Baba .. Unapoamua kukagua simu za mabinti zako!!!

Baba .. Unapoamua kukagua simu za mabinti zako!!!

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
450
.....Siku hizi Matumizi ya simu yamekuwa ni ya uwazi na ya kurahisisha maswala mbalimbali kimaisha na si vibaya kununua simu kwa ajili ya watoto nyumbani kwa mawasiliano ya haraka..... ni kawaida... baadhi ya watu wamefanya simu kuwa kama rafiki wa karibu na kuifanya kuwa sehemu ya kuweka mambo mengi ya kimaisha pamoja na kumbukumbu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maswala ya siri... Nimemshuhudia Baba mmoja siku moja anarudi nyumbani saa 3 za usiku kisha kuwaambia mabinti zake watau wenye umri kati ya miaka 15 na 22 waje mbele yake na kisha kuwaamuru kila mmoja apeleke simu yake kwa ukaguzi wa ghafla... huu ni uungwana kweli.....!!!!
 
Niwatoto wake na mamuzi ni yake, kila familia ina malezi yake...Kama baya kwawengine yeye anaona sawa..
 
Ana lengo zuri la kuhakikisha watoto wake hawatumii uhuru wa simu vibaya hata mimi walikuwa wanachunguza simu nilipokuwa 18's ikanibidi majina ya kiume nisave kwa majina ya kike iki wasistukie.
 
sasa wewe inakuhusu nini na we si uwe na wakwako uwape uhuru unaotaka,chezea mafataki wewe.
 
Mabinti ukiwachunga haimaanishi ndio unawampa malezi bora ila ni muhimu vilevile kuwe na mipaka.Ikumbukwe lazima atatafuta upenyo tu wakufanya yale anayoyataka ni jambo la muhimu sana kuwaamini watoto haswa kuanzia miaka 18 ni watu wazima hivyo anavyowalea ni kikoloni..Ndio wanaadamu tulivyo tunapowekewa vizuizi tunatafuta tactic za kuovercome hizo circumstances...Hata mimi nilikuwa nikichungwa sana lakini i always had my ways lol :smile-big::smile-big::smile-big:kwahio kitendo cha huyo baba kukagua simu ni useless kusema kweli kwa mtazamo wangu mimi!!
 
mi mama angu alikuaga anakagua sim enzi ziko advance nikija

nashangaa message zote zimefutwa...halfu hanisemeshi kitu

ilekukaa kimya ndo ilikuwa inanikosesha amani kabisaaaa...
 
Ni jambo jema na la kuigwa. Mambo ya papuchi na mitarimbo wakajadiliane nje ya nyumbani. Na awe anawazaba makofi watakaokutwa wametongozwa halafu wakakubali
 
.....Siku hizi Matumizi ya simu yamekuwa ni ya uwazi na ya kurahisisha maswala mbalimbali kimaisha na si vibaya kununua simu kwa ajili ya watoto nyumbani kwa mawasiliano ya haraka..... ni kawaida... baadhi ya watu wamefanya simu kuwa kama rafiki wa karibu na kuifanya kuwa sehemu ya kuweka mambo mengi ya kimaisha pamoja na kumbukumbu mbalimbali ikiwa ni pamoja na maswala ya siri... Nimemshuhudia Baba mmoja siku moja anarudi nyumbani saa 3 za usiku kisha kuwaambia mabinti zake watau wenye umri kati ya miaka 15 na 22 waje mbele yake na kisha kuwaamuru kila mmoja apeleke simu yake kwa ukaguzi wa ghafla... huu ni uungwana kweli.....!!!!

Ni uungwa japo huwa wanazifuta hizo sms
 
Ana lengo zuri la kuhakikisha watoto wake hawatumii uhuru wa simu vibaya hata mimi walikuwa wanachunguza simu nilipokuwa 18's ikanibidi majina ya kiume nisave kwa majina ya kike iki wasistukie.

Ndo kama hivi inakuwa haisaidii
 
mabinti hao watamzidi akili ni bora kuwaeleza ukweli kuliko kuwafanya wawe na nidhamu ya woga baada ya ukaguzi si anarudisha kwa wenyewe usiku badala ya kusoma wanachati
 
Kila familia ina njia yake ya kuwalea watoto wao na jinsi ya kuwarekebisha pindi wanapokwenda nje ya maadili
 
Back
Top Bottom