Baba amtoboa macho bintiye wa miaka 12 kisha naye kujinyonga

Baba amtoboa macho bintiye wa miaka 12 kisha naye kujinyonga

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,603
Reaction score
22,717
Mkazi mmoja aishiye katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha Bushemba,Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera anayefahamika kwa majina ya Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) amejinyonga hadi kufa (Kama picha zinavyoonesha.

Sababu iliyopelekea kifo cha Baba huyo ni baada ya huyo Baba kumpiga mtoto wake wa kumzaa. Inasemekana kuwa alimpiga na kumjeruhi kichwani kwa fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mtoto huyo anafahamika kwa jina la Agripina Godfrey (12) anayesoma Darasa la Kwanza ktk S/M Ilambika.

Sasa kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…
Hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kata kata kumfungulia Mlango.
Basi Mama akaondoka kujiweka sehemu.

Baba yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo mtoto aliyeonekana kama ndo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa "Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba yake aanze kumpiga saana! Mpaka kumuumiza vile.

Sasa damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi na kuanza kuimimina kwenye jeraha kichwani(hiyo nyeupe kwenye Picha)

Basi mtoto alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba akaandika kijibarua haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo vingine ambavyo huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika kwenye Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe. Mtoto alipelekwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.

Maelezo haya na Picha nimepewa na Afisa Mtendaji Kata ya Buganguzi Bwana Wilson Dickson.

Credit; Sweetbert Rwabukambara
 

Attachments

  • babanew.jpg
    babanew.jpg
    24.7 KB · Views: 9,235
  • mtoto picha.jpg
    mtoto picha.jpg
    90.6 KB · Views: 13,959
Pole sana Agripina, umepata ulemavu lakini hutakuwa peke yako wapo wasamaria wema walioguswa na unyama uliofanyiwa, Mungu yunawe
 
Utaisha siku ambapo tutaanza kuyatambua magonjwa ya akili na kuyafanyia kazi. Mtu ana depression ila anajichukulia poa tu

Hata tukianza kuyatambua sidhani kama utaisha ila unaweza ukapungua kwa kiasi kidogo.

Na hivi kwenye haya maduka yetu ya dawa baridi antidepressants zinauzwa kweli?
 
Watu wanaishi na matatizo ya akili. Hapana budi kwamba mtu akionekana anatabia za ajabu ni vyema kutoa taarifa kunakostahili. Mara nyingine matatizo ya akili siyo mpaka utembee bila nguo.
 
Ni kwa nn amefanya hivyo?? Kumtoboa binti mdogo jamani kama hvyo ana makosa gani??
 
Au aligundua labda kuwa sio mtoto wake , labda kabambikiziwa.???
 
Binadamu wengine ni zaidi ya wanyama kwa matendo yao.
 
Kuhalalisha na kumaliza ukatili ni vitu tofauti. Jamaa hakuweza kuhalalisha japokuwa hakuwa na akili timamu. Huoni kajihukumu mwenyewe?

Anafukuza mke and yet anafika home anamuulizia. That girl is way too smart manake alimjibu na baba akajigundua amechemka
Hata ingekuwa hivyo, bado hakuna sababu itakayoweza kuhalalisha huo unyama.
 
Kuhalalisha na kumaliza ukatili ni vitu tofauti. Jamaa hakuweza kuhalalisha japokuwa hakuwa na akili timamu. Huoni kajihukumu mwenyewe?

Hata sijakuelewa hapo.

Jitahidi uwe eloquent kidogo....
 
Watu wanaishi na matatizo ya akili. Hapana budi kwamba mtu akionekana anatabia za ajabu ni vyema kutoa taarifa kunakostahili. Mara nyingine matatizo ya akili siyo mpaka utembee bila nguo.

Huko kunakostahili ni wapi katika nchi hii?
 
Mmmhhh jaman jaman mweeee watu makatili kama hawa sijui wanamatatizo gan
 
Back
Top Bottom