Baadhi ya watumishi wapinga kuisoma ilani ya CCM

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,754
21,170
Baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wa Manispaa ya Ilemela mkoani hapa wamepinga agizo la kutakiwa kusoma na kuielewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020.

Wakuu hao wanadai kuwa agizo hilo linakiuka Katiba ya nchi kuhusu haki ya mtu kuchagua chama anachokitaka.

===================================

Mwanza. Baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wa Manispaa ya Ilemela mkoani hapa wamepinga agizo la kutakiwa kusoma na kuielewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020.

Wakuu hao wanadai kuwa agizo hilo linakiuka Katiba ya nchi kuhusu haki ya mtu kuchagua chama anachokitaka.

Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Leonard Masale kwenye mkutano na watumishi hao.

“Atakayeona hawezi kufanya hivyo, afadhali aache kazi kwa hiari yake badala ya kusubiri kutumbuliwa,” amesema Dk Masale.

Amesema hawezi kufanya kazi na watumishi wa umma ndani ya ofisi yake au manispaa ambao hawatekelezi yaliyomo kwenye Ilani ya CCM kwa kuwa ndicho chama kilichoshika Serikali inayotawala.

Pia, amewataka kuhakikisha vinafanyika vikao mara kwa mara vya watumishi wa kila idara, kuanzisha dawati la mafunzo kwa wenyeviti wa Serikali za mitaa na kubaini watumishi hewa.

Mtumishi aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, amesema baada ya kikao hicho kuwa agizo la kusoma Ilani ya CCM ni sawa na kuingilia uhuru wa watumishi.

“Kauli hii ni ya kibabe, ambayo kwa namna moja au nyingine inaingilia uhuru wa mtu kuamini chama akipendacho,” amesema mtumishi huyo.

Chanzo:
Mwananchi

2015 vyama vimenadi ILANI tofauti na hatimaye ILANI ya CCM ilikubaliwa na wengi. Uchaguzi umeisha sasa ni muda wa kutekeleza yaliyomo kwenye ilani iliyoshinda. Tuiunge mkono na kauli mbiu ni hapa kazi tu
 
Ni sawa tu, wasome waelimike. Wakumbuke kila wafanyacho ni reflection ya ilani ya chama kilichokabidhiwa dola.

Hata yale yasiyo kwenye ilani, hayatolewi na Mbowe wala Lowassa bali ni waliokabidhiwa kutawala
 
CCM wameanza kutafuta pakuchificha, ili waseme tulitaka kujenga viwanda ila watumishi wa serikali hawakufata ilani ya chama! watumishi wa umma wapo na miongozo yao, inatia kinyaa eti unaingia ofisini unakuta afisa utumishi anakamua Tabu La Kijani Badala ya Standing Orders, pia mie sioni link kati ya kusoma ilani na eti watumish kwenda kinyume na serikali, wao wajenge tu viwanda sisi tupo tayari kulipokea hilo
 
Njia bora ya kuahakikisha wanatenda sawa sawa na matakwa ya Chama, baada yakusoma ni kuwapa mtihani kuhusu ILANI ya chama na watakao shindwa uwe mwisho wa utumishi wao naamini hiyo itampa credit nyingi sana mkuu wa wilaya husika. Ikumbukwe kuwa ukipewa assignment ya kusoma ni lazima ufanye mtihani ili kuhakiki uelewa wako.
 
2015 vyama vimenadi ILANI tofauti na hatimaye ILANI ya CCM ilikubaliwa na wengi. Uchaguzi umeisha sasa ni muda wa kutekeleza yaliyomo kwenye ilani iliyoshinda. Tuiunge mkono na kauli mbiu ni hapa kazi tu

Joto Balaa,
Acha ukasuku wa kukariri jambo na kuanza kurirudiarudia pasi na kujua maana.
Hapa kazi tu maana yake si kulazimisha watu wakariri Ilani ya CCM wala siyo kuzuia vyama vya siasa visifanye siasa kwa kufanya mikutano ya ndani na nje wala kuandamana. Wala haina maana ya Rais au Mwenyekigoda wa CCM aendeshe nchi kwa kutofuata au kuvunja Katiba.Hakuna!
Hivi mpaka sasa hii Hapa Kazi Tu imewasaidia nini Watanzania na wewe ukiwemo? Maana mpaka sasa hata JPM anasema hela hazionekani eti watu wameficha kwenye magodoro wanazilalia. Lakini jana Gavana wa Banki Kuu Tanzania ameanza kupingana na Bosi wake kuwa hela zipo nyingi tu hivo hakun mdororo wa Uchumi na watu wasiwe na wasiwasi........!!!!! Lakini wakti huohuo kule Bukoba kwenye Maafa ya Tetemeko la ardhi, serikali ya CCM inatembeza bakuli kuchangiwa na watu ili iweze kupeleke misaada Bukoba. Sasa hiyo hela 1.x Bilioni wanayokusanya TRA kila mwezi tangia Novemba mwaka jana mpaka sasa iko wapi? Hii ni lugha gongana kati ya Rais na Gavana inayowachanganya watu wasielewe nini hasa kinaendelea hapa nchini kwa sasa....
 
Joto Balaa,
Acha ukasuku wa kukariri jambo na kuanza kurirudiarudia pasi na kujua maana.
Hapa kazi tu maana yake si kulazimisha watu wakariri Ilani ya CCM wala siyo kuzuia vyama vya siasa visifanya siasa kwa kufanya ikutano ya ya ndani na nje wala kuandamana. Wala haina maana ya Rais au Mwenyekigoda wa CCM aendeshe nchi kwa kuvunja Katiba.
Hivi mpaka sasa hii Hapa Kazi Tu imewasaidia nini Watanzania na wewe ukiwemo? Maana mpaka sasa hata JPM anasema hela hazionekani eti watu wameficha kwenye magodoro wanazilalia. Lakini jana Gavana wa Banki Kuu Tanzania ameanza kupingana na Bosi wake kuwa hela zipo nyingi watu wasiwe na wasiwasi........!!!!! Lakini wakti huohuo kule Bukoba kwenye Maafa ya Tetemeko la ardhi, serikali ya CCM inatembeza bakuli kuchangiwa ili ipeleke misaada Bukoba. Sasa ile hela 1.x B wanayokusanya TRA kila mwezi tangia Novemba mwaka jana iko wapi? Hii ni lugha gongana kati ya Rais na Gavana inayowachanganya watu wasielewe nini hasa kinaendelea hapa nchini kwa sasa....
Uzi huu una agenda moja kubwa. Watu wasome na kuielewa ILANI ya CCM. Sasa wewe umerundika mambo mengi kiasi kwamba umepoteza lengo la mleta mada. Watumishi wa umma wanaguswa haraka sana na ilani hiyo kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu katika kuhakikisha huduma za jamii kama vile maji, afya, elimu, miundombinu n.k. inaenda sambamba na jinsi zilivyoainishwa kwenye ilani hiyo ili 2020 iwe rahisi kupembua pumba na mchele. Umeelewa sasa
 
CCM wameanza kutafuta pakuchificha, ili waseme tulitaka kujenga viwanda ila watumishi wa serikali hawakufata ilani ya chama! watumishi wa umma wapo na miongozo yao, inatia kinyaa eti unaingia ofisini unakuta afisa utumishi anakamua Tabu La Kijani Badala ya Standing Orders, pia mie sioni link kati ya kusoma ilani na eti watumish kwenda kinyume na serikali, wao wajenge tu viwanda sisi tupo tayari kulipokea hilo
Standing orders sawa, acha afisa utumishi azipitie. Nakubali hilo lakini kumbuka ndani ya ilani imeelezwa idadi ya watumishi watakaoajiriwa katika kada tofauti kipindi hiki cha 2015-2020. Hivyo ni vizuri akaisoma na kuielewa ili anapoomba kuajiri watumishi ajue mahitaji na ukomo wake. Hilo la viwanda ni vizuri maafisa biashara wasome na kuelewa na washauri haraka iwezekanavyo juu ya uwezekano wa kuanzisha viwanda katika maeneo yao. Acheni porojo 2020 sio mbali. Tuchape kazi
 
Uzi huu una agenda moja kubwa. Watu wasome na kuielewa ILANI ya CCM. Sasa wewe umerundika mambo mengi kiasi kwamba umepoteza lengo la mleta mada. Watumishi wa umma wanaguswa haraka sana na ilani hiyo kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu katika kuhakikisha huduma za jamii kama vile maji, afya, elimu, miundombinu n.k. inaenda sambamba na jinsi zilivyoainishwa kwenye ilani hiyo ili 2020 iwe rahisi kupembua pumba na mchele. Umeelewa sasa
Mkuu tenganisha siasa na taaluma za watu.

Anaetakiwa kuisoma hiyo ilani na kuitekeleza ni viongozi wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom