Baba Askofu Gwajima, Mwenyezi Mungu anakuona

Baba Askofu Gwajima, Mwenyezi Mungu anakuona

Maandiko Matakatifu, kwa Dini zote zinazojulikana Duniani, yanasema usichukue HAKI YA MWINGINE NA KUIFANYA KUWA HAKI YAKO.

Shughuli za uchaguzi zinazoendelea zimetuweka njia panda wale wenye Imani kamilifu sawa sawa na wenye Imani haba. Pamoja na kwamba mie sio mjuzi wa Biblia, lakini ninaelewa kwamba Askofu ni mtu mkubwa sana katika muundo wa kanisa, kwa dhehebu lolote hapa Duniani. Askofu anapaswa aishi kwa mifano ya kumpendeza Mungu, kiimani hata kijamii. Askofu hapaswi kupokea wala kutoa kilicho haramu machoni pa Bwana. Haijalishi ni kitu gani.

Uchaguzi wa Kura za maoni katika Chama cha Mapinduzi umefanyika na kupita, walioshinda kihalali wapo waliotangazwa na majina yao kurudi ili kuendelea na mchakato wa uchaguzi, lkn pia wapo walioshinda na majina yao hayakurudi. Wapo walioshindwa na majina yao kurudi wakiendelea na mchakato wa uchaguzi, lkn wapo walioshindwa na safari yao kuishia kwa wajumbe.

Mojawapo ya majina ya walioshindwa lkn majina yao yamerudi ni Askofu Gwajima. Kushindwa kihalali kwa Baba Askofu Gwajima, ilikuwa ni maamuzi halali ya Wajumbe wa CCM Jimbo la Kawe walioona kwamba Askofu Gwajima hawezi kuwa Mwakilishi sahihi wa wana Kawe. Pengine waliona haifai kuchanganya Dini na Siasa kama tunavyofundishwa siku hizi. Wakampa kura Mgombea waliedhani anafaa, akashinda.

Hata hivyo waliomtaka Askofu Gwajima wakaona walichokifanya wajumbe wa Kawe ni Ujinga, wakampa ushindi usio wake ili aendelee na mchakato wa uchaguzi. Askofu bila haya wala aibu akachekelea kupokea kisicho halali kwake na machoni pa Bwana. Hapa ndipo ilipo njia panda ya Imani.

Askofu Gwajima anajisikiaje kupokea kilicho haramu na kisicho chake? Ni maandiko gani yaliyomwelekeza Baba Askofu kukubali kupokea haramu? Hii ina maana gani kwake, kanisa lake na Mungu wetu? Kama Baba Askofu anaweza kutenda haya, vipi kwa wale wasio na Dini?

Kwenye Siasa hasa siasa za Afrika, mara nyingi kuna udanganyifu mwingi hasa pale inapotokea aliyekuwa na mamlaka anapoelekea kupoteza ushindi. Mara nyingi huwa mambo yanavurugwa na mshindwa kuwa mshindi, huku mshindi akiwa mshindwa. Baba Askofu atakuwa tayari kupokea matokeo ya kushindwa na kusimama kwenye ukweli ama atakuwa tayari kupora ushindi usio wake kwa mara nyingine?

Nafsi ya Baba Askofu inasema nini katika hilo?

Maswali ni mengi.

Kama ikitokea Baba Askofu atashindwa kihalali, atakuwa tayari kuyapokea matokeo kwa jinsi yalivyo? Bila shaka ni suala la kusubiri na kuona.

Baba Askofu, Mwenyezi Mungu anakuona.
Ndipo ujue Gwajiboy ni mwabudu lucifer! na wote manaojipeleka kwenye lile pagala mko safarini kwenda kwa lucifer
 
Yusuph alkuwa waziri mkuu na alimtumikia Mungu na watumishi wengi kwenye Biblia walikuwa viongozi wakubwa na walimtumikia Mungu why Gwajima ashindwe achen kukariri maisha we bado uko kwenye zama za ujinga na upumbavu
Msichanganye mambo jamani.Nipe maandiko yanayo onyesha kwamba Yusufu alikuwa Kuhani au hata mwalimu wa torati.Yusufu alikuwa msaidizi wa Pharaoh kiutawala,so he was a political figure,infact kwa leo naweza kusema angekuwa Waziri Mkuu.Hata hivyoo,mbona unasahau kwamba Mungu amesema zile zilikuwa nyakati za ujinga na sasa ameamuru tuishi kwa misingi ya Agano Jipya?Naomba ukweli wa neno la Mungu uheshimiwe,nao ni kwamba huwezi kutumikia mabwana wawili,kwa kuwa utamuacha huyu na kuandamana na huyu.Gwajima ni tapeli wa Injili na ukweli utabaki huo.Msichakachue Injili kwa tamaa zenu za mwili.
 
Nagundua tatizo la watu wengi Hawana Maarifa ya kutosha na Udini umewakaa kwenye vichwa vyao ,Wamejaa mazoea TU Gwajima Yuko Sahihi kabisa
Kwa muktadha wa Kimungu mkuu,Gwajima hayuko sahihi na hii imetuhakikishia kwamba kweli sio mtumishi wa Mungu,ni mchumia tumbo na tapeli wa Injili.Watu wasichanganye mambo na tunaomba ukweli wa neno la Mungu uheshimiwe,nao ni kwamba huwezi kutumikia mabwana wawili,kwa kuwa utamuacha huyu na kuandamana na huyu.Gwajima ni tapeli wa Injili na ukweli utabaki huo.
 
Back
Top Bottom