Baba hana haki ya kuishi na Mtoto wake chini ya Miaka Saba?

Prezdaa Shaco

Member
Sep 3, 2013
46
8
Naombeni Msaada wenu,

Nimempeleka ustawi wa jamii mwanamke alienizalia mwanangu ili ikiwezekana anipe mwanangu nimlee mwenyewe kwani mazingira anayoishi nae mwanangu hayaniridhishi. Lakini Ustawi wa jamii inaonekana ipo kuwatetea wanawake na sio wanaume kwani licha ya kuwaambia naitaji nimlee mwanangu mwenyewe ili kumuokoa na mazingira hatarishi anamoishi lakini walimtetea mwanamke kuendelea kukaa nae mtoto na mimi niendelee kupeleka matumizi.

Roho inaniuma kwani nilimwandikisha English Medium amesoma miaka miwili hana alichojua kuandika wala kukisoma kwakua akirudi nyumbani hamna wa kumsimamia.

Naombeni msaada nitumie njia ipi niweze kumpata mtoto kabla ya kufikia miaka saba kwani kwa sasa ana miaka mitano lakini naona kama anaharibikiwa mana mama ake amemtoa private amempeleka public school na nimeenda ustawi wa jamii pia haikuwa msaada kwangu.
 
Acha dharau ya public school.

Ukienda ustawi weka fact za usalama wa mtoto,kazi ya mwanamke ni hatarishi kwa tabia ya mtoto Na kwa vile mkevyupo duni mtoto anapata udumavu wa akili na ukuaji.

Ila upambane sana ikishindikana wawaruhusu muende mahakamani.
 
Nenda mahakamani ukiwa umeandaa ushahidi wa madai yako na pia mazingira unayoishi wewe yawe yanakubalika kulea mtoto, uwe na msaidizi wa kike kama make au mfanyakazi wa ndani atakaekua tayari kwenda mahamani kuileza mahakama kuwa atamlea huyo mtoto

Suala la shule pengine ni vizuri kuwa mkweli, maana haingii akilini ulipe ada shule ya private na risiti uwe nayo na wewe ndio unatoa huduma za mtoto kwa mujibu wa sheria halafu mama ahamishie mtoto shule ya public. Logic ni ipi? Amehamisha mtoto ili amkomoe nani? Si kwamba kashindwa kulipa ada?
 
WANAHARAKATI WANATUHARIBIA NCHI...

MTOTO NI WA BABA...ILA HII INAYOITWA USTAWI WA JAMII...NI USTAWI WA MWANAMKE...WANATUMIA MTOTO KAMA CHANZO CHA MAPATO YAKE NA FAMILIA YAKE...
 
mwanamke alienizalia mwanangu ili ikiwezekana anipe mwanangu nimlee mwenyewe kwani mazingira anayoishi nae mwanangu hayaniridhishi.

Hajakuzalia wala mtoto sio wako ni WENU unless mlikubaliana awe mbeba mimba tu na kama ingekua hivyo asingekataa kukupa mtoto mara baada ya kujifungua.
 
Back
Top Bottom