Baba Mkwe ananidai Mahari

Yani kumbe una nusu na unapata shida?

Mpigie simu mwambie nakutumia nusu kuna mambo mengine yamenibana inadidi nimalizane nayo.

Na akikuuliza unamazilia lini mwambie nitakujulisha usimpe ahadi kama ulivyofanya.

Mtu unapompa ahadi na yeye anapanga mambo yake.

Mwisho mahali haimalizwi hata kama anasumbua.
 
Naombeni Ushauri wenu maana wakati mwingi nakua na mawazo.
Mpigie simu mwambie baba mkwe ile million tayari ipo ila imebaki 500,000 tu. Mwanao ameikopa laki 5 nyengine kwahio utamdai mwanao.

Hapo mpange mkeo kuhusu hili ili ukipata laki 5 yake unamalizia miezi sita ijayo au unasemaje Chali wangu?.
 
Hiyo kete inasukumwa na mke wako kwa ustadi mkubwa ongea na mkeo muelewane yataisha mkuu
 
Nimeongea nae kaikubali ila sasa bado amenibana kwa kuniuliza nitamalizia lini kiasi kichobakia, kabla ya hapo alisita kuchukua kwakusema mbona kiasi ni kidogo ingekua Vizuri niongeze angalau ifike laki 7.
uyo mzee anapenda sana pesa we mwambie utampa kisha mwambie mtoto wake akaongee na babaake vizuri mahali inalipwa hata kwa miaka 10 wasikuchanganye hii ishu mkeo anahusika kuifosi.
 
Laki 5 unapata wengine wawili.
Ila lipa magari mkuu maana mlishakubaliana
 
Mbona mimi baba mkwe msukuma ananidai mahari kama songesha 😂next time akinipigia natia block
Msukuma njaa huyo. Utamaduni huwa ni huo huwa kuna wazee tangu mwanzo mnaelewa mahali yeye anakuwa ameshasema mahali isipungue kiasi hiki basi.

Hapo akisema hao wazee watakao muwakilisha hawawezi kushuka zaidi ya hapo hata mnaweza msielewane nao kabisa na wanarudi bila kuelewana.


Hata kwenye kuwapa mahali hutampa baba yake ni hao wazee na hata kudai watadai hao wazee.

Mimi mwenyewe ni MUHAINI nilibakiza laki2 hadi sijawahi daiwa na mzee walinidai mara1 wale wazee nikawaambia bado sijaipata wazee wangu. Japo hii mahali kama.hujamaliza ikitokea mkeo akafa wanaidai na kama hutawapa siku hiyo wanabeba maiti kwenda kuzika kwao!

Huyo mzee wako either ndo hawa wazee wa .com
 
uyo mzee anapenda sana pesa we mwambie utampa kisha mwambie mtoto wake akaongee na babaake vizuri mahali inalipwa hata kwa miaka 10 wasikuchanganye hii ishu mkeo anahusika kuifosi.
Kweli mkuu hapo kwenye mke kufosi itakua kweli maana kila siku ananiambia Umeongea na Baba, Umempigia Simu Baba. Nilitegemea yeye awe kimya kwasababu mimi na Baba yake tulikubalia na kuelewana sasa nashangaa yeye ndiyo anakua na kihere here cha kunisumbua nimpigie Baba yake nimlipe mahali yote.
 
Mkuu nimeshajichanganya nimempa ahadi tayari ndani ya miezi 3
 
Mkuu wengi hatuzoea mambo ya kusumbuliwa symbolically maana tuna jazba tunaweza kutoa majibu taka muuzi Baba mkwe
 
Lipa hiyo mahari uishi kwa amani! Ingawa mahari huwa haidaiwi kihivyo mpaka mtu uteseke. Sisi baba alidaiwa na babu mpaka wakasahau! Tusidharau mila za watu!
Kwahiyo Mzee wako hakumaliza yote ?
 
Lipa hiyo mahari uishi kwa amani! Ingawa mahari huwa haidaiwi kihivyo mpaka mtu uteseke. Sisi baba alidaiwa na babu mpaka wakasahau! Tusidharau mila za watu!
Tatizo wazazi wetu hawafati Mila zao na wakati huo wataka wafate Mila kwenye kudai mahali ila kwenye kulipa Mahali kwa Vijana wao wanajifanya hawajui Mila, Mfano Mimi Mila la Kabila letu mahali ya kuolea inatakiwa itoke Nyumbani,Nichukue Ng'ombe niende kulipa Mahali kama alivyofanya Mzee wangu.
 
Usiogope kumpigia,deni la mahari si sawa na madeni ya kawaida,mpigie na mwambie kuwa una nusu yake na nusu nyingi mpe tarehe nyingine
 
Kijana, yaani matatizo madogo haya ndo yanakufanya ukose raha, uwe na hasira hadi uje uombe ushauri hapa?

Hivi kweli utaweza kukabiliana na magumu yaliyoko mbele yako? Unaweza kukabiliana na hali ngumu ya maisha ikiwa itatokea na ukiwa na watoto? Nimesikitika sana
 
Nimeongea nae kaikubali ila sasa bado amenibana kwa kuniuliza nitamalizia lini kiasi kichobakia, kabla ya hapo alisita kuchukua kwakusema mbona kiasi ni kidogo ingekua Vizuri niongeze angalau ifike laki 7.
Hiyo hailipwagi, mi nilimtapeli tu bamkwe na nikarudi na mzigo wangu wa maana bongo na sikulipa tena,
mdingi kanitafuta hadi kanipata miaka nilimpa 150k wala hakubisha akatambaa zake.
Mpaka leo marafiki tu, mwenyewe anakiri we fala sana binti yangu mzuri vile umemchukua kilaini tu.
Ukamzalisha,
Uzuri binti ndo alitoa mbinu ya kumtapeli dingi yake😅.
 
Ndio umekuja kumsengenya Swahiba wangu na jana tukashindwa Kupombeka!
 
Ama kweli mahari siku hizi ina maana nyengine kabisa. Mtu ushaanza kuishi na mwanamke kwamiaka tele na pengine hata mshapata watoto halafu eti wazazi wanataka mahari, mahari ya nini? Mahari huko nyuma yalikuwa yakitumika kwa ajili ya sherehe za harusi lakini naona sasa wazee wanaiona kama ni mtaji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…