongo.Je, wewe ndiye mchunguzi huyo? Habari yako haina reference hata moja ya mchunguzi wa mambo ya kiroho na taarifa yake inasemaje? Ninachoona ni porojo zako zisizoenda shule na ambazo zina mwegemeo wa mafundisho ya Biblia yaliyo nusu nusu.
3. Kwa kutumia Yeremia 23:25-32, unajaribu kushawishi watu kuwa Mungu haoteshi watu ndoto kipindi hiki kwa vile ni makapi: Katika mistari hiyo, BWANA Mungu anazifananisha ndoto na makapi.Huu ni upotoshaji wa Biblia wa waziwazi. Petro katika Mdo 2:17 alimnukuu Nabii Yoeli na alisema : Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho wa yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Je, andiko hili haliko kwenye Biblia yako? [Kwa bahati mbaya sana kama unaamini juu ya litera translation ... basi ni wazee ndo wanaota ndoto na hapo kwa babu ndo imefika].
4. Unasema: Vyanzo vingine vya habari kutoka nje ya nchi, vimethibitisha kuwa huyo babu wa Loliondo ni nabii wa uongo - Unaendeleza uongo wako kwa kusingizia vyanzo vingine kutoka nje ya nchi - vyanzo gani hivyo? Acha kutuzuga hapa? Kama una vyanzo sema nani na nani kasema nini kwa ushahidi upi?

Nasisitiza: Mediaman ni mwongo kwa vile anajitahidi kutafuta kuungwa mkono na watu ambao hawapo. Biblia inasema: Bali maneni yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu (Mat 5:37).
Na kwavile Mediaman umethubutu kusema uongo basi wewe ndiye mtumishi wa shetani. Yesu alisema: Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuuaji tangu mwanzo ; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa huo. (Yon 8:44).
Nafurahia zaidi inavyosomeka kiingereza: (John 8:44) - You belong to your father, the devil, and you want to carry out your father's desire. He was a murderer from the beginning, not holding to the truth, for there is no truth in him. When he lies, he speaks his native language, for he is a liar and the father of lies.
 
MediaMan bado naendelea kutafakari some of the issues in your post naona havina muelekeo wa kuweka ukweli zaidi

Unapohoji mtu kupata uhalali kwa kuwa amebatizwa maji mafupi unamaanisha nini?

Didnt God use the lowly to perform great and mighty works?

Kati ya Babu Mvh. Mstaafu "aliebatizwa kwa maji mafupi" na yule Mwanamke Kahaba wa kwenye Biblia Mungu aliemtumia, ni nani mwenye uhalali wa kutumiwa na Mungu kwa context yako?

:embarassed2:

Au ulitaka afunuliwe Mwingira, Kakobe na wana-maji marefu ndio uamini?

Weka hoja nyingine lakini sio hizi maana Mungu hutumia wanaodharaulika kufanya mambo makubwa.......He is God and not MediaMan...and ofcourse thanks that he is not maana tungekoma
 

Hata angeenda Obama sishangai
 

Mungu anaweza kuwatumia wanaodharauliwa na watu sio wanaomdharau Mungu. Mungu ameagiza tubatizwe katika maji mengi wewe unajitungia ubaatizo wako, atakutumia wewe! Utatumiwa na "mungu" wa herufi ndogo. mungu wa dunia hii shetani anayemtumia babu sasa
 

Nenda kwanza shule ya uandishi wa habari ndio utaweza kuchambua post zangu na vichwa vyake.
 

Unasubiri Revelation ndio ujue kuwa shetani yupo. Pole sana
 
Mtoa mada ana kila dalili ya kuchanganyikiwa na kuijiona yeye ndiyo hasa anaejua ufunuo woote wa bibilia!!
Mchingaji anasema mungu kamwabia kupitia ndoto....mleta nada unatumia biblia kumwinua shetani!!!
Mwacheni mchingaji afanye kile alichoambiwa na Mungu. Nanyie anzisheni tiba itayotoka kwa Mungu kama hamuwezi kaeni kimya!!
Mshindwe na mwende motoni!
 

Wewe kwenye post hii umeandika Ndiyo Siyo Ndiyo Siyo - ongea pointi !
 

Afadhali umetambua kuwa babu kaambiwa na mungu kupitia ndoto. mungu anayeandikwa kwa herufi ndogo ni shetani. Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…