Baba haoni kuku mpaka awashe taa

Baba haoni kuku mpaka awashe taa

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,270
Ilikuwa mchana kama saa nane hivi. Niliingia kwenye banda langu la kuku wa kienyeji kukagua hali zao. Nikagundua kuku wengi walikuwa wanashambuliwa na funza kwenye mzunguko wa macho yao. Dawa niliyozoea ya kuwaondoa funza ni kupaka mafuta taa kidogo kwenye mzunguko wa macho. Basi haraka nikamwita mtoto wangu wa miaka mitatu aniletee taa ya chemli nitoe huko mafuta kidogo. Akaniletea na kuondoka zake. Kwa mbali nikamsikia akiwaambia wenzake:'Baba haoni kuku, ameniambia nimpelekee taa!
 
teh teh teh kwani huwa unavaa miwani?
 
Utitiri mzee co funza.. Jirekebishe kabla hajafika badili tabia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom