Babu Kikombe alikuwa turufu ya Kisiasa?

Jamani - Miafrika Ndivyo Tulivyo.. tunaishi kwa rehema za Mungu sasa iwe dawa ya babu inaponyesha au haiponyeshi, siku zote tumeepuka madhara mengi kwa reham za Mungu tu..Madawa yenyewe hospitalini mengi ni fake na watu wanazidi kununua kama wanaokwenda Loliondo. Na wala huyu Babu sii wa kwanza maanake asilimia 50 ya watanzania wanaenda kwa waganga wa Kienyeji hata kama wanakwenda Hospitali. Kwa hiyo, siasa tumeziunda wenyewe kutokana na Ile chuki pevu ya kisiasa inayoambatana na UDINI..

Haikuwa turufu ya Kisiasa kama wengi wanavyofikiria isipokuwa ukweli ni kwamba Viongozi wengi serikalini ni WAGONJWA wa MAGONJWA SUGU..Kifupi Babu anaweza kutumiwa kktk kukusanya takwimu za maradhi mbalimbali na pia hesabu ya waathirika wa magonjwa hayo maanake ni mila ya Mtanzania kuficha Ugonjwa ndio maana kuna msemo usemao - Ukificha Ugonjwa...!

Kikombe cha Babu kisingekuwa na mashaka kama asingetumia jina la Yesu au Mungu na kuoteshwa. Anechukuliwa kama waganga wengine tu isipokuwa naye kwa kutazama soko na ubunifu wa tiba alijua Watz wanaishi kwa kudra za Mungu, kulihusisha jina la Mungu na tiba yako ni ushindi mtupu. Na pili wanasiasa pia wakaona sehemu ya kujipatia umaarufu na sifa vile vile..
 
Babu Kikombe alikuwa turufu ya Kisiasa?

Miezi minne iliyopita Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Masapila aliiomba Serikali imsaidie kupata gari la kubeba dawa, vyombo vya kunywea, kuni na vyombo vikubwa vya kuchemshia dawa hiyo ili kukabili wingi wa Wagonjwa waliokuwa wakijitokeza kupata Tiba katika kijiji cha Samunge huko Loliondo.

Maoni ya wagonjwa waliopata Tiba kila mmoja alijibu kwa staili ya aina yake, wengine walisema "Sijui kama nimepona kabisa au la, lakini sasa najisikia vizuri tofauti na mwanzo,"

Baadhi ya watu wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU), ambao wamepewa dawa hiyo, licha ya kudai kuwa sasa wana hali nzuri, bado hawajapima kuthibitisha uponyaji huu wa ajabu.



Utashangaa ndani ya kipindi hiki kifupi cha ndani ya miezi minne kutoka maombi hayo ya Babu hadi tamko la Waziri Mkuu, Kasi ya kwenda Loliondo bado ipo lakini si kwa kiwango cha juu kama kipindi hicho,kwa sasa barabara ni nyeupe na ukifika muda huo huo unapata tiba na kuondoka.

Ni kweli wagonjwa wamekwisha? wamepungua kwa kiasi hicho? au hali ngumu ya ukata kuweza kugharamia safari hadi Loliondo? Maswali yote haya majibu yanabaki kuwa katika mioyo wa watanzania.

Kiini cha hoja yangu ni ukimya uliopo kwa baadhi ya taarifa za kufedhehesha kuhusu mamia ya watanzania waliopoteza maisha licha ya kugonga kikombe kwa matumaini makubwa kabisa kuwa afya zao zingetengemaa kama awali.

Naandika haya nikiwa na uthibitisho wa zaidi ya vifo kumi huku simulizi kutoka kwingineko zikinukuu vifo vingi zaidi, kibaya ni mlipuko wa vichaa wengi kutokana na kukatiza ARV’s, ushahidi wa kitabibu unaonyesha mgonjwa anayekatiza ARV’s ghafla ana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa hilitafu ya akili.

Wengi wamekimbizwa mahospitalini kwa hofu kwa malaria zimepanda kichani kumbe tayari walikwishakatiza dozi kwa matumaini ya kupata ahueni kupitia kikombe cha miujiza.

Hivi kwa nini serikali iliingia kichwakichwa katika hili, na kwa nini wanahabari hawaandiki madhara haya ya kikombe zaidi ya Ushabiki, hii ni ajenda ya nani hasa na nini mwisho wake kwa matokeo haya ya kudhoofisha kabisa katika jamii ya watanzania.

Sasa hoja iliyopo mezani wenyewe mnaijijua babu kasahaulika kabisa. Mchezo huu mchafu hadi lini??



Adios




muulize baba batilda biriani
 
Back
Top Bottom