GE2025 Baba Levo: Zitto sio mpinzani na hatoweza kunidhibiti

GE2025 Baba Levo: Zitto sio mpinzani na hatoweza kunidhibiti

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Mtangazaji wa Wasafi FM, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, na mtia nia Ubunge Jimbo la Kigoma mjini Kupitia CCM, amekea vikali kauli za Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyoitoa kuwa Wasanii, Wachekeshaji na Watangazaji sio watu sahihi wa Kugombea Ubunge.

Baba Levo amesema kauli za Kiongozi huyo ni za Kibaguzi kwa Wana tasnia hizo, kwani zimezalisha ajira nyingi mno ambazo yeye akiwa Kiongozi kwa zaidi ya Miaka 15 ameshindwa kuzitengeneza.

Mimi nimwambie tu baba levo kwamba kwangu mimi amekwishapoteza sifs ya kupewa ubunge kwa sababu ya uchawa wake, maana yake ni kwamba hawezi tena kuisimamia au kuikosoa serikali hana ujasiri huo kwa sababu tunamjua ni mtu wa mapambio, amuache zitto ambae anajielewa. Na wasanii wengine msiingizwe kwenye mkenge na baba levo, huyo ni mchumia tumbo
UBUNGE JAMANI SIO LELEMAMA
 
Zitto alikuwa anajielewa sio sasa
 
Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Mtangazaji wa Wasafi FM, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, na mtia nia Ubunge Jimbo la Kigoma mjini Kupitia CCM, amekea vikali kauli za Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliyoitoa kuwa Wasanii, Wachekeshaji na Watangazaji sio watu sahihi wa Kugombea Ubunge.

Baba Levo amesema kauli za Kiongozi huyo ni za Kibaguzi kwa Wana tasnia hizo, kwani zimezalisha ajira nyingi mno ambazo yeye akiwa Kiongozi kwa zaidi ya Miaka 15 ameshindwa kuzitengeneza.

Hawa wote ni "wataalam" Acha walogane, unaambiwa hapo Buzeba zeba bei ya radi imeshuka hadi buku jero ili kuua mtu mmoja
 
Siasa ni mahesabu,huyu ameanza kutanguliza ya mbele kabla hajafika popote pale! Asipokua makini atapoteza pambano kabla hata ya refa wa mchezo hajapiga filimbi.
 
Uongozi nimukuja kugundua ni ujanjajanja tu Wala sio weledi kama nilivofundishwa kwenye somo la Uraia shule ya msingi na Mwalimu ODOLIA.
 
Zitto alipofikaga bei, around 2012/2013, nilijua tuu huko mbele atakuja kuonekana mpuuzi. Atadharaulika mpaka na wajinga wasiokuwa na shule kichwani. Utabiri wangu umetimia. 😁
 
Hili Jimbo lipo kimkakati kwa CCM kuachi upinzani ili kubalansisha Ubunge kuonekana uchaguzi huru

Hii ni kuokoa Ile ya COVID-19
Jimbo la Kigoma mjini ni jimbo la upinzani kama ilivyo Arusha mjini, Moshi, Mbeya mjini, hutokea wakati mwingine majimbo haya yakaangukia chama tawala, lakini ukweli huo uko wazi tangu tumeanza uchaguzi wa kwanza mwaka 1995.
 
CCM, Chama Cha Maukuli, kipande Cha mnofu Cha dhuluma dhidi ya Tanganyika/TANZANIA anakiwinda.
 
Back
Top Bottom