Baba amuua kijana aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti yake

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
1,968
2,000
Wakuu habarini..

Ni jana mapema, tuliitishiwa kikao cha dharura hapa ofisini baada ya Polisi kuja kumuulizia mmoja kati ya mzee mtu mzima aliekuwa katika kitengo fulani hapa ofisini. Tulichosimuliwa-

Huyu mzee ana mtoto wake wa kike ana miaka kama 12 au 11 hivi, na anasoma hapa mkoani Iringa Mjini, katika shule moja ambayo sitapenda kuiweka wazi. Huyu binti alikuwa na boyfriend mwenye miaka 23 hivi na taarifa tulizopewa ni kuwa huyu jamaa siku ya Wasafi Festival hapa mkoani kama week 1 na nusu hivi limepita, marehemu alimtorosha binti huyo wa miaka 12 au 11 hivi akamfanya mke wake kwa siku 3 ikiwepo kwenda nae huko Wasafi Festival.

Siku ya 3 baada ya mzazi kutafuta bila mafanikio, huyo binti alirudi nyumbani bila maelezo yaliyoeleweka mzazi akambamiza sana huyu binti mpaka binti akasema ukweli basi mzazi (baba), akamfuata huyo kijana na kumpa onyo asiendelee kutembea na binti yake kwani binti yake ni mdogo na huyo binti kutokana na kuzidiwa na huba, akawa haudhurii hata shule muda wote anashinda kwa huyo kijana.

Siku ya tukio kijana kama kawaida alimchukua binti na kwenda nae kwake alipopanga ikiaminika kumfanya matusi.

Usiku wa saa 3 binti alirudishwa na huyo jamaa. Baba wa huyo binti alikuwepo ndani alipandwa na hasira kwamba kijana anapata ujasiri wa kumrudisha binti hadi nyumbani mlangoni tena anamnyonya mdomo (kiss) hapo hapo.

Basi baba akachukua kisu akakuta kijana amemuegemea binti kiasi fulani wanaongea, akamchoma visu sehemu ya shingoni na ubavu wa tumbo kijana akadondoka chini, na baba kuona ile hali akakimbia na mpaka sasa haijulikani alipo

Vijana tuwe makini sana wazazi wanaumia sana na hawa watoto nao kama hawatabadilika basi vifo vya namna hii havitakoma.
 

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,941
2,000
12 kwa 23, tena kaenda nae mpaka kwenye onesho la mziki?
Shida ipo kwao (baba) mtoto wa kike.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom