Baba Rostam!

Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,522
643
Siku ya Ijumaa tarehe 7/10/2011 mke wangu alijifungua mtoto wa kiume na tulikubaliana kuwa yeye ndo amchagulie jina mtoto. Sasa leo usiku narudi home toka kwenye mishemishe zangu, mke wangu ananiambia kampa mtoto jina la ROSTAM.

Nikadhani ananitania kumbe she's serious na yeye anajua vilivyo msimamo wangu dhidi ya mafisadi lakini yeye kasisitiza kuwa hajachagua jina hilo ili kunichokoza bali analipenda tu jina hilo licha ya kuwa mtu maarufu mwenye jina kama hilo hapa TZ anahusishwa na tuhuma za rushwa.

Kwa kuwa tulikubaliana awali kuwa yeye ndo atampa jina mtoto sina jinsi imebidi nikubali kuwa BABA ROSTAM kuanzia leo! Je ingekuwa wewe ungeamuaje?
 
BongoLogik

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
260
44
duu! msala, ila kwa kuwa ulishakubali yeye achague jina hiyo ni ahadi na ukiivunja utakuwa huna msimamo lakini hilo ni jina tu kuhusu tabia ataiga kuanzia kwenu wazazi,kwa majirani au kwenye jamii kwa ujumla ila msingi wa tabia jitahidi mjenge nyie wazazi! pole sana BABA 'FISADI'
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,951
287,542
Pole sana kuna majina mengine ni noma sana kuwapa watoto hasa kama majina hayo yanaweza kutumiwa katika kuwatenga au kuwanyanyasa watoto wenye majina hayo. Kama umelikubali basi hakuna ubaya. Hongera sana kwa kupata mtoto.
 
Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,522
643
duu! msala, ila kwa kuwa ulishakubali yeye achague jina hiyo ni ahadi na ukiivunja utakuwa huna msimamo lakini hilo ni jina tu kuhusu tabia ataiga kuanzia kwenu wazazi,kwa majirani au kwenye jamii kwa ujumla ila msingi wa tabia jitahidi mjenge nyie wazazi! pole sana BABA 'FISADI'
we acha , nitazoea tu, kuna watu wanaitwa Baba Osama, Baba Yuda (msaliti wa Yesu) sembuse mimi!
 
Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,522
643
Pole sana kuna majina mengine ni noma sana kuwapa watoto hasa kama majina hayo yanaweza kutumiwa katika kuwatenga au kuwanyanyasa watoto wenye majina hayo. Kama umelikubali basi hakuna ubaya. Hongera sana kwa kupata mtoto.
shukran kwa hongera itabidi dogo nimlee awe na maadili mema sana tofauti kabisa na mtuhumiwa
 
Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,435
Mtoto wako unaweza ukamwita Pope lakini ukamlea kwenye mazingira ya kishetani akawa jambazi/mwizi ,sizani kama hil jina la Rostam litamfanya naye awe fisadi
 
uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,718
1,378
Nyie Wamakonde nini hahaha! ? maana wenyewe jina lolote linalovuma kwenye vyombo vya habari wakati huo ndio hilohilo Bush twende,Saddam twende, koffi Annan twendeOchama twende yaani vurugu tupu.
 
joramjason

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
425
131
Please you nid to think twice kabla mambo hayajahrbika mbeleni. Hivi mnataka watoto wenu waje kuwalaani sababu ya majina mliowapa wakati wadogo? Hilo jina linaweza kuja mcost huko mbeleni hasa katika mambo ya ajira. Anaweza fikiriwa fisadi ingw ni mtu mwema 2. Hy ni mwz yangu lkn.
 
Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,522
643
Nyie Wamakonde nini hahaha! ? maana wenyewe jina lolote linalovuma kwenye vyombo vya habari wakati huo ndio hilohilo Bush twende,Saddam twende, koffi Annan twendeOchama twende yaani vurugu tupu.
mimi si mmakonde na wala si kabila moja na mke wangu ambae naye si mmakonde
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,951
287,542
Please you nid to think twice kabla mambo hayajahrbika mbeleni. Hivi mnataka watoto wenu waje kuwalaani sababu ya majina mliowapa wakati wadogo? Hilo jina linaweza kuja mcost huko mbeleni hasa katika mambo ya ajira. Anaweza fikiriwa fisadi ingw ni mtu mwema 2. Hy ni mwz yangu lkn.

Kwa maoni yangu ni vizuri mkubaliane jina mnalotaka kumpa mtoto kabla ya kulitoa jina hilo, bahati nzuri mwenzetu kalikubali jina hilo la Rostam. Mie ningelipiga chini mara moja, lakini binadamu tunatofautiana katika kufanya maamuzi.
 
Chuma Chakavu

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,522
643
Please you nid to think twice kabla mambo hayajahrbika mbeleni. Hivi mnataka watoto wenu waje kuwalaani sababu ya majina mliowapa wakati wadogo? Hilo jina linaweza kuja mcost huko mbeleni hasa katika mambo ya ajira. Anaweza fikiriwa fisadi ingw ni mtu mwema 2. Hy ni mwz yangu lkn.[/QUOTE
Ok, hilo laweza tokea iwapo unaaminii huko mbeleni watakuwa wanaajiri kwa kuzingatia majina badala ya qualifications!]
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom