Baba Lowassa, Sumaye na babu Kingunge sheria ni msumeno

Baba Lowassa, Sumaye na babu Kingunge sheria ni msumeno

Tulimwamini Lowasa, Tuna imani na Lowasa. Na tutaendelea kuwa na imani na Lowasa. Tunaamini yeye sio dhaifu na hatatuangusha katika kuhakikisha haki inatendeka katika uchaguzi huu wa 2015. Kura za rais zihakikiwe na mshindi halali ndiye atawale nchi hii.
 
wamevuna walichopanda,kwenye madai yao ya katiba ni ukomo wa ubunge,tume huru,uraisi kuhojiwa mahakamani na mgombea binafsi,wao walivyoenda kwenye bunge la katiba wakabeba ajenda ya serikali tatu,ajenda ya msingi wakaweka pembeni
 
Maada imekaa poa sana, sheria ni msumeno, hawakujua kama siku watakuwa wapinzani. Walimuona warioba mjinga, leo wao ndio wamekuwa wajinga. Wafunge midomo yao, waache kihaha
 
Ushauri wa bure kwa wana Ukawa na Ccm uchaguzi wa 2020 jaribuni kufunga cctv camera sehemu zote zinazojumlishwa matokeo ili wale wanaosubilia matokeo nje ya sehemu hizo wapate kuangalia live kwenye runiha hapohapo hii itasaidia kuondoa utata wa kile kinachoendelea huko ndani

Hii inaweza kusaidia sana lakin wacwac wang pia ni hko barabaran hzo kura za majumuisho zikiwa zinapelekwa sehem husika
 
Sheria zetu za nchi haziruhusu kujadili matokeo ya urais mahakamani, so to say, huwezi kuyaquestion kokote isipokuwa kwa wananchi. Na ukishitaki kwa wananchi utasababisha uvunjifu wa amani, na hakuna mtanzania hata mmoja atakayekubali ujinga huo wa kuvunja Amani.

Twende mbele, turudi nyuma. Wakati sheria hizi zinatungwa, au zinafanyiwa marekebisho, Lowassa, Kingunge na Sumaye walikuwa CCM wakiyapinga mapendekezo ya wapinzani kutaka matokeo ya urais yajadiliwe mahakamani; wakaisimamia katiba mbovu iliyopinga uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Leo sheria zile walizozisimamiawakiwa CCM ndiyo zimewatafuna. Wameonja joto ya jiwe walilolirusha wenyewe. Hawana tena uwezo wa kushitaki kuhusu matokeo waliyoyapata, na sisi hatupo tayari kuandamana.

Hapa wanalazimika kukubali kukubaliana na wasiyokubaliananayo, maana wakati yanatengenezwa waliyatetea. "Walitega mtego mtego ambao umewanasa wenyewe".

Nampongeza sana Mbowe kwa kuwakaribisha hawa wanaCCM ndani CDM. Angalau wale waliobaki CCM watajifunza kutetea maslahi ya nchi badala ya kutetea maslahi ya chama na maslahi binafsi.

Huko sahihi kama wewe ni mwana UKAWA, tumecheka na ngedere tumevuna mabuwa, wale wale waliozikandamiza ndio zimewamaliza, Asante lowasa kwa kutuongezea nguvu, usichoke tuendelee kudai katiba mpya na tume huru, naomba leo akampe mkono tu akubali yaishe.
 
Huwa nawacheka sana Wasaliti wa CCM kina SUMAYE, KINGUNGE , MWAPACHU na wengi wao ambao waliamini CCM itashindwa na Lowassa atakuwa Rais wapewe vyeo! Hakika wameaibika sana! Sijui sura zao wataweka wapi? Wengine wanalipwa pensheni kibao kwa pesa za walipa kodi lakini bado walihadaiwa na LOWASSA kwamba atawapa vyeo.

AIBU SANA! WAMEUMBUKAAAA!
 
Aisee.........sasa tutawasaidiaje..........?.......
 
Hao wala sio wa kuwaongelea tena,kisiasa walishakata pumzi.
 
Uloi nga mâché68;14803108 said:
Huwa nawacheka sana Wasaliti wa CCM kina SUMAYE, KINGUNGE , MWAPACHU na wengi wao ambao waliamini CCM itashindwa na Lowassa atakuwa Rais wapewe vyeo! Hakika wameaibika sana! Sijui sura zao wataweka wapi? Wengine wanalipwa pensheni kibao kwa pesa za walipa kodi lakini bado walihadaiwa na LOWASSA kwamba atawapa Vyeo. AIBU SANA! WAMEUMBUKAAAA!
Wewe ni wa kupimwa akili, nenda ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kaulize kazi za vyama kisha nenda mahakamani kawaulize kuna jinai ipi mtu kuhama ccm? kenge wewe.

Katika hao wote uliowataja huwapati kwa lolote kimaisha wewe na ukoo wenu wote, hata mbwa tu wa Lowasa ana maisha mazuri kuliko wewe mbumbumbu na zuzu wa kwanza.
 
Aisee.........sasa tutawasaidiaje..........?.......
Hao ni wakutusaidia sisi tuliojichokea, hakuna hata mmoja kati yao tunaemfikia kimaisha, juzi tu Lowasa kawapa laki tano tano wale wachimbaji wadogo Apolo walionusurika kifo. hii thread ni ya mtu mwenye njaa ambaye maisha yamemshinda sasa ni chuki tu bila sababu, ati sisi ambao hatuitaki ccm jina letu ni wasaliti! haitokaa itoke tena milele kwa ccm kuipata kura yangu never over my dead body.
 
Kwa DR SLAA na Lipumba sawa. Sio LOWASSA, SUMAYE. KINGUNGE na makapi wengine wa CCM ambao waliwalaghai hata akina MATOLA wakawafuata kama nyumbu bila hata kuhoji kwamba matatizo yanayodaiwa kuletwa na CCM wao walichangia kwa sehemu yao. Wanaletaje mabadiliko nje ya CCM? Hapo ndipo uwezo mdogo wa kufikiri wa watu wa aina ya MATOLA uliishia kwa kudeki barabara! SHAME!
 
Aisee nimegundua kuwa bila ya kumtaja Lowassa walahi hampati posho yenu. Yaani leo tu hili ni kama bandiko lenu la kumi kumtaja taja Lowassa! Sumaye alikuwa anataka cheo gani?
 
Lowassa ni mroho wa madaraka aliyeamini ni yeye tu anafaa kuwa rais. Wengine 37 hawafai. Ndio kaumbuka hivyo!
 
Nampenda lowasa, napenda vyama upinzani hata wangeweka jiwe ningelichagua ila CCM bado Sana, kihalali hamjashinda!!!kura mlizoiba zitawatokea puani Insha'Allah
 
Back
Top Bottom