"Babu" na mseto wa kauli zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Babu" na mseto wa kauli zake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohammed Shossi, Mar 30, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wote tumeshuhudia media inavyotupasha habari kila uchao kuhusu yanayojiri kule kijiji cha Semunge wilaya ya Loliondo. Babu amekuwa kwenye kurasa za mbele za magazeti yetu kila uchao na kutufanya kusahau mambo muhimu ya nchi. Hii ni faraja kwa baadhi ya watu kwani kwa kiasi fulani wamepumua na ni hasara kwa wale wengine kwani sasa hivi hakuna asikiae malalamiko yao watu wako bize na "babu".


  Babu kazungumziwa sana na yeye kuzungumza nimeanzisha thread hii ili kila alichosema babu tuki quote then tu read between the lines.

   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kuna kauli fulani kali, ngoja niipekue niiongezee hapo
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kazi ipo!

  source:https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/119766-hoja-ya-shossi-juu-ya-sh-500-ya-babu-17.html

  eti tiba ya Mungu isiporatibiwa na viongozi wa serikali haitakuwa endelevu!! tafakari huyu ni Mungu gani?

  source:Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu
   
 4. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,993
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  simshabikii sana babu lakini kama source ya hizi quotes ni magazeti, then sina uhakika na credibility ya hizi quotes. for obvious reasons...

  kama kuna video clips, zinaweza kusaidia zaidi....ziweke hapa ili tuzijadili.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Thomaso!!
   
 6. N

  Nhunda Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  {QUOTE=Miss Judith;1797201]kazi ipo!

  source:https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/119766-hoja-ya-shossi-juu-ya-sh-500-ya-babu-17.html

  eti tiba ya Mungu isiporatibiwa na viongozi wa serikali haitakuwa endelevu!! tafakari huyu ni Mungu gani?

  source:Waziri Simba aonja joto ya jiwe kwa Babu}

  Kumbuka kuwa ya kaisali mpeni kaisali na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu, Lakini pia haiishii hapo tu tunahimizwa kuzitii mamlaka zote zilizopo duniani kwani mamlaka hizo zimewekwa na Mungu. Kwa mantiki hiyo sioni kama babu alikosea chochote.
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ni kauli zilizonukuliwa kwenye mahojiano kadha wa kadha na kusikiwa na watu wengi kupitia Television!
   
 8. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  suppose kwamba serikali imeamua kuipinga hii huduma, ina maana haitakuwa endelevu na mwishowe itakufa?

  tangu uzaliwe hadi leo umeshaona huduma gani iliyoanzishwa na inayoungwa mkono na Mungu wa kweli imekufa kwa sababu ya kukosa uratibu wa serikali? kama unajua historia ya kanisa, nitajie ni lini huduma gani ya Mungu wa kweli ilikufa kwa sababu ilipingwa na serikali?

  bado unapaswa kujiuliza tena kwa autulivu mkubwa: ni mungu gani huyu ambaye huduma yake isiporatibiwa na viongozi wa serikali haitakuwa endelevu na hatimaye itakufa?

  ee Bwana umenichunguza na kunijua,

  wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu


  umezifahamu njia zangu zote
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Babuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

  Naona "babu" karibu ataanza kufufua wafu teh teh teh teh................
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135

  hahah, babu bado tu anaendelea kuota?

  siku ile itakuja kama mwivi
   
 12. p

  papaamahuli Member

  #12
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana JF. Mimi ninafanya kazi hapa Halmashauri ya Wilaya Ngoro2, makao makuu yake ni Loliondo. Kutoka hapa kwenda Sami=unge ni km 56Km hivi

  Mi naomba tu niwaondoe dukuduku maana nyie mpo mbali na hapa.

  Ni hivi, Hapa tulipo tulio wengi hatujaenda kwa babu kwa maana ya ule usemi "Nabii hakubaliki kwao". sisi tunaendelea kuwashangaa tu wapitaji wanaotokea kanda ya ziwa kwenda kwa babu maana njia ni hapa kwetu.

  cha ajabu zaidi ni kwamba watu tunaendelea kugawanyika kila uchao maana kila siku tunasikia na kuona baadhi ya mabo mapya maana kila mtu anasema la kwake.
  wengine wana mashaka na namna alivyoanza; kwamba, Wakuu wa makanisa hasa yale wanayojiita "makanisa ya kiroho" huko mijini kwenu DSM, Mwanza nk karibu wote wanatoka Mbeya (kasoro Rwakatare nk) wengine wote wanatokea Mbeya. watu wanahoji, je MBEYA tu ndiko Mungu anakoona kuwa kunafaa sana watu wa maajabu watokee?(ukizingatia babu naye ni mtu wa mbeya)

  Je Mungu haoni mahala pengine??

  Pili, babu haishi na familia yake hapo samunge, kaiacha Babati miaka mingi, mh, hii nayo ni sawa??

  Tatu, babu ni mch.mstaafu, uliwahi kuona wapi manabii wa Mungu wote walioandikwwa kwenye Biblia wamefanya maajabu lakini kwa malipo? (hata kama ni kidogo?) walipewa bura lakini wakatoa bure pia, babu yeye analipisha kidogo 500/= ni sawa kibiblia? au ndo mambo mapya ya Mungu?

  Nne, Babu anasema asipo kupa yeye dawa huponi, mbona kwenye biblia hata Yesu, nabii Elisha nk wenyewe walisema tu neno na mtu akapona hukohuko alipo?? hii ya babu ni mpya??

  Tano, kama ni Mungu kweli, mbona ameruhusu na wengine wajitangaze kuwa wanatoa dawa kama ya babu?? Si angeacha tu babu aendelee kugawa dose??
  Tutawatambuaje???????

  Sita, saba nk, ngoja niishie hapo nisije nikawaondolea imani wana JF ambao walikuwa na mpango wa kuja!

  kwa ujumla hili suala bado lina utata sana, niwaombe tu kwamba msome Mathayo 7, Luka 21, na Mathayo 24 mtaona namna Yesu mwenye alivyotahadharisha watu wake juu ya mabo haya hasa ukizingati hizi ni "siku za mwisho"

  Nitaendelea kutoa ufafanuzi kadri mtakavyohitaji.
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Babu ndoto yake ni ndefu sanaaaaaa kama sinema ya kihindi kwahiyo kila aakikumbuka scene anasimulia tehe teh teh.............kuna sehemu walimnukuu alisema kiama bado siku 59 nikajiuliza kama kiama bado siku 59 wale watu wanaotaabika porini wanaenda kufanya nini wasiosubiri mwisho wa dunia na kujiweka busy kuupata uzima wa milele kuliko kuupata uzima wa miezi miwili.
   
 14. P

  Paul S.S Verified User

  #14
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Eti hata kikombe hicho kililetwa na Mungu wake, yeye hajui kilipotoka
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa, haya yote uliyoweka hapa leo tulishayyajadili hapa kwa siku kadhaa sasa na baadhi yetu tumekaribia kung'olewa macho na mashabiki wa babu. lakini hatuachi na tunaendelea kuyajadili hapa hadi ukweli ujulikane na kila mtu.

  karibu sana katika mjadala unaoendelea na tunafarijika kupata mtu anayemjua babu na mazingira yake na hata familia yake

  angalau leo tumejua kuwa babu katelekeza familia yake na kujichimbia kijijini samunge huku familia yake ikiteseka kwa kukosa mapenzi ya baba yao na labda hata mahitaji ya kimaisha na babu huyu hajali. kweli huyo mungu wake kiboko

  basi kwa kuwa tumezungukwa na wingu kuwa la mashahidi namna hii,
  na tuweke kando mzigo wa dhambi ile ituzingayo kwa upesi
   
Loading...