Babu Loliondo kufilisiwa??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu Loliondo kufilisiwa???

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ngoshwe, Dec 19, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  babu.jpg

  [​IMG]
  Mojawapo ya magari anayomiliki babu Ambilikile Masapile.

  MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi' (pichani), anaendelea kusakamwa na wagonjwa wanaodai hawakuponyeshwa na dawa yake, wapo walioweka nia ya kumburuza mahakamani lakini mpya ni pendekezo la kumfilisi.


  babu2.jpg

  ..nyumba yake mpya.
  Wanaharakati wameeleza kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo wanamfungulia Babu Ambi, mojawapo ni kumfilisi mali zote alizochuma endapo atakutwa na hatia ya ulaghai, wakati wa kutangaza maono aliyopewa na Mungu kuhusu tiba ya kikombe.Wanadai kuwa Babu Ambi, mkazi wa Kijiji cha Samunge, Loliondo, alitumia matatizo ya Watanzania ya kuugua maradhi sugu ili kujinufaisha, hivyo akatengeneza ulaghai wa tiba ya kikombe kwa maelezo kwamba ni ufunuo aliopewa na Mungu.Madai hayo yanakuja wakati ambao Babu Ambi ameukata, ameshakamilisha ujenzi wa nyumba yake ya kisasa kijijini Samunge, pia anamiliki magari mawili ya bei mbaya, Toyota Land Cruiser (pick-up) na Isuzu (pick-up).Babu Ambi, ameshahama nyumba chakavu aliyokuwa anaishi zamani na sasa anaendesha maisha yake kwenye mpya ya kisasa ambayo kwa Samunge, inaonekana ni kama Ikulu kwa jinsi inavyomeremeta.
  [​IMG]...sola anayotumia nyumbani kwake.
  Wakati Babu alizoea kukanyaga vumbi kwenye nyumba yake ya awali ya udongo, yenye chumba kimoja cha kulala, hivi sasa anatembea juu ya sakafu iliyotandikwa vigae (tiles) kila eneo.Nyumba ya Babu, pia ina kila kitu ambacho hustahili kuwemo kwenye nyumba ya kisasa yenye hadhi ya mtu mwenye fedha, vile vile ina umeme wa mionzi ya jua na maji ya uhakika.Mali zote hizo, wanaharakati wanataka zifilisiwe kwa sababu zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.Muungano wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (Tanopha) ni wanaharakati wa kwanza kutoa tamko la kumburuza mahakamani.Tanopha wanasema, miongoni mwao, walitumia kikombe cha Babu Ambi lakini hakuna hata mmoja aliyepona.Wanasema, kila walipokwenda kupima ili waone matokeo ya tiba ya kikombe, majibu yalikuwa ni yaleyale kwamba hakuna mabadiliko.

  [​IMG]
  .babu akiwa amepozi nyumbani kwake.
  "Hatuwezi kupoteza muda na fedha zetu kwa kwenda kunywa dawa ambayo haitibu, hii ni kuwarubuni wananchi, wengi wameuza mali zao, wengine kutumia akiba ya fedha walizokuwanazo kwenda Loliondo wakijua wangepona lakini cha kushangaza ni kwamba baadhi yetu wanakufa."Wengine wako mahututi baada ya kupewa kikombe, tulikuwa na matumaini ya kupona hadi tuliacha kutumia vidonge vya kurefusha maisha vya ARV, hatuna mengi zaidi ila tunaomba umtafute mwenyekiti wetu akueleza zaidi," alisema mmoja wa wanachama wa Tanopha.Mwenyekiti wa Tanopha, Julius Kaaya, aliliambia Uwazi kwa njia ya simu kuwa taasisi yake ilipeleka watu 14 kunywa dawa Loliondo lakini hakuna hata mmoja aliyepona."Nakumbuka kwamba kipindi tunaenda huko Loliondo Machi 19, mwaka huu, tulifanya mkutano na waandishi wa habari, tulifika Samunge Machi 22, ambapo Machi 24 walikunywa dawa hiyo kila mmoja akiwa na matumaini ya kupona."Baada ya siku 20 tangu wanywe dawa hiyo walienda hospitali kuangalia kama wamepona, daktari aliwaambia hakuna hata mmoja aliyepona, siku 90 baadaye majibu yakawa yaleyale," alisema Kaaya.MCHUNGAJI MTIKILANaye Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation, Christopher Mtikila kwa upande wake amesema kwamba dawa hiyo haitibu na analishughulikia suala hilo ili kumfikisha mahakamani pamoja na mawaziri, wabunge na viongozi wa juu waliokunywa kikombe.
  [​IMG]...mjengo wake mpya.
  "Mawaziri hao wamewahamasisha wananchi kwenda Loliondo kunywa dawa, lazima tuwashitaki pamoja na viongozi wa dini waliopiga debe," alisema Mtikila. Viongozi wa dini waliohamasisha ni Askofu Thomas Laizer na Martine Shayo.Baadhi ya Mawaziri waliopata kikombe ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli. Wengine ni wabunge Augustino Mrema, Edward Lowassa na wakuu wa mikoa Yohana Balele na Abbas Kandoro.TAMKO LA WIZARAWaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda, alisema hivi karibuni kuwa kikombe cha Babu siyo tiba na kwamba wote waliokwenda Loliondo, walipoteza muda.Kauli ya waziri, ilifuatia ripoti ya uchunguzi wa madaktari bingwa kwamba kikombe cha Babu wa Loliondo, hakitibu.WABUNGE NAOKatika Mkutano wa Tano wa Bunge la 10, baadhi ya wabunge walitaka Babu wa Loliondo achukuliwe hatua kwa sababu dawa yake haitibu.Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka mawaziri waliokwenda Loliondo, wahojiwe na waseme kama wamepona, kwani wao kwa kiwango kikubwa walihusika kupotosha umma.
  [​IMG]...babu Ambi akiwa amepozi, pembeni ni bafu la kisasa analotumia kwa sasa.
  UTETEZI WA BABUKwa upande wa Babu Ambi, ameendelea kushikilia msimamo wake kuwa dawa yake imeponyesha wengi."Kama hawajapona siyo makosa yetu. Tuliwaambia kabla kuwa katika tiba hii kigezo cha kwanza ni kuwa na imani na hapa tuna uthibitisho wa kutosha wa watu walioponywa na maajabu ya dawa hii wakiwemo wagonjwa wenye Ukimwi," alisema Babu Ambi na kuongeza kuwa anapigwa vita na wengi kwa sababu ya wivu.Kuhusu utajiri wake, alisema kuwa yeye hana mamilioni ya fedha kama inavyodaiwa ila akakiri kumiliki nyumba ya kisasa pamoja na magari mawili ambayo amesema yanamsaidia kubeba dawa pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Loliondo.KUHUSU KIKOMBEKwa mujibu wa Askofu Mkuu wa KKKT Arusha, Thomas Laizer, zaidi ya watu milioni tatu wameshatibiwa Loliondo.Kila mgonjwa alikuwa analipa shilingi 500, hivyo kwa hesabu ya watu milioni tatu, maana yake kikombe kimeshaingiza zaidi ya shilingi bilioni 1.5.
  HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO
   
 2. Loading.....

  Loading..... Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajinga ndio waliwao
   
 3. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Naona babu sasa ana vimisuli kama anapiga chuma mpaka kawa kijana pesa bwana kweli ni sabuni ya roho.
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Babu ametokea uzeeni!. Kweli wajinga ndio waliwao.
   
 5. M

  MaMkubwa1 Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  True!! Hakulazimisha mtu .... Je wale waliomshikia 'bango' je?
   
 6. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  maisha magumu,, inabidi tuwe wabunifu,, babu kabuni lake katoka sasa hivi mambo yake mchekea,,, mlioenda hesabuni imekula kwenu,,,,, kaaazi kweli kweli.....

  Tatizo watu wengi maisha yao wanayaendesha kwa matukio...
   
 7. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwani mlilazimishwa kwenda ,si mlijipendekeza Hongera babu,zindua deal lingine., uwafolenishe.....
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ,matatizo ya watu ndio neema ya watu...
   
 9. bayonamperembi

  bayonamperembi JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Kama alivyosema Babu ni kwamba imani ndiyo inaponyesha. Walioamini walipona na wale wasioamini hawakupona. Watu wengi sana wa mtaani kwangu wamepona akiwamo bibi yangu na wengine japo hawakupona kabisa ila wana nafuu kubwa tofauti na hapo awali. Ingekuwa busara kama kila mtu aliyetumia au anaemfaham alietumia kikombe angetoa ushuhuda hapa ili wale wanaofuata mkumbo wa kuipinga wajiridhishe. Kuhusu kufa, Ikumbukwe kuwa hicho kikombe siyo cha kukufanya uishi milele, siku yako ikifika LAZIMA uondoke.
   
 10. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mimi mama yangu alikuwa na sukari kwa miaka 30. ametumia kikombe cha babu na sasa hivi ni historia. sasa kama hao ambao hawakupona, si waendelee na maisha yao? Hawana kazi za kufanya which are more productive na zenye TIJA???

  Mimi nawashauri kuwa kama wanataka kumfungulia babu mashtaka, basi kwenye hati waongeze na DistrictConucil ilikyokuwa inachukua Tshs 5,000-10,000 kwa kila gari na 70,000 kwa kila helicopter inapotua. wajipange kufillisi na council pia. wasisahau na village government ambao walinufaika sana na kuwepo kwa babu pale Kijijini!!!

  Kwani walilazimishwa kwenda kwa babu? Mbona watz wengi sana hawakwenda? waganga wa kienyeji wangapi wametapeli watu na hawajafunguliwa mashtaka? Kwani babu was the only option to them?

  Nchi imejaa maovu na uvundo kila kona, si wangeifungulia serikali mashtaka kwa kuwaletea dawa fake za UKIMWI, kupandisha gharama za maisha, kupanda bei za mafuta na umeme kila siku na mengine.

  Watu walioshiwa kimawazo wana matatizo sana. Mabere Marandu SIASA zimemshinda sasa anajikita kwa babu!

  Kwa taaarifa yenu, tutaaanzisha mchango wa kumtetea Babu and we will hire the best advocates, SHAME ON YOU
   
 11. T

  Taita500 New Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Babu Ambi iwe fundisho kwetu,2cpende kuamin miujiza saaana mana hta shetani anaweza fanya miujiza
   
 12. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Kweli nimeamini utapeli cyo lazima usomee!! .....akifilisiwa mi nachotaka ni 500/= yangu tu.
   
 13. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Wapi Miss Judith
   
 14. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Out of 500, Babu got only 200 Tshs!
  The rest, I am not sure of the breakdown, went to KKT
   
 15. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hakuna cha babu kupelekwa popote coz hajamlazimisha yeyote kwenda huko ispokua ni kuogopa kufa kwenu! Looh! "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" komaa.
   
 16. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Kumbe babu naye ameshakuwa Cerebrity!
   
 17. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Kekundu kekundu!!!!!!!!!!!!
  Oooh wajinga ndio waliwao, wajinga ndio waliwaooo
  Mwacheni babu wa watu ale good time. Hakuna alieshikwa miguu kwenda.
  Imani zenu haba zimewaponza.
   
 18. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Lazima sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke!!! Babu katapeli, hivyo hana budi kurudisha pesa ya watu kwa staili ile ile aliyochukulia pesa hizo! Babu hakutoka Samunge, bali wananchi ndio walienda huko...hivyo ni lazima wale wote waliotapeliwa na babu wafunge safari hadi Samunge wakachukue jero jero zao....VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hebu wasituletee bange zao hapa!

  Kuna mkataba walisainishwa na babu kuwa ni LAZIMA wapone...............hii ni DECI nyingine mmeingia kichwa kichwa mmenyolewa asa mnalia lia nini na maujinga yenu?
   
Loading...