Lech Poznan
JF-Expert Member
- Jul 3, 2025
- 450
- 585
Hapa nilipo nimechanganyikiwa kabisa, Baba mkwe wangu ananidai Mahari Nimalizie Nusu iliyobakia shilingi Milioni moja na Mimi kwasasa Mambo Magumu na tulikubaliana Mwezi huu wa kumi na mbili sasa Mambo yangu bado siyo Mazuri na uwezo wa kumpa hiyo Milioni hakuna ila nina Nusu yake, Shida ni jinsi ya kumpigia simu na kumueleza inaonekana yeye anahitaji Milioni
Kwasasa anampigia simu mwanae na kumuulizia na Mke wangu kila siku ananiuliza umempigia simu Baba yani mpaka wakati mwingine nakua na hasira, Najiuliza Je, nimpigie simu nimwambie kiasi nilichonacho na Je, akigoma kuchukua nitafanyeje?
Naombeni Ushauri wenu maana wakati mwingi nakua na mawazo.