Baba halali hapa ni yupi :

Baba halali hapa ni yupi :

Wakuu Bwana asifiwe,

Ni hivi kuna mwanamke mdogo wangu alikuwa anatembea nae miaka mitano iliyopita , sasa mara mwisho kutembea nae mwaka 2015 ,na walikuwa wanakaa kota za jeshi kipindi iko,

Jamaa wakapotezana na huyo mwanamke tangu kipindi iko, hata namba uyo mwanamke akawa kabadilisha, na pia akaolewa.

Sasa huyo mwanamke wiki iliyopita alionanaa na mtu ambae wanajuana na Mdogo wangu, huyo mshkaji akampatia namba ya mdogo wangu huyo mwanamke , wakawasiliana na mdogo wangu, katika story Yule mwanamke anamuambia mdogo wangu kuwa mwenzio baada Ya kusex nawewe siku ile mwaka 2015,baada ya wiki nikaona mabadiliko na nilivyoenda kupima ikawa ni mimba,

ila nilishindwa kukuambia sababu we mme wa mtu na mkeo alikuwa mtata, halafu namimi pia nilikuwa na mchumba wangu kipindi kile, kwaiyo mimba nilimpa Jamaa ambae alinioa na akawa mme wangu

Ila kiukweli mimba ilikuwa yako na mpaka mama yangu anajua ilo, na cha kusikitisha zaidi huyo mme wangu ameshakufa, na mpka mama yangu kipindi chote alikuwa anajua kama mimba ilikuwa yako na mtoto ni wako sio wa mwanaume yule ambae kanioa , ila aliniambia iwe siri sana,

Sasa mdogo wangu akamuambia sawa, mi kwasasa nipo Zambia , ngojea nikirudi nije nimuone mtoto

Ila alimtumia picha ya huyo Mtoto katika twitter, dogo anasema ni kama Kweli amefanananae huyo mtoto,
SASA HAPO wana Jf imekaaje Jamaa akirudi akija kumuona mtoto , na akajiridhisha kweli amefanana nae , sasa atafanyaje ili achukue damu yake ilhali kadi ya clinic na cheti cha kuzaliwa kinasoma jina la baba mwingine ambae ni marehemu Kwa sasa (R. I. P)

Je, anaweza akabadili cheti cha kuzaliwa cha uyo mtoto? na je taratibu na gharama za kupima DNA zipoje Kwa Tz ili ajiridhishe zaidi.

Muandiko mbaya tusameheane.

Ngoja waje wataalamu wa mambo..
 
DNA kwanza huo upuuzi wa vyeti cjui majina utafata
 
Kubadili jina si tatizo, ajiridhishe kwanza Kama mtoto ni wake.
Loss report, kwamba birth certificate is lost.
Pata kingine.
Au ata hati ya kiapo kubadili majina.
Baba halali ni baba yeyote: iwe biological au wa kufikia.
Nina jirani yangu mkewe ana mtoto ila inside news ni kwamba baba halali alikuwaga anapiga simu kumjulia hali na kuleta zawadi kwa kificho.
Mtoto anafanana na mama, ni mweusi kama mume wa ndoa.
Siri sirini: ndiyo maana wanawake wengi hawapendi kitu DNA
Anayejua baba wa mtoto ni mama tu!
Wanawake heshima kwenu.
Akil kumkichwa
 
Ana mke na watoto then bado anamhitaji huyo wa nje ili iweje?

Tupe story ya upande wa pili kwa nn anataka amhalalishe huyo mtoto mpaka majina? Kuna kitu nyuma ya pazia ambacho huyo ndugu yako anakitafuta.

Na huyo mwanamke alimpa taarifa ndugu yako ili iweje? Yani alikuwa anamjulisha tuu aujue ukweli ama amemjulisha kwa lengo la kupata masaada wa malezi?
 
Umenena vyema.
 
kimbembe kipo kwenye ndugu wa marehemu, vyovyote watakavyo react inabidi muwe wapole maana inauma
 
Ana mke na watoto then bado anamhitaji huyo wa nje ili iweje?

Tupe story ya upande wa pili kwa nn anataka amhalalishe huyo mtoto mpaka majina? Kuna kitu nyuma ya pazia ambacho huyo ndugu yako anakitafuta.

Na huyo mwanamke alimpa taarifa ndugu yako ili iweje? Yani alikuwa anamjulisha tuu aujue ukweli ama amemjulisha kwa lengo la kupata masaada wa malezi?
Sidhani Kama nia ni msaada wa malezi. Nadhani alikuwa anafeel guilty mtoto kutomfahamu baba halisi wakati yupo hai. Anafanya hivyo kwaajili ya mtoto, ni vizuri kumfahamu mzazi wako no matter what happened.
 
Huko ni kuharibu saikolojia ya watoto tuu. Mtoto anajua baba ake alishakufa then leo unamwambia baba ako halali ni huyu. Kwanza ili iweje? Na itamsaidia nn huyo mtoto.

Cha msingi huyo jamaa kashajua ni mtoto wake basi inatosha, sioni haja ya kumwambia mtoto.

Mmh haya
 
Kabla ya DNA wamwangalie kwa macho ya kawaida tu, mbona mara nyingi huwa yana majibu sahihi
Macho kama hayaridhiki ndo utumie DNA.
 
Back
Top Bottom