Babu wa Loliondo ashitakiwe ICC

hahah mikoa ya kaskazini ndo wana ushuhuda mzuri ndugu zao walokufa na kama sio huyo babu bado wangekuwepo namshukuru Mungu amewafungua wamepunguza kama sio kuacha kabisa kwenda
 
Kwa watu ambao walikuwa wanatumia dawa za kurefusha maisha na hatimae kuziacha kutumia kwa madai kuwa Kikombe cha babu kimewatibu kuna uwezekano wa virusi wa ukimwi kuwa sugu na kuzalisha kizazi kingine ambacho hakitafaa kwa ARV hivyo kuwa na maambukizi ya virusi vipya hapa nchini.............Tutakao umia ni wewe na mimi.....kwa nini tufumbie macho jambo hili?......au ni mpango mahususi wa kuzalisha kizazi kipya cha virusi? ni kweli watu hawaitwi lakini ukimwi nao hauchagui
 
Nikweli hajashika mtu mkono lakini kuwahimiza watu wakapate kikombe ndiko kuwashika mkono huko! na mna uhakika gani kwamba walio tangaza kuwa wamepona hawako mpango mmoja na huyo Babu ili mwisho wa siku waje wagawane mapato? maana nasikia kunamtu kateuliwa kuyatunza haijatoka hata senti inasubiriwa siku ya mgao na huku mazingaombwe yanaendelea hivyo siyo vizuri kusema hajaitwa mtu fikiria kama huyo mtu aliye fia kwenye foleni ni mtu anaye kuhusu utajisikiaje?
 
hapo kwenye red ni hatari!
mtu akijinyonga ni kosa ua si kosa? watu wanaoacha madaktari na kwenda kwa babu ni sawa na kujinyonga. Wanapaswa kulindwa au kushitakiwa kwa kutaka kujiua.
Na je,watu wanaoacha madaktari wa hospitali hii na kwenda nyingine ni kosa si kosa?jibu utakalo lipata liwe jibu la hapo juu!!
 
hapo kwenye red ni hatari!
mtu akijinyonga ni kosa ua si kosa? watu wanaoacha madaktari na kwenda kwa babu ni sawa na kujinyonga. Wanapaswa kulindwa au kushitakiwa kwa kutaka kujiua.

Kujinyonga si kosa, kosa ni kujaribu kujinyonga
 
1. Ila nadhani serikali ya TZ inatakiwa kuchukulia hatua. Kama watu wanakufa hospitali, ao njiani wakienda hospitali, angalao idadi ya wanao pona inaonekana kua juu.
Kwa kesi ya Babu Kwanza ni kama hakuna daktari alie jitokeza kuhakikisha kua asilimia kubwa ya wagonjwa walipona, na wachache tu ndio waripotiwe katika vifo.
Pili, ingawa Babu mwenyewe anasema wagonjwa wasiache dawa za hosii, anasema anaponya. kusema tu hivo ni sawa na kuwaambia watu waache dawa, na hiyo inawapelekea kufa.
Tatu, kweli serikali imejaribu kuweka order pale, ila mazingira bado hayaswihi kwa kuwahudumia wagonjwa.
Kwa sababu zote hizo mimi ningeshahuri Babu apigwe suspension, 4 dawa yake ifanyiwe uchunguzi kujua kama inadhuru.. .
1.Kwani kuna takwimu za kuonyesha kuwa wanaokufa kwa babu ni zaidi ya wanaopona?. Wanaokufa njiani si jukumu la babu kama vile lisivyokuwa jukumu la hospitali
pili Wrong quotation, babu amesema (hasa wale wa ukimwi) wasiache dawa zao hadi watakapodhibitisha kuwa wamepona.
Tatu Babu kupigwa suspension kwa kuwa mzingira hayajawekwa sawa haina tofauti na kusema kwa kuwa kuna msongamano mkubwa wa magari dsm, basi yasiruhusiwe magari kwenda tena dsm na mkurugenzi/ meya wa jiji apewe suspension!
4. Dawa imeshafanyiwa uchunguzi na kuonekana kuwa haina madhara. Hivyo kama kuna mtu anasema amekunywa kikombe cha babu na akafa au kuugua, huyi kafa kwa sababu nyingine si dawa. Suala la kudhibitisha kama inaponya au la linaweza kupimwa tu kwa kupima wagonjwa waliokwenda kwa imani wakanywa kikombe; kisayansi hutaweza kupona neno la Mungu liliwekwa kwenye huo mti!.
Nilisikia eti kuna watu 200 walijitokeza wakafanyiwe majaribio ya kikombe cha babu; hakika hao hawatapona maana wanakwenda kumjaribu Mungu na Mungu hajaribiwi!
 
Back
Top Bottom