Sijajua kama nitakuwa nimeenda kinyume na mapenzi,huruma,mtazamo au mawazo ya walio wengi ila hata mimi kumbuka ni binadamu niliye na uhuru wa kutoa mawazo au kushauri jambo ambalo katika hisia zangu naona haliko sawa
Jambo lenyewe ni hivi
Katika maisha yangu napenda sana kujitolea kuwasaidia watu mbalimbali katika ushauri lakini pia ninajitahidi kurushia visenti vya mia mbili,mia moja,elfu moja na kadhalika katika bakuli za watu wanaosimama na bakuli njiani wakihitaji msaada ili wapate kula kutokana na wao kutokuwa na uwezo wa kutafuta mkate kwa uwezo wao kwa sababu ya uwezo wao duni au ulemavu walionao katika viungo vya miili yao napenda kuwatia moyo na kuwaambia ya kuwa Mungu wetu si kiziwi wala kipofu ya kuwa hawaoni au hasikii kilio chenu bali anaona na kusikia kilio chenu ndo maana mpaka leo mpo hai hivyo msife moyo Mungu anawapigania kila saa
Mimi binafsi:
Kwa upande wangu mimi kila nipitapo njiani na kumkuta mtu anaomba msaada na ni mlemavu wa viungo vyake huwa najikuta naishiwa nguvu na kulengalenga kwa machozi ya huruma na shida inayokuja ni kuwa namna gani nitoe msaada na sijui kwa upande wangu nina tatizo gani maana huwa naona aibu sana kutoa hela huku watu wananiona na huwa najilazimisha kutoa kwani huruma yangu uwa inazidi sana pindi nimwonapo mtu wa namna hii naombeni ushauri au mbinu mnayotumia wenzangu kuwapa msaada hawa watu bila ya mimi kuona aibu maana muda mwingine huwa napita kabisa lakini najifikiria mbele kisha nageuza na kufika kuiweka ile hela kwa hali ambayo ni ya kujilazimisha na ikitokea nipo njia moja na mtu tunayefahamiana naye hapo ndo huwa nafeli yaani siweki chochote na naishia kujilaumu tu kuwa why sijaweka chochote????
Mapendekezo Yangu:
kwa hawa wahudumu wa walemavu hawa yaani waongozaji/wanasukuma baiskeli za hawa wahitaji basi wajitahidi kutafuta chombo ambacho ni kikubwa ili kusudi mtu anavopita awe na uwezo wa kudondosha bila hata ya kuinama wala kuogopa watu wengine ilikusudi anavotoa msaada wake asiogope maana akifika pale ni kuachia tu kuliko kuinama na kuiweka kwenye kikombe au mbinu zingine mbadala zitumike naamini wanaotaka kutoa msaada juu ya watu hawa ni wengi ila mazingira ya kutoa msaada sio rafiki
Dukuduku langu/hasira yangu /kero yangu/Jambo la kusikitisha juu ya hawa wasaidizi au wanaowatembeza hawa walemavu
Ukiangalia kwa jicho lingine hawa wasaidizi wameifanya hii huduma ya kuzunguka na walemavu kwenye baiskeli kama njia ya kuwaingizia kipato na si msaada tena kwani inavoonyesha familia yote ya hawa watu wanakuwa wanategemea riziki kutokana na kile kinachopatikana na kusaidiwa kwa mlemavu huyu hivyo ndugu zake kumfanya huyu mlemavu kuwa fursa na wao kushindwa kufanya shughuli zingine za kuwaingizia kipato zaidi ya kumtembeza mlemavu juani wakiomba msaada kutwa nzima
Naomba nieleweke wazi kuwa sio kila anayemwongoza mlemavu anakusudi hilo lahasha! Ila baadhi ya watu
Mfano;
kuna maeneo nilipita nikamwona kijana ambaye ana nguvu zote,mwili wake umekaa vyema kuwa anauwezo wa kujitafutia kwa nguvu zake au akawa na biashara yoyote ile na akayamudu maisha yake lakini cha kushangaza nimemkuta akimtembeza mtoto mdogo mwenye umri kati ya miaka 5 hadi 8 kwenye kibaiskel yaani wheelchair ambaye huyo mtoto ni mlemavu wa miguu
Swali la kujiuliza?
Je,yule kaka ameshindwa kweli kujihangaisha na kupata hela au chakula cha kumlisha mtoto mdogo kama yule?
Je,kama yule mtoto asingekuwa na ulemavu huo kwa ule umri wake angeweza kujitaftia ?
Je, hapo hatuoni kuwa baadhi ya watu wanaifanya hii shughuli kama njia ya kujipatia kipato kupitia hawa watoto walemavu?
Ombi langu kwa serikali:MNAPOZUNGUMZIA HAKI ZA WATU WALEMAVU IVI HUWA MNAMAANISHA NINI AU LENGO LENU LA KUWATAMBUA HAWA WATU NI LIPI HASA?
Mnaonaje kama serikali mkatafuta njia mbadala za kuweza kuwasaidia hawa watu yaani hawa watu ambao ni walemavu na hawana watu wa kuwasaidia kupata mahitaji yao ya msingi mkawaingiza katika mpango maalumu ili kusudi wawe wanasaidiwa kiasi fulani kila mwezi ambacho kitakuwa kinawasaidia kukidhi mahitaji yao ya kila siku kuliko kuwaachia mashirika binafsi na walezi pekeee?
Samahani na mniwie radhi kwa nilio wakosea ila ulikuwa ni mtazamo wangu tu!