Logic ya mtoto ni kuwa, huyo ndo anamlipia ada na chakula na all her basi needs ndiyo maana inamuwia ngumu kumsemea.
Wakati niko polisi hizi issue zilikuwa sana, yani binti kapewa mimba na mjomba au hata baba yake mzazi/kambo ila yupo tayari kwa lolote ila asimtaje maana anajua akienda ndani na yeye future yake inayumba (mara nyingi wanakuwa walishawatishia hivyo, ikiwamo na kuwatishia kuwaua). Kwa mtoto maneno na vitisho hivyo viko deep kuliko tunavyotaka kuamini sisi wenyewe (I mean kama mtu mzima ni rahisi kupuuza na kuona anapenda mwenyewe nk).
Nadhani serikali iko bize kuwafunga wakosaji na sio kuwahudumia wahanga wa haya mambo ndiyo maana hayaishi. Wizara husika iwezeshwe kifedha na iandae mfumo mzuri wa kuhakikisha mabinti hawa wanapata maisha baada ya abusers wao kufungwa.
My 5 cent.