Baba aua watoto wake wanne, naye ajinyonga.

Baba aua watoto wake wanne, naye ajinyonga.

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,030
Reaction score
59,684
EVANCE Damiani (43), mkazi wa kijiji cha Gekrumu, wilayani Karatu, Arusha amewaua watoto wake wanne na yeye mwenyewe kujiua kwa kile kinachodaiwa wivu wa mapenzi.Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa kuamkia juzi nyumbani kwa Evance baada ya kukosana na mkewe wakituhumiana kusalitiana na baadaye mkewe kukimbia kusikojulikana.

Evance baada ya kuona mkewe amekimbia, alichukua shoka na kuanza kuwacharanga watoto wake: Theophil Damian (11), Ritha Damiani (9) na mapacha Jigimu Damiani na Theodore Damiani (6) na kuwaua!
Baada ya kuwaua watoto hao na yeye akajinyonga na kufariki na maiti zote hizo kukutwa asubuhi nyumbani hapo.
Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza uchunguzi wa chanzo cha mauaji hayo unaendelea ikiwa ni pamoja na kumtafuta mwanamke huyo aliyekimbia.
Habari zaidi kutoka kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo zinasema kwa muda sasa Damiani alikuwa na mzozo na mkewe hivyo kusababisha ugomvi wa mara kwa mara nyumbani hapo.
source:dullonet
 
Back
Top Bottom