Baba wa mbinguni nakushukuru!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Hatuna budi kumshukuru Aliye Juu kwa uumbaji wake wa kushangaza ambao majira haya ya kiangazi yanaufunua kwa namna ya ajabu na ya kutisha. Tumshukuru kwa kutupa macho ya kuweza kushuhudia uumbaji huo na mioyo ya kufurahia kazi yake isiyo na mfano. Hivyo popote pale ulipo tumia sala au dua hii kumshukuru Mungu.

"Ee Mola uliye mwingi wa fadhili na rehema
Mkuu usiye na mfano wala usiye na mshirika
Unayetoa yale yote yaliyo mema
Na kuwajaza watu wako baraka
Ninakushukuru kwa uumbaji wako
Kwa viumbe viendavyo kwa maringo na mapozi
Viumbe ambavyo pasipo hivyo ulimwengu huu hakika ungekuwa sana na Jehanum!
Tunashukuru kwani katika uumbaji wako
Tunaona ukuu wa upendo wako kwetu.
Tunaomba uwabariki viumbe vyako hawa
Si kwa baraka zile za Kichina
Bali kwa baraka za Kijamaika na Brazili!
Na zile za kwetu za Kimakonde!
Na utuwezeshe sisi tunaofurahia uumbaji huo
Kuzidi kukaa macho bila kupepesa
Ili tusipitwe na lolote na tukalikosa!
Na tunawaonea huruma wale wanaoishi kwenye nchi ambazo uumbaji wako
Si rahisi kuonekana namna hiyo!
Ila tunaomba sana tena chonde chonde.. hata tukiingia majaribuni usitutoe mapema
Ila kwahakika usituache tuzame huko na kujisahau
Ila kama ulivyomfanyia Yona/Yunus yule nabii nasi hatimaye uturudishe kwenye nchi kavu!"

Na watu wote wasema AMEN, aMINA, AMEEN!
 
I don't undestand what you wanted to communicate here, but sounds trivial!

I didn't know that God wants us to thank him just for the profound and the sublime but not the mundane and the trivial.. My Bible says somewhere "shukrani kwa kila jambo, furaha yenu ijulikane na watu wote". I'm just obeying the word.
 
Hatuna budi kumshukuru Aliye Juu kwa uumbaji wake wa kushangaza ambao majira haya ya kiangazi yanaufunua kwa namna ya ajabu na ya kutisha. Tumshukuru kwa kutupa macho ya kuweza kushuhudia uumbaji huo na mioyo ya kufurahia kazi yake isiyo na mfano. Hivyo popote pale ulipo tumia sala au dua hii kumshukuru Mungu.

"Ee Mola uliye mwingi wa fadhili na rehema
Mkuu usiye na mfano wala usiye na mshirika
Unayetoa yale yote yaliyo mema
Na kuwajaza watu wako baraka
Ninakushukuru kwa uumbaji wako
Kwa viumbe viendavyo kwa maringo na mapozi
Viumbe ambavyo pasipo hivyo ulimwengu huu hakika ungekuwa sana na Jehanum!
Tunashukuru kwani katika uumbaji wako
Tunaona ukuu wa upendo wako kwetu.
Tunaomba uwabariki viumbe vyako hawa
Si kwa baraka zile za Kichina
Bali kwa baraka za Kijamaika na Brazili!
Na zile za kwetu za Kimakonde!
Na utuwezeshe sisi tunaofurahia uumbaji huo
Kuzidi kukaa macho bila kupepesa
Ili tusipitwe na lolote na tukalikosa!
Na tunawaonea huruma wale wanaoishi kwenye nchi ambazo uumbaji wako
Si rahisi kuonekana namna hiyo!
Ila tunaomba sana tena chonde chonde.. hata tukiingia majaribuni usitutoe mapema
Ila kwahakika usituache tuzame huko na kujisahau
Ila kama ulivyomfanyia Yona/Yunus yule nabii nasi hatimaye uturudishe kwenye nchi kavu!"

Na watu wote wasema AMEN, aMINA, AMEEN!

Mkuu there is something 'good' happening in ur life right now. I can feel the glowing in ur face..he he he he..
 
Thanks mwanakijiji..ni vyema siku zote kumshukuru mungu kwa matendo makuu anayoendelea kutufanyia siku hadi siku.
 
Thanks a lot mwanakijiji umetukumbusha kushukuru sisi tulio wachoyo wa shukrani
 
Watu wote tumesema
Aaaaaaaaaaaaaaamiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiina
ATUKUZWE YEYE ALIYE KILA KITU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom