Babu Kikombe alikuwa turufu ya Kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu Kikombe alikuwa turufu ya Kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jul 11, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Babu Kikombe alikuwa turufu ya Kisiasa?

  Miezi minne iliyopita Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Masapila aliiomba Serikali imsaidie kupata gari la kubeba dawa, vyombo vya kunywea, kuni na vyombo vikubwa vya kuchemshia dawa hiyo ili kukabili wingi wa Wagonjwa waliokuwa wakijitokeza kupata Tiba katika kijiji cha Samunge huko Loliondo.

  Maoni ya wagonjwa waliopata Tiba kila mmoja alijibu kwa staili ya aina yake, wengine walisema "Sijui kama nimepona kabisa au la, lakini sasa najisikia vizuri tofauti na mwanzo,"

  Baadhi ya watu wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU), ambao wamepewa dawa hiyo, licha ya kudai kuwa sasa wana hali nzuri, bado hawajapima kuthibitisha uponyaji huu wa ajabu.  Utashangaa ndani ya kipindi hiki kifupi cha ndani ya miezi minne kutoka maombi hayo ya Babu hadi tamko la Waziri Mkuu, Kasi ya kwenda Loliondo bado ipo lakini si kwa kiwango cha juu kama kipindi hicho,kwa sasa barabara ni nyeupe na ukifika muda huo huo unapata tiba na kuondoka.

  Ni kweli wagonjwa wamekwisha? wamepungua kwa kiasi hicho? au hali ngumu ya ukata kuweza kugharamia safari hadi Loliondo? Maswali yote haya majibu yanabaki kuwa katika mioyo wa watanzania.

  Kiini cha hoja yangu ni ukimya uliopo kwa baadhi ya taarifa za kufedhehesha kuhusu mamia ya watanzania waliopoteza maisha licha ya kugonga kikombe kwa matumaini makubwa kabisa kuwa afya zao zingetengemaa kama awali.

  Naandika haya nikiwa na uthibitisho wa zaidi ya vifo kumi huku simulizi kutoka kwingineko zikinukuu vifo vingi zaidi, kibaya ni mlipuko wa vichaa wengi kutokana na kukatiza ARV's, ushahidi wa kitabibu unaonyesha mgonjwa anayekatiza ARV's ghafla ana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa hilitafu ya akili.

  Wengi wamekimbizwa mahospitalini kwa hofu kwa malaria zimepanda kichani kumbe tayari walikwishakatiza dozi kwa matumaini ya kupata ahueni kupitia kikombe cha miujiza.

  Hivi kwa nini serikali iliingia kichwakichwa katika hili, na kwa nini wanahabari hawaandiki madhara haya ya kikombe zaidi ya Ushabiki, hii ni ajenda ya nani hasa na nini mwisho wake kwa matokeo haya ya kudhoofisha kabisa katika jamii ya watanzania.

  Sasa hoja iliyopo mezani wenyewe mnaijijua babu kasahaulika kabisa. Mchezo huu mchafu hadi lini??  Adios   
 2. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Ww unataka aendelee na huduma wakat Magamba wote wameshakunywa dawa
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwa mimi kikombe cha babu kwenye HIV naona kimeprove failure kabisa labda kwenye magonjwa mengine lakini siwalaumu wale waliotumia najua mtu ukiumwa kila ukimabiwa hii ni dawa ni lazima utajaribu kabisa. Mwisho mimi naamini babu wa Loliondo sidhani kama kweli ile message ni kutoka kwa Mungu maana maneno ya Mungu huwa hayadondoki chini!
   
 4. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nilipatwa fadhaha sana Mkuu wikiendi hii nikimshuhudia mama mmoja akihangaika na kubweka mithili ya Mbwa, ndugu zake wakidhani Malaria imepanda kichwani na kuwashurutisha wahudumu wa afya wamsaidie kafungwa kamba ni balaa kumbe ARV's zikikatizwa ghafla hayo ni moja ananithibitishia daktari mtaalamu wa magonjwa ya ukosefu wa Kinga na akiniambia kesi hizi ni nyingi mpaka inahuzunisha.

  Sijui huko mlipo kama haya hamjayasikia.

  Nilimsikia wiki kadhaa Baba Askofu R'uaichi wa Jimbo katoliki akiwataka wagonjwa waliopata kikombe wakapime, ni baada ya kuripotiwa wingi wa matukio hayo katika Hospitali ya Bugando huko Mwanza ambapo yeye ni Askofu wa Jimbo kuu Katoliki ilipo hospitali hiyo. Ila kama alipotezewa hivi kwa habari hiyo.
   
 5. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Suala si kunywa mkuu ni uponyaji. wagonjwa wa sukari wamerudi kati sindano za Insulin huku wengine wakipoteza maisha akiwemo mzee mashuhuri jijini Arusha, wakazi wa huko wanamjua vema sipendi kulizungumzia hilo kwa sababu za kifamilia.
   
 6. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #6
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mna shida gani na bau nyie?
  Kwasasa babu anapokea wageni wa toka nchi za jirani na za ng'ambo.
  Kaeni mnamdiscuss huku misururu inazidi kurefuka!
   
 7. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Upo off the point Mkuu soma vema thread utazame tunalojadili hapa ni lipi.
   
 8. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Tulisema toka mwanzo kuwa kila aliyekuwa anashabikia ushirikina atakuja kukiri mwenyewe, sasa naona mnaanza kurudi kwenye ubinadamu sasa. Mzee Ambikile alikuwa na matatizo ya kisaikolojia kwa kutumikia kanisa kipindi chote akidhani ni njia sahihi kwake kujipatia mahela sasa alipoona kisha jiuzulu lakini hata nauli ya kurudi kwao Mbeya hana akaamua kubuni uganga na akabahatika kupata mainterijensia.

  Wakamtumia ili kuhamisha mawazo ya watanzania kutoka kwenye habari za uchaguzi na kuanza kuhangaika kwenda Loliondo, kitu kilichozaa vifo vingi sana na familia nyingi zikajikuta zinaomboleza. Babu aliwachota hata wasomi wajinga, na mbaya zaidi hata kanisa likaweka biblia pembeni na kuanza kushabikia.
   
 9. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapo wanaosema wamepona hasa wa kisukari kuwa kime-stabilize lakini wapo waliopoteza maisha. utafiti ufanywe jamani ili tupate kitu kinachoeleweka. Wakati huo huo tunaambiwa dawa ya babu iko mbioni kupatiwa hati miliki!! confusion tupu. jamani wataalamu njooni mbele fanyeni utafiti na mtujuze au sivyo tutaishia kwenye "madhanio" au hypotheses
   
 10. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani haya mwaswali yote hayawezi kupata jibu hapa.
  Serikali ilisaidia kurahisisha huduma hiyo ya Babu baada ya watu kukataa kuacha kwenda huko. Kumbukeni serikali iliomba watu wasiendi kwa muda ili wajaribu kurahisisha mazingira ya Samunge ila wagonjwa na familia zao walikataa abadan katani.

  Mimi binafsi siamini kama dawa hiyo ilikua na nguvu yoyote ila imani ya mtu inaponya. Kuna dawa zinaitwa "placebo", hazina effect yoyote mwilini ila ukinywa kwa kufikiri ni dawa na unapona kweli. Ilitokea hivo hivo.

  Kwa wale walio amini 100% dawa inatoka kwa Mungu na wakaendelea kumuomba, MAYBE kuna baadhi yao Mungu alijibu na kuwaponya kweli ila kwa asilimia kubwa sana ya watu walipona kwa muda tu (kimawazo) na baada ya shangwe kushuka wakajikuta katika hali ile ile ya mwanzo.

  Swali lako ni kwa nini hawamsimamishi babu kutoa huduma hiyo? sababu hakuna anacho haribu yeye kama yeye. Halazimishi kuacha dawa, kuacha kupima wala kuamini anaponya. ni watu wenyewe wanaenda kwa hiyari na wanaamua kuacha dawa. Kosa lake nini?

  Na kama mchangiaji alivosema ukiwa umekata tamaa alafu unaambiwa kuna mtu anaponya lazima utaenda. kama ukipona unashukuru na kama hujapona at least ulijaribu. na ukinyimwa haki ya kujaribu basi unaona walio kunyima haki hiyo ni maadui.
   
 11. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hii thread ikimptata miss judith upande mmoja ...............na paka jimmy upande wa pili ndo itanoga.................
   
 12. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umeona Mkuu sina shaka watapita maana hii ni hatari zaidi ya maelezo ya kawaida. Kibaya sasa hata Bunge eti linasikitika Wakenya kutangaza kuwa Samunge ipo mashariki mwa Nairobi na kwamba ni rahisi na kwa nafuu zaidi kutoka nje ya Nchi kwenda kupata Tiba Samunge. Tunatambua waarabu na baadhi ya mataifa ya Ulaya kama uchina na India wanavyoshabikia Tiba asili kwa hiyo haitashangaza kuona misururu kutoka nje inaendelea kuja Samunge.

  Sikushangaa kuona ambavyo Media makini za Nje ambavyo zilipuuza ushabiki huu licha ya baadhi ya wadau kuona kama ni moja ya agenda zao kupuuza ugunduzi kutoka Afrika na mambo mema zaidi ya kushabikia mambo mabaya Pekee.

  Nani sasa anakubali kuamasisha kufanyika kwa uchunguzi huu ikiwa wale wachochezi (MEDIA) waliowafikisha watanzania hapa wnaogopa kula matapishi yao.

  Gazeti la Mwananchi soma Ishue zote za April na May hakuna ishu ambayo haina habari za Babu kikombe, alipewa teaser kwenye kila cover ishu. Kulikoni ukomya huuu??
   
 13. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Asilimia kubwa wamerejea katika sindano upya. Nashukuru kipindi kimoja kilirushwa na Channel 10 na tokea hapo hakijarudiwa tena alionyesha kijana mmoja pale Mwanza Airport ambaye alitibiwa na pamoja na tiba hiyo hakupona Ukimwi. Hiki kipindi nashangaa hakirudiwirudiwi kama vile wanavyorudia baadhi ya mambo yasiyokuwa na Tija. Huu ni mzaha kwa Taifa.
   
 14. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #14
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  GR ulikuwa wapi wewe? au Bi Kiroboto alikupiga BAN ya kutoingia Bungeni?
  Wapi Habari za Bunge ?
  Mis Man
   
 15. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #15
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bi Kiroboto Nuksi, majukumu Mkuu, wembe ni ule ule hapa nilipo nimeshajipanga kuunasa mjadala wa Jioni nasikia kuna vyombo vya moto huko.
  Am back man

  Ngoja nikupige na lithanks la maandishi kabisa kwa kutambua mchango wa GR kutoka mjengoni
   
 16. m

  maoniyangu Member

  #16
  Jul 11, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi hii nchi ya vikombe imeshanichosha
   
 17. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha COUNTRY OF CUPS, For God sake wale wliojipenyeza kwa maslahi binafsi nje ya Babu (A Targeted Focal Point) walikufa kifo cha mende. Ila huyu kingunge mwenye Ajenda anazidi kupenyeza licha ya kutokuwa na mashiko kama hapo awali.

  Wakigundua mlango wa pili hoja na agenda iliyoko mezani imeanza kusinzia utasikia kikombe anakumbukwa tena, ati juzi from nowhere anatafutiwa hati miliki khaa watanzania hawa!!!!!!!!
   
 18. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bado tutayasikia mengi:
  Makala ya Raia mwema ya leo inatoa picha kwa kina ni kwa kiasi gani huyu mzee hakuwa Muujiza wa Mungu wala nini, bali turufu ya Siasa ya Serikali dhalimu

  Pata Nakala uisome kwa kina: waliokunywa kwa matumaini ya kupona Ukimwi, wapima baada ya siku tisini, mwendo ule ule
   
 19. M

  Mwalukasa New Member

  #19
  Aug 5, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />Mr kama huna point ya kuchangia kaa kimya,na kama hujui maandiko ya bible dont speak anything,Tiba ya ya Loliondo ni tiba sahihi ki biblia,na watu waliokwenda kule wakiwa na imani wengi walipona,kama we huamini pole,lkn watu wanaendelea kumiminika huko.
   
 20. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama ulikwenda kwa Babu pole, subiri zamu yako.Wajinga ndio waliwao.Tulisema ushenzi anaoufanya mpuuzi yule, una mkono wa shetani mkakaza shingo,mtavuna mlichopanda.
   
Loading...