Baba Lowassa, Sumaye na babu Kingunge sheria ni msumeno

COARTEM

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
3,617
Reaction score
3,681
Sheria zetu za nchi haziruhusu kujadili matokeo ya urais mahakamani, so to say, huwezi kuyaquestion kokote isipokuwa kwa wananchi. Na ukishitaki kwa wananchi utasababisha uvunjifu wa amani, na hakuna mtanzania hata mmoja atakayekubali ujinga huo wa kuvunja Amani.

Twende mbele, turudi nyuma. Wakati sheria hizi zinatungwa, au zinafanyiwa marekebisho, Lowassa, Kingunge na Sumaye walikuwa CCM wakiyapinga mapendekezo ya wapinzani kutaka matokeo ya urais yajadiliwe mahakamani; wakaisimamia katiba mbovu iliyopinga uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Leo sheria zile walizozisimamiawakiwa CCM ndiyo zimewatafuna. Wameonja joto ya jiwe walilolirusha wenyewe. Hawana tena uwezo wa kushitaki kuhusu matokeo waliyoyapata, na sisi hatupo tayari kuandamana.

Hapa wanalazimika kukubali kukubaliana na wasiyokubaliananayo, maana wakati yanatengenezwa waliyatetea. "Walitega mtego mtego ambao umewanasa wenyewe".

Nampongeza sana Mbowe kwa kuwakaribisha hawa wanaCCM ndani CDM. Angalau wale waliobaki CCM watajifunza kutetea maslahi ya nchi badala ya kutetea maslahi ya chama na maslahi binafsi.
 
lakini si kosa kufanya msukumo wa kuona sheria hizo za hovyo zikifanyiwa marekebisho tuwe kama nchi nyingine zilizoendelea kidemokrasia.
 
Tatizo watu wanajisahau wakiwa madarakani.
 
Kufumbia macho uozo wa sheria kandamizi ni ulofa ulopitiliza.
Hii nchi ni ya watanzania wote na siyo kikundi cha watu wachache na familia na marafiki zao ambao wanaendele kugawana vyeo mpaka siku za mwisho.
 
Ushauri wa bure kwa wana Ukawa na Ccm uchaguzi wa 2020 jaribuni kufunga cctv camera sehemu zote zinazojumlishwa matokeo ili wale wanaosubilia matokeo nje ya sehemu hizo wapate kuangalia live kwenye runiha hapohapo hii itasaidia kuondoa utata wa kile kinachoendelea huko ndani
 
lakini si kosa kufanya msukumo wa kuona sheria hizo za hovyo zikifanyiwa marekebisho tuwe kama nchi nyingine zilizoendelea kidemokrasia.

Sasa tusimwage damu za watu kwa kisingizio cha kuraka kurebisha sheria na ni vyema hao akina kingunge lowassa na sumaye waandamane wao wake zao na watoto wao pia
 
Ushauri wa bure kwa wana Ukawa na Ccm uchaguzi wa 2020 jaribuni kufunga cctv camera sehemu zote zinazojumlishwa matokeo ili wale wanaosubilia matokeo nje ya sehemu hizo wapate kuangalia live kwenye runiha hapohapo hii itasaidia kuondoa utata wa kile kinachoendelea huko ndani

Kujenga makao makuu ya chama wameshindwa na ruzuku yote ile, iwe kuweka camera nchi nzima? Labda camera wapewe msaada, na wakipewa wale mchwa kina lema wataziacha bila kuuza?
 
Mleta Mada nakupongeza kwa kulileta hili, ni kweli kabisa, walishiriki kusimamia haya. Lambda kama walitumwa kufanya kazi Maalum ambayo wameifanikisha. Muda utasema.
 
Kwny Mijadala sio lazima upate vyote, kwny bunge la katiba iliondolewa serikal 3 lakin tume huru ya uchaguz na ruhusa ya kupinga matokeo ya urais mahakamani wao kwa ujinga wakasusia Katiba mpya sasa Magufuli halazimiki kwa lolote kwny katiba mpya na hata kuahirishwa kwa katiba mpya hapakuwa na time limit. Mtamkumbuka sana Jakaya Kikwete
 
Kufumbia macho uozo wa sheria kandamizi ni ulofa ulopitiliza.
Hii nchi ni ya watanzania wote na siyo kikundi cha watu wachache na familia na marafiki zao ambao wanaendele kugawana vyeo mpaka siku za mwisho.

Saa nyingine ujio wa aliyekuwa adui ni baraka kutoka kwa Mungu, pamoja na Mengi yaliyosemwa kuhusu Lowassa, ujio wake una impact kubwa kwenye upinzani:-

1. Ameondoa kigugumizi kilichokuwa ndani ya CCM kwamba kujiondoa ndani ya CCM ni dhambi. Baada ya yeye kuanza tuliona wengine wakifuata kama F.Sumaye.

2. Ujio wake umekisaidia Chadema kuongeza wigo wa majimbo ambayo yalikuwa kama yamemilikiwa na Wabunge fulani. Mfano Simanjiro, Monduli.

3. Kugombea kwake Urais kulisababisha taharuki ndani ya CCM na kuwafanya wasiamini kama watashinda uchaguzi lakini pia kuliongeza hamasa kwa wananchi ya kupiga kura. Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia nchi hii mgombea wa upinzani akipata kura nyingi na pia mgombea wa CCM akipata kura chache chini ya asilimia 60%.

Hayo aliyoyatoa mtoa mada ni kweli lakini kwa kuwa yamewakuta wao nadhani yatatoa elimu kwa wengine waliomo madarakani kuwa sheria ni msumeno unakata kotekote. Na sisi kama binadamu hatuwezi kujua kesho yetu itatukuta tukiwa wapi.
 
Umesema kweli kabisa, ni vema kuipenda nchi zaidi kuliko chama.
 
nadhani sasa bodaboda na watoto wa shule wametoka humu jf tumeanza kujadili mada muhimu
wazo zuri
 
Ushauri wa bure kwa wana Ukawa na Ccm uchaguzi wa 2020 jaribuni kufunga cctv camera sehemu zote zinazojumlishwa matokeo ili wale wanaosubilia matokeo nje ya sehemu hizo wapate kuangalia live kwenye runiha hapohapo hii itasaidia kuondoa utata wa kile kinachoendelea huko ndani
baada ya kuwashauri wapiganie tume huru ya uchaguzi wewe unawadanganya waingie mkenge tena na cctv. hivi ukiweka uzio kwako na CCTV unaweza kumzuia kibaka asikuibie kama kadhamilia?
 
Edo will remain instantly in our heart no matter what u say..gat dem wooo..!
 
Saa nyingine ujio wa aliyekuwa adui ni baraka kutoka kwa Mungu, pamoja na Mengi yaliyosemwa kuhusu Lowassa, ujio wake una impact kubwa kwenye upinzani:-

1. Ameondoa kigugumizi kilichokuwa ndani ya CCM kwamba kujiondoa ndani ya CCM ni dhambi. Baada ya yeye kuanza tuliona wengine wakifuata kama F.Sumaye.

2. Ujio wake umekisaidia Chadema kuongeza wigo wa majimbo ambayo yalikuwa kama yamemilikiwa na Wabunge fulani. Mfano Simanjiro, Monduli.

3. Kugombea kwake Urais kulisababisha taharuki ndani ya CCM na kuwafanya wasiamini kama watashinda uchaguzi lakini pia kuliongeza hamasa kwa wananchi ya kupiga kura. Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia nchi hii mgombea wa upinzani akipata kura nyingi na pia mgombea wa CCM akipata kura chache chini ya asilimia 60%.

Hayo aliyoyatoa mtoa mada ni kweli lakini kwa kuwa yamewakuta wao nadhani yatatoa elimu kwa wengine waliomo madarakani kuwa sheria ni msumeno unakata kotekote. Na sisi kama binadamu hatuwezi kujua kesho yetu itatukuta tukiwa wapi.

pia usisahau kukatwa kwake kumetoa fundisho kwa wanachama wake kuwa amna aliyejuu ya chama , ccm wamemkata fisadi na wameshinda
 
Mfumo mmbovu ndo tatizo!!!
Watz wana majonzi kila kona wakidhan mabadiliko yalishaa wafika?!!!!
Kuhesabu kura kwa tochi ya tecno cyo maendeleo..........
 
Kujenga makao makuu ya chama wameshindwa na ruzuku yote ile, iwe kuweka camera nchi nzima? Labda camera wapewe msaada, na wakipewa wale mchwa kina lema wataziacha bila kuuza?
kwani Ccm inejenga au imepora majengo
 
Back
Top Bottom