Hahaha...hiyo inaitwa kuuziwa kanyaboya na kuna wanaume unakuta wanalea si mtoto mmoja tu bali watoto lukuki ambao hawana hata chembe ya damu ya baba...
Unadanganywa kirahisi tu kuwa leo tufanye ndio siku ya hatari kumbe wapi kuna mkware alishapewa jana yake mwanamama anaokoa tu jahazi...
hospitali zetu ni chanzo pia cha tatizo hili..
Mtoto wa madame b kapewa lara 1 na wa lara 1 kapewa lady doctor.. Yule wa lady doctor kapewa heaven on earth..
Kwa hii cycle unategemea nini?
Simplicity., haya mambo nimeyasikia sana tu, wala si kidogo kwa namna mbili tofauti. Kwa zamani, wadada walikuwa wakiwafanyia hivi waume zao pale ambapo walikuwa wakipata manyanyaso toka kwa wifi, ndugu za mume au mume mwenyewe kuwa kwanini tangu aolewe hajazaa! Kwa mantiki hiyo, baadhi yao walikuwa wanatoka nje ya ndoa kimya kimya, na kwenda kujaribu nje kisha kuleta mimba za nje ndani kuondoa adha ya kusemwa na kunyanyaswa. Na enzi hizo technolojia ilikuwa si kubwa, hivyo kugundua mtoto si wako haikuwa rahisi, labda kwa muunekano awe tofauti kabisa.
Kwa nyakati hizi, nafikiri kukuwa kwa utandawazi, kumomonyoka kwa maadili, kuingia kwa tamaduni za nje, watu kutokumuogopa Mungu, kutokuheshimu ndoa, migogoro ya ndani ya ndoa, nk kumesababisha baadhi ya wanandoa kutokuwa waaminifu na kuwa na mahusiano na watu wengine. Mahusiano yanapozidi, uangalifu hupungua na matokeo yake ndiyo hiyo unakuta mke/mume wa mtu kazaa nje ya ndoa yake au mume anabambikwa mtoto.
Sasa tukirudi kwenye mada yako na hasa swali lako "Jamani hili swala la akina mama kuplagiarise watoto na wapambe wao kujaribu kuwanusuru kwa kuwapa watoto fake brands mbona linakua kwa kasi sana siku hizi?" Ni kuwa binafsi naona sababu ya kubambikwa mtoto, kama si kosa la mke kuwa mzinzi na kujikuta kabeba mimba ya mwanaume mwingine, basi mume mwenye mke anaweza kuwa chanzo. Maana matatizo ya uzazi yapo, na yanaweza kuwa kwa mke au mume. Wengi wa wanaume hukiria tatizo ni mwanamke na kuanza kumlaumu na kumnyanyasa mkewe kwa kutokushika mimba badala ya kukaa chini na kuhangaika kwa pamoja kujua kiini cha tatizo.
Wanaume twapasa kubadilika tunapokuwa na changamoto za kupata watoto ndani ya ndoa kwa kushirikiana na wenzetu ili kuepuka matatizo kama haya.
BTW, huyo mume wa huyo dada alifahamu kuwa huyo mtoto si wake?
Jamaa anaweza kuwa alishtukia, au labda aliwachukulia wale wanawake kiutani.
Najaribu kufikiria kipuuzi kama mimi ndo baba wa huyo mtoto halafu majirani wanakuja na kuanza kusema kimafumbo kwamba mtoto si wangu, sijui moyo utaniuma kiasi gani! Duuu, Mungu atupishilie mbali na changamoto za namna hii!
duh!
mi kama sijalewa hiv!
nani anieleweshe!
Tumefika mahali ambapo wanaume tuondoe mawazo kuwa watoto wote ni wa damu yako! Heri sasa hivi kuna vipimo, zamani hali ilikuwa mbaya kwa kulainishwa na maneno matamu 'amefanana na babu wa bibi yake na mdogo wa binamu yake'
.
Tuwalee Tuwatunze ni raia wa Mungu
^^
Hospitali zetu ni chanzo pia cha tatizo hili..
mtoto wa Madame B kapewa lara 1 na wa lara 1 kapewa Lady doctor.. yule wa Lady doctor kapewa Heaven on Earth..
kwa hii cycle unategemea nini?
lazima asilimia iwe kubwa kwa sababu wote wanaoenda kupima toka mwazo mazingira ya kupatikana mtoto yalikuwa na walakini, lakini yawezekana kama kila mtoto akipima tatizo lisiwe kubwa kiasi hicho. kwa utashi wangu mdogo naona nikazi sana kumsingizia mtu mtoto yataka uwe na moyo wa ajabu. pia wababa watafute elimu ya uzazi kuna mazingira ukiibiwa ukahesabu vizuri unaweza ukajua.Hahaha tatizo huwa halitatuliwi kwa kulikwepa au kulikimbia, bali kulikabili...
Kuna wakati ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilitoa takwimu kuwa 48% ya wanaume wanaopima DNA hupata majibu kuwa watoto sio wao
Sosi: J2WISDOM: Mkemia Mkuu: Asilimia 48 siyo wa baba halali,Wanaume wabambikizwa watoto!!!
Hata kama si wako??
Ndugu Simplicity, neno 'plagiarism' linatumika kwenye wizi wa kazi za sanaa tu, sio kwenye masuala mengine kama haya ya 'kupakaziana' watoto. Ni mtazamo tu, unaweza kuangalia maana yake kwenye dictionary yoyote.