Mke wangu tunaishi nae nyumbani lakini bado sijafunga naye ndoa.
Nimekaaa nae yapata miaka 6 sasa. Niko naishi pia na baba yangu nyumba moja.
Mke wangu analalamika kwanini baba yangu anamuita wewe badala ya jina lake.
Je, ni sahihi baba yangu kumwita mkewangu "Wewe"?
Naombeni mawazo yenu niweze kutatua hili jambo[emoji1488][emoji1488]
Si sahihi kama imekuwa ni utaratibu wake.
Kuna suala la utamaduni hapa lakini--msikurupuke na huyo mwenzako. Ukumbuke wengi wetu Kiswahili ni lugha ya pili, na lugha si kuumba sentensi pekee bali inahusisha utamaduni na miiko yake. Yani mzungumzaji afahamu anazungumza nini, na nani, wakati gani, mahali gani, na kivipi kulingana na kanuni za lugha husika.
Je, unadhani huyo mzee anafanya makusudi, ama ni kutofahamu Kiswahili na tamaduni zake? Ukute mpaka umrudishe na kumtafsiria kwenye lugha yake ya asili ndipo atajua anavyokosea. Ni sawa na mtu anapojifunza lugha ngeni, kuna wakati anaudhi na kutukana lakini hajijui. Umeona wazungu au Wahindi, kwa mfano, kabla hawajawa mahiri kwenye Kiswahili? Utasikia Wewe fulani, kuja hapa, Kwenda kule n.k. Sasa Kwa Mswahili thabiti, katika mazingira ya kawaida, haya ni makosa. Lakini, mzungumzaji hajui, anatiririka tu.
Kazi kwako kujua kama baba anafanya makusudi ama udhaifu wa lugha. Ikibidi apewe shule