Baba wa kambo adaiwa kuua mtoto

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Kagera. Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Gwanseri wilayani Muleba kuuawa na baba yake wa kambo kisha kumfukia ndani ya nyumba akiwa amemuweka kwenye mfuko wa plasitiki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Olomi amesema tukio la mwanafunzi huyo kuuawa lilitokea jana katika kijiji cha Karutanga wilayani Buleba na kumtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Remijius Poncian(16).

Kamanda Olomi amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni baba wa kambo, Hassan Misigaro (52) anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

pic+baba+kambo.jpg

Chanzo: Mwananchi
 
Mimi sheria inaponichosha huwa ni pale mtu anapoua, na preliminary observations zote zinaonesha muuaji ni huyo baba wa kambo, pamoja na ushahidi wote wa kimazingira unakuta mwisho wa mwishoni, sheria unamuacha huru, anaenda zake..!
 
Angetajwa mama hapa thread ingekua page ya tano.
R.I.P kijana.
 
Mimi sheria inaponichosha huwa ni pale mtu anapoua, na preliminary observations zote zinaonesha muuaji ni huyo baba wa kambo, pamoja na ushahidi wote wa kimazingira unakuta mwisho wa mwishoni, sheria unamuacha huru, anaenda zake..!
"...proved beyond reasonable doubts..." Siyo kazi nyepesi. Ushahidi wa kimazingira hautoshi kumshinda mtu.

Sheria za jinai dunia nzima, zinawapa watuhumiwa wa uhalifu haki zaidi ya watendewa wa uhalifu.
 
Ni kweli unachosema, lakini wapo ambao wamekuwa wakitumia sheria kama mwavuli wa kujikinga na tuhuma, na mwisho wa siku wasio na hatia ndio waliohukumiwa.

Katika kozi ngumu ambayo sio ya kisayansi vyuoni, SHERIA huwa ipo miongoni. Na huu ugumu inatokana na kujifunza kubadili uongo kuwa ukweli. Kumtetea uongo hadi uwe ukweli sio jambo dogo.
 
"...proved beyond reasonable doubts..." Siyo kazi nyepesi. Ushahidi wa kimazingira hautoshi kumshinda mtu.

Sheria za jinai dunia nzima, zinawapa watuhumiwa wa uhalifu haki zaidi ya watendewa wa uhalifu.
images
Onus Probandi
 
Ndg tuache masihara najua jamaa kachua maamuzi magumu na ya kipumbafu
Ila twende kwenye ukwel

Hivi kwel unalea mtt mapaka anafika form2

Alafu unagundua mzazi mwenzake anaendelea kumega kama kawaida
Kiukwel inauma
Mungu atutie wanaume ujasiri katika hili
 
Back
Top Bottom