Baba anataka kuniondoa kwenye urithi na anawapendelea binti zake

amita bacha

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Posts
180
Reaction score
411
Ndugu zanguni kwenye maisha tunapitia mengi kila mtu anayo yale aliyoyapitia lakini sidhani kama kuna aliyeyapitia kama haya ninayoyapitia mimi kiukweli inauma na kusikitisha sana .

Baba yangu kwa muda mrefu amekuwa akiwapendelea watoto wa kike na hiki kitu ni kibaya kinajenga matabaka na chuki kwenye familia.kwa Nyakati tofauti amekuwa akiwasikiliza binti zake kiufupi ameshikwa masikio na wanaye wa kike na wasiwasi atakuwa amerogwa au kawekewa zindiko sababu mimi hanijali na haonyeshi mapenzi kwangu mimi.Kanifukuza nyumbani kama sio damu yake hivi kweli nitakuja kumsaidia kweli huyu mzee ?

Lakini binti zake wanaishi kwa amani sawa kama hio haitoshi nimepata tetesi anataka aniondoe kwenye list ya watakaorithi Nyumba na mali kiukweli nimeumia baada ya kusikia tetesi hizi huu si uonevu dhahiri na upendeleo uliokithiri?

Hao binti si wataolewa na kuishi kwa waume zao sasa mimi kama mwanaume ilibidi ndio niwe na haki na mali hizo lakini cha kushangaza nasikia anataka kuondoa jina langu.Sasa mimi nitafanyaje endapo ikitokea akifa na ni haki yangu .

Nifanyaje unaweza kuweka pingamizi mahakamani ndugu zanguni?

Na kuhusu kupendelea binti zake kuliko mimi kwanini wakati mimi ndiye nitakaye mzika..
 
Mzee machale yamemcheza kuwa wewe ni mtoto wakubabikizwa kwahiyo anakukataa mapema
 
Kijana tafuta mali zako..
Kaishi maisha yako hukoo we urithi waachie
Umekazana kuwaza urithi ndo mana akili zimelala na mdingi kaamua kukukomesha
Siku utatakiqa kuwa baba nawe pia iwaachie urirhi wanao.. Kama akili ndo hizo utawaachia nini?
Katafute maisha yako.
Mi hapa mtoto wa kike sina hata huyo baba wala mama.. Sina urithi hata wa kigoda..lakini bado naiona njia ya kutokea..vipi wewe huoni lolote mbele?
 
Ndugu zanguni kwenye maisha tunapitia mengi kila mtu anayo yale aliyoyapitia lakini sidhani kama kuna aliyeyapitia kama haya ninayoyapitia mimi kiukweli inauma na kusikitisha sana .

Baba yangu kwa muda mrefu amekuwa akiwapendelea watoto wa kike na hiki kitu ni kibaya kinajenga matabaka na chuki kwenye familia.kwa Nyakati tofauti amekuwa akiwasikiliza binti zake kiufupi ameshikwa masikio na wanaye wa kike na wasiwasi atakuwa amerogwa au kawekewa zindiko sababu mimi hanijali na haonyeshi mapenzi kwangu mimi.Kanifukuza nyumbani kama sio damu yake hivi kweli nitakuja kumsaidia kweli huyu mzee ?

Lakini binti zake wanaishi kwa amani sawa kama hio haitoshi nimepata tetesi anataka aniondoe kwenye list ya watakaorithi Nyumba na mali kiukweli nimeumia baada ya kusikia tetesi hizi huu si uonevu dhahiri na upendeleo uliokithiri?

Hao binti si wataolewa na kuishi kwa waume zao sasa mimi kama mwanaume ilibidi ndio niwe na haki na mali hizo lakini cha kushangaza nasikia anataka kuondoa jina langu.Sasa mimi nitafanyaje endapo ikitokea akifa na ni haki yangu .

Nifanyaje unaweza kuweka pingamizi mahakamani ndugu zanguni?

Na kuhusu kupendelea binti zake kuliko mimi kwanini wakati mimi ndiye nitakaye mzika..
Wewe jamaa mbona unapenda sana kugombania urithi tafuta mali zako Shangazi wanatishia kuniloga na wanashirikiana na polisi kunimaliza - JamiiForums
 
Chai,wewe Jamaa naona umejikita kutuletea chai,lakini ni mambo yanayotokea katika Jamii zetu,unayoyaongea hayana uhalisia lengo lako Jamii upate somo
 
Yaani uweke pingamizi kwa mali ya Mwingine?

Wewe cha kufanya kanunue shamba mahali, jenga Nyumba kali, alafu weka pingamizi asmilikishwe Mwingine kwa sababu hiyo sasa ndio itakuwa mali unayomiliki.
 
Na kuhusu kupendelea binti zake kuliko mimi kwanini wakati mimi ndiye nitakaye mzika.

Aliyekwambia baba yako atakufa kabla yako ni nani? Mali aliyochuma baba yako ni mali yake na anakila haki ya kuamua ni nani atakaye faidika na mali yake akiwa hai na hata baada ya kifo chake.

Inavyoelekea kutokana na maelezo yako, baba yako hana imani na jinsi unavyoendesha maisha yako na inavyoelekea wewe ni mtu mzima lakini huna msaada kwake na inaelekea ni tegemezi na ndio maana hakuthamini na anakufukuza nyumbani kwake uende ukatafute maisha yako. Inaelekea hao dada zako wanajitambua kuliko wewe na ndio maana baba yako anawathamini.

Kama kabla ya kifo chake baba yako ataandika wosia wake na wewe kutokuwemo hata uende mahakamni ni kazi bure huwezi kupata kitu.

Wewe ndio aina ya vijana wanaoombea wazazi wao kifo ili waweze kurithi mali, badala ya kujishuhulisha na kuchuma mali yao wenyewe!!
 
ni kweli kijana nimekuondoa kwenye urithi
kwa sababu hujakizi vigezo
1.wewe ni mvivu miaka 48 bado tu upo kwangu,hadi dada zako wanakushangaa
na hii ni notice kesho asubuhi uwe umeshahama hapa nyumbani.
_
2.unagombana na shangazi zako
3. tabia zako tumizichoka
4. sipendi tu kulumbana na mwanagu huku mtandaoni ila hakuna namna..
 
Anafanya kazi bure tu kisheria mtoto wa kike au watoto wanapata 1/20 ya mali za marehemu mtoto wa kiume anapata fungu kubwa kaabisa we mwache ajifurahisue.
SHERIA ZA MIRATHI ZIPO NA ZINAMKANDAMIZA MTOTO WE KULA ZAKO BATA.
(Ila fanya fanya utafute na vyako acha uboya utamegwa)
 
ni kweli kijana nimekuondoa kwenye urithi
1.wewe ni mvivu miaka 48 bado tu upo kwangu,hadi dada zako wanakushangaa
na hii ni notice kesho asubuhi uwe umeshahama hapa nyumbani.
_
2.unagombana na shangazi zako
3. tabia zako tumizichoka
4. sipendi tu kulumbana na mwanagu huku mtandaoni ila hakuna namna..
Unaambiwa yesu anayo 2000 na zaidi lakini hataki kutoka kwa baba ake😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom