TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,562
Hali ya yote natanguliza samahani kwa leo kugeuka 'mwanaume wa Darisalama',ni kwa leo tu jamani, siku nyingine sitakuwa 'mwanaume wa Darisalama'(natania tu jamani).Tuje kwenye mada sasa,kilichonisukuma kutaka kudadisi juu ya Diamond ni kufuatia kauli ya Babu Tale kwamba pamoja na kutaka kumsaidia Chid Benz...pia aliwahi kumsaidia Diamond kipindi cha nyuma japo ilikuwa siri sana,
Je alimsaidia Diamond kuhusiana na nini hasa?Maana matatizo ya Chid Benz kila mtu anayajua.Msiniulize zaidi kwamba nahisi Babu Tale alimsaidia Diamond kivipi maana mimi mwenyewe sijui.Nimelazimika kuileta hii mada tujadiliane kwa heshima na adabu baada ya mimi leo kusikiliza mahojiano kati ya Babu Tale na Sam Misago katika kipindi cha E-NEWS.
Ciaooooooo!
============

Hii hapa habari yenyewe mleta mada hebu isome kwa umakini na uielewe.
Akiongea kwenye kipindi cha eNews kinachorushwa na East Africa Television, Babu Tale ameweka wazi kuwa Diamond Platnums ambaye anamsimamia, alishawahi kumsaidia Chidi Benzi kuacha madawa, kwa kwenda kumtoa damu na kumuwekea damu safi, lakini jambo hilo lilikuwa la siri ndio maana aliweza kurudia.
"Diamond alimshamtoa Chidi damu, kutoa ile yenye madawa, lakini alirudia unajua Chid anaacha na kurudia, sasa labda ndio maana ilikuwa rahisi kwa yeye kurudi kwa sababu ilikuwa siri, Damond siku hiyo alishinda hospitali kutwa nzima, akimtoa Chidi damu", alisema babu tale.
Kwa sasa Chid Benzi amepelekwa Rehab bagamoyo baada ya kurudia matumizi ya madawa ya kulevya, na kumuathiri kwa kiasi kikubwa, na ameahidi kuacha matumizi ya madawa hayo.